Mimba za utotoni Misungwi zaongezeka

Mimba za utotoni Misungwi zaongezeka

Nyanswe Nsame

Senior Member
Joined
Jul 9, 2019
Posts
165
Reaction score
181
Mimba za utotoni Misungwi zaongezeka

IMEBAINIKA kuwa wilaya ya Misungwi katika kipindi cha miezi mitatu ya Januari hadi Machi mwaka huu kiwango cha wanafunzi na watoto wadogo kupata ujauzito imeongezeka.

Katika kipindi cha miezi mitatu, wilaya hiyo jumla ya wanafunzi na watoto wadogo wamepata mimba jambo ambalo limetajwa ni hatari kwa maendeleo ya ustawi wa jamii.

Pia inaelezwa katika kipindi cha rikizo ya maambukizi ya homa kali ya mapafu (COVID 19) kimechangia wanafunzi kupata mimba kutokana na kuwa huru.

Hayo yameibuliwa leo wakati wa kampeni ya amsha hali ya kuwapa stadi ya utayari wa kurudi shuleni walimu wilayani humo pamoja na namna ya kufundisha na kurudi darasani baada ya rikizo ya COVID 19.

Mafunzo na elimu hiyo inatolewa na Shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za wanawake na watoto la KIVULINI.

KIVULINI inaendesha oparesheni hiyo kwa walimu wa shule za msingi na Sekondari katika wilaya za Misungwi, Ilemela, Kishapu na Tarime.

Pia shirika hilo linaenda mafunzo kwa walimu namna ya kujikinga na COVID 19 mara ya shule kufunguliwa jumatatu ijayo.

Shirika hilo pamoja na kutoa mafunzo hayo, pia linatoa matenki ya kuhifadhia maji yenye ujazo wa lita 1000 kwa baadhi ya shule zenye uhitaji katika wilaya zilizochaguliwa.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Yassin Ally amesema katika kipindi cha miezi mitatu ongezeko la mimba za utotoni limeongezeka kwa kasi.

Yassin amesema, kwa mjibu wa dawati la jinsia la Polisi wilayani Misungwi walizo toa zimeonesha idadi hiyo na kwamba itahitajika oparesheni maalumu ya kuwapima mimba wanafunzi wote.

Amesema itahitajika oparesheni maalumu baada ya mimba za utotoni kuongezeka kwa kasi kubwa ili kuwabaini wenye ujauzito.

"Misungwi ni moja ya Wilaya ambayo tumefanya kazi kubwa katika kampeni ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni, baada ya kutoa elimu Misungwi utoaji wa taarifa ilikuwa kubwa.

"Ukiangalia miezi mitatu tu minba 46 hi inaonesha nilazimisha lifanyike opareshe ya kubaini kuwapima mimba ili tupate takwimu halisi ya wanafunzi wenye mimba," amesema Yassin.

Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Misungwi Diana Kuboja amesema wamejipanga kuhakikisha tahadhari inachukuliwa katika shule zote dhidi ya ugonjwa huo.

Amesema maandalizi ya kuwapokea wanafunzi wote katika wilaya hiyo yamekamilika na kwamba wamejiwekea mikakati ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.

By Charles Charles

Mwisho
 
Back
Top Bottom