Mimba Inayoua Mtoto Bila Mama Kujua, Siri Inayofichwa Na Damu Yako...🩸
Wanaume na wanawake wengi wanaishi bila kujua kundi la damu zao – hadi wanapopoteza mimba ya pili kwa maumivu makali yasiyoeleweka…
JE..?
—Unajua kundi lako la damu?
—Na la mwenza wako je?
—Ni RHESUS POSITIVE au RHESUS NEGATIVE?
Ili unielewe vizuri Tuanzie hapa....
🔬 Rhesus Factor ni nini..?
Ni protini inayopatikana kwenye chembechembe nyekundu za damu. Watu wenye protini hii huitwa Rhesus Positive (Rh+).
NA...
Wale wasio nayo huitwa Rhesus Negative (Rh–). Hii ni kwa Makundi yote ya Damu (O, A, B na AB)
(Tatizo linatokea pale mwanamke aliye Rh– anapopata Mimba na Mwanaume aliye Rh+).
👶 Mimba ya kwanza hupita salama... Lakini ya pili?
↳ Katika mimba ya kwanza, mwili wa mama huanza "kujifunza" kuwepo kwa protini ya Rhesus Positive kutoka kwa mtoto aliye ndani ya tumbo lake.
Kwa kawaida, hakuna madhara makubwa...
↳ Lakini baada ya kujifungua, damu ya mtoto inaweza kuchanganyika kidogo na damu ya mama.
Hapo ndipo mwili wa mama huanza kutengeneza antibodies za kupambana na Rhesus Positive...
Mimba ya pili ikija… Mwili wa mama huona mtoto kama ADUI...!
Ndiyo Na maanisha ADUI.!
↳ Antibodies zile sasa huanza kushambulia damu ya mtoto wa pili, wakidhani ni "mchokozi" Hii inaweza kusababisha...
☠ Kupoteza mimba.
☠ Mtoto kuzaliwa akiwa na upungufu mkubwa wa damu.
☠ Ulemavu wa ubongo kwa mtoto.
☠ Kifo cha mtoto kabla au Dakika 15 mara tu baada ya kuzaliwa.
Uzuri ni kwamba Suluhisho Lipo — Lakini wengi hawajui..!
↳ Mara baada ya kujifungua mtoto wa kwanza, mama mwenye Rh (–) anapaswa kupewa sindano maalum ya Anti-D Immunoglobulin ndani ya masaa 72.
↳ Pia inapaswa kupewa wakati wa ujauzito ikiwa kuna damu ya mtoto inaweza kuchanganyika na ya mama mfano, bleeding, kuumia tumboni, nk).
↳ Sindano hii huondoa kabisa hatari ya mwili wa mama kutengeneza antibodies zitakazoshambulia mimba zinazofuata..!
Elimu hii imeokoa Maisha ya Mamilioni ya Watoto Duniani..!
↳ Lakini hapa kwetu Bongo, Ndoa nyingi zinaingia kwenye mateso bila kujua sababu. Wanawake wanahangaika bila kujua mwili wao wenyewe ndio unawaumiza watoto wao – kimyakimya..!
↳ Wanaume tupo, kama matwantwa, Hatushirikiani na wakezetu, Kuanzia kabla ya mimba, baanda ya mimba, hatuendi kabda clinic...!
Wanandoa wote, tafadhali: Fanyeni vipimo vya damu kabla ya ndoa..!
✔ Tambueni kundi la damu na Rhesus factor zenu,
✔ Panga uzazi kwa maarifa,
✔ Linda maisha ya watoto wenu — si kwa bahati, bali kwa ELIMU!