Mimea yangu ya siku 45 inanyauka, nifanye nini kuinusuru?

unalima wapi?? hii hutokea kama umwagilianji unakuwa sio sahihi au kama utamwagilia hioni saana kuelekea giza! pia inategemea mbolea uliyotumia katika kukuzia,
Iringa ruaha mbuyuni natumia nitrabor mkuu
 
Mimea ya mazao gani? Unalimia wapi?

Miti, maua, mboga, nafaka?? Funguka..
Angalia maji kama ni chumvi pole, utajua hilo kama udongo unatengeneza kitu cheupe juu.

Everyday is Saturday...........................😎
Hii nimeiona mkuu
 
Pole sana mkuu, wakulima huwa hatulimi kilimo cha kiangazi wenye udongo aina hiyo, hiyo magadi au chumvi, na treatment yake ni mbolea za asili, samadi kwa wiingi na maji yasiyo na chumvi kwa wingi. Udongo usikauke!

Mimea itaota lakini inafikia mahali inakufa au haizai! Hapo tegemea mvua ije iokoe jahazi.

Siyo kila udongo unafaa kilimo cha kiangazi

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Tikiti halilimwi kwenye udongo mfinyanzi, huo udongo unanata, tikiti linataka tifutifu ya kichanga.

Pole, nikushauri uachane na kuendelea kutumia gharama, wenyeji ni wahuni watakupa swagga mwaka juzi mtu alivuna tikiti milioni 6, ili wao waendelee kula hela yako zinduka. Unawahudumia wao kijanja wewe hupati kitu!

Hilo shamba wamekuingiza chaka!

Everyday is Saturday.............................. 😎
 
Duuh nakubali mkuu nimepata somo.
 
Hii nimeambiwa sana mkuu
 
Aphids hao

Tafuta dawa inaitwa Actara

Kuna wadudu chini ya jani japo umepiga picha juu ya jani
 
Aphids hao

Tafuta dawa inaitwa Actara

Kuna wadudu chini ya jani japo umepiga picha juu ya jani
Kwa mtazamo binafsi, tikiti kishachelewa 45+days, hata akipiga dawa gani, lifespan inaelekea ukingoni..

Ajifunze hii iwe somo au aanze upya.

Everyday is Saturday............................. 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…