NN, hutaki hausi gelo sababu ya lifestyle ya huko
chakula cha supamarket almost kimetayarishwa vizuri wewe ni kwenda kumalizia tu
hapa siku nakula kuku nina kazi ya kumkimbiza, nimchinje, nimnyonyoe na kumpika
huko mna maharage ya kopo, mie nina masaa 3 ya kusubiri maharage yaive kwenye mkaa
huko mna dishwasher hapa nika kazi ya kusugua sufuria kwa mchanga wa bahari
mna washing mashine, nina kazi ya kufua, na kuanika nisubiri zikauke
maji na umeme 24/7 hapa maji yakitoka hatulali tunajaza hadi vijiko.
Siku nyingine zote ni ya kuchota kisimani au bomba la kijiji
umeme ungekuwepo ningechemsha maharage ya wiki nzima lakini siwezi andaa vitu na kutegemea kutunza kwenye friji sababu umeme sio wa uhakika
hata hivyo familia ngapi zinauwezo wa kumiliki friji?
Huko unasafisha nyumba labda mara moja kwa wiki, hakuna vumbi lakini huku kudeki ndani kila siku is a must, kufuta madirisha na vitu vyote ndani vinginevyo utakuwa kama unakaa chini kwa vumbi
haya una watoto wadogo, huko mnapeleka day care centre, kwanza day care ni chache, ni gharama kubwa mtanzania wa kawaida hawezi kuaford hata kama inawezekana kuaford bado hazina usalama kwa watoto wadogo sana
bado uende kazini na trafiki jam kama uko dar, sure you need someont to help you somewhere
lifestyle ni tofauti na mazingira ni tofauti.
Mimi kama mimi sifagilii kabisa haya mambo ya kuwa na 'housegirl' na huwa sieleweki na wengi humu kwa nini nina msimamo huo.
Kwanza sipendi kutumikisha wengine. Maadili yangu yananikataza kabisa. Naonaga hao wasaidizi wa ndani kama huwa hawatendewi kwa haki.
Pili, yote anayofanya huyo 'housegirl' nami naweza kufanya. Napika, nasafisha, nafua nguo, napiga pasi....you name it, I do it.
So why hire someone to do my house chores when I can do them myself they way I want to? I see no need to!
Tatu, unaweza kuta mtu hana hata familia, labda yupo yeye na mumewe tu lakini eti ana 'housegirl' nyumbani. Really? What for? I guess maybe having one is a status symbol or something.