DALILI ZINAWEZA ZIKATOFAUTIANA KATI YA MMOJA NA MWENGINE
Kwa ufupi ni kama ifuatavyo.
1) Mwili kuchoka sana
Hii ni kutokana na kuwa, baada ya kupata ujauzito mwili wa Mama hujitahidi kupeleka mahitaji ya msingi kwa kiumbe aliyeko tumboni. Endapo wako viumbe wawili au zaidi tumboni na uhitaji nao unakuwa mkubwa hali inayo pelekea Mjamzito kuchoka sana.
2) Kukithiri kwa maudhi madogo ² ya mimba(morning sickness) .
Hayo maudhi ni kama vile KICHEFU ² na KUTAPIKA.
3) Kuongezeka sana kwa uzito hasa katika miezi mitatu ya mwanzo.
4) Tumbo kuonekana kuwa kubwa kuliko umri halisi wa mimba .
Dalili hizo ni zile ambazo anaweza kuzihisi mama mwenyewe, ila kuna ambazo mpaka mtaalamu afanye vipimo.
Nimeeleza kwa ufupi tu, wengine wanaweza kuongezea zaidi.