Mimi bado mwanachama wa Simba SC – Mzee Kilomoni

Joined
Jun 14, 2017
Posts
74
Reaction score
44
Mbali na taarifa za kuondolewa kwenye bodi ya wadhamini wa klabu ya Simba na kusimamishwa uanachama wa klabu hiyo huku akipewa sharti la kufuta kesi aliyofungua mahakamani, Mzee Hamis Kilomoni hana habari na masharti hayo na ameendelea kukomaa kuwa hatafuta kesi hiyo mahakani kwani hajapata barua ya kufukuzwa uanachama.



Kupitia Mkutano mkuu wa Simba uliofanyika wiki mbili zilizopita klabu hiyo iliamua kumuondoa Hamisi Kilomoni katika bodi ya wadhamini na nafasi yake kuchukuliwa na Adam Mgoyi huku kaimu rais wa klabu hiyo, Salim Abdallah akieleza Kilomoni kusimamishwa uanachama hadi atakapofuta kesi mahakamani huku akiutanabaisha umma kuwa asipofanya hivyo watamfuta uanachama moja kwa moja.

Nangoje barua ya uamuzi huo, ninachojua mimi bado niko Simba kwa kuwa sijapewa barua rasmi hadi sasa, Siwezi kulizungumzia kwa kina sababu sina barua, nitakapoletewa barua rasmi ndipo nitakuwa katika nafasi ya kulizungumzia,“amesema Mzee Kilomoni kwenye mahojiano yake na gazeti la Mwanaspoti.

Kuhusu taarifa za yeye kufuta kesi mahakamani, Kilomoni alisema hajafuta na hawezi kufanya hivyo hivi sasa ingawa hakutaka kuzungumzia kama atakuwa tayari kufuta kesi endapo ataletewa barua hiyo.

Narudia tena nikishapewa barua rasmi nitakuwa kwenye nafasi ya kuzungumza kila kitu, najua klabu yetu ina matatizo mengi, lakini yote tuyaache kwanza nisubiri barua yangu ya kusimamishwa kwanza,“amesema Kilomoni.

Hata hivyo, klabu ya Simba leo Jumapili itakuwa na mkutano wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu hiyo mkutano utakaofanyika jijini Dar es Salaam, huenda ikalijadili kwa mara nyingine sakata la Kilomoni.
 
Hali tete ndani ya mikia fc iko wazi kabisa.

Sitashangaa kusikia kundi moja linajiita Simba Original na kundi jingine Simba MO.
 
Mzee Chilomoni huyu,
Kabila lake atakua ni
Mmaviya.
Hizi ni tabia za Wamabia.
 
Huyu mzee kwanini Mungu asimchukuee tuuu! Hawa wazee wanaboa sana!

Pogba wa tz nchi imekushinda!
 
Ni njaa inamsumbua huyo mzee, anatumiwa na wapinzani ili kuihujumu
Simba sc.
Kama alikuwa na shida muhimu kwa nini asiiweke kama ajenda ili ijadiliwe na wanachama wa Simba ?

Huyu mzee haaminiki tena hapo Klabuni.

Ni bora kumfukuza uanachama kabisa. Kajidhalilisha sana.

MO hawezi kumpa hela mamluki huyo.
Aende akafuge ndoa na Bi Hindu wake.

Simba sio mali ya mtu mmoja, hata MO anaweka hisa zake tu ili kuiendesha timu. Anaweza kuuza hisa zake kwa wanachama hapo baadae au akamwuzia mtu au kampuni nyingine yoyote.

Elimu pia inampiga chenga huyo Babu na Bibi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…