Mimi Kama Shabiki wa Dar Yanga SC nawatakia ushindi Azam FC dhidi ya Yanga SC

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Kuna neno fulani la kizungu linaitwa "Enlightment Period" Ila sitawezeza kulifanyia tafsiri sisi kabisa kwenye mjadara huu. Ila kwa kifupi ni kipindi ambacho yaliyo mema na mazuri ambayo yanasifiwa na kufurahisha na kuonekana yalipata kufanyika kwenye nyakati hizo.

Wanajanangwani kwa sasa wamemaliza kipindi chao hiko, ambapo itawapasa wachukue tena miaka 3 ijayo kujitengenezea enlightment period nyingine kwenye tasnia ya soka.

Kusua sua kwake msimu huu kunadhihirishsa wazi kuwa nyakati zao sasa zimekwisha, na kipindi cha mwingine. Hivyo basi bila kusema mengi ningependa kuwatakia Azam FC ushindi mnono hapo Jumamosi watapokutana na Yanga SC. KUna uwezekano ikawa isiwe dhahiri kuwa ni enlightment period ya azam fc lakini siku zote waswahili wanasema "nyota njema huonekana asubuhi", na hatma haiumbwi na kisicho dhaniwa.

Licha ya ukimya wao naona kabisa Azam FC wanafaa kuwa mabingwa wa ligi kuu msimu 2017/18, hivyo basi hata kulingana na shaka yangu izaliwayo na muenendo wa Yanga SC napenda kuweka wazi kuwa nawatakia ushindi mnono walamba koni ifikapo jumamosi.

Kabla sinatamatisha andiko,

Niseme kuwa kila klabu kubwa ulimwenguni yenye kupitia kwenye "enlightment period" ni lazima ipumzike kwa muda mfupi ili kupisha mabadiliko ya nyakati kabla haijarudi kwenye kipindi chake.

Kwa mfano :-
Timu yenye mafanikio makubwa nchini Uhispania "Real Madrid" iko kwenye kipindi hiko hiko cha mpito.

Timu yenye mafanikio makubwa uingereza "Manchester Unite" iko kwenye kipindi hiko hiko cha mpito.

vile vile
Timu yenye mafanikio makubwa Tanzania "Yanga SC" iko kwenye kipindi hiko hiko cha mpito.

ANGALIZO:-
Kipindi hiko cha mpito huwa hakidimu kwa zaidi ya miaka 3, ukiona timu iko kwenye kipindi cha mpito kwa zaidi ya miaka 3, Tambua kuwa haikuwahi kuwa kwenye "Enlightment Period". Kigezo pekee cha timu kuwa kwenye Enlightment period kuanzia miaka 10 na kuendelea.

Nawasilisha,

Demigod-
 
Angalau mmeanza kuwa wakweli, baada ya kujiumauma kwa muda mrefu.
Yanga haikustahili hata kuwa bingwa msimu uliopita, ilikuwa dhaifu kulinganisha na misimu 2 iliyopita. Huu ni ukweli uliowazi
 
Simba wamepambana na Yanga nje ya uwanja kupitia Bashite...
 
Yanga hawana lolote bila Manji.

Yanga hawana lolote bila tajiri wa kulipia mishahara.

Yanga si kitu wasipobebwa uwanjani.

Azam 4-0 Yanga

--by mshabiki wa mbao fc
 
mbaya zaidi unacho omba hakiwezekani, Yanga bado atakuwa bingwa mwaka huu.
 
Yanga hawana lolote bila Manji.

Yanga hawana lolote bila tajiri wa kulipia mishahara.

Yanga si kitu wasipobebwa uwanjani.

Azam 4-0 Yanga

--by mshabiki wa mbao fc

Yanga imezaliwa na kuanza kubeba mataji kabla mimba ya manji haijatungwa kwenye tumbo la mama yake..

Yanga imeanza kubebwa tangu mwaka 1935 mpaka mwaka 2018

Unalingine?
 
mbaya zaidi unacho omba hakiwezekani, Yanga bado atakuwa bingwa mwaka huu.


Dalili za Ubingwa naziona kwa Azam FC kwa msimu huu tu. Ila nakuruhusu kuendelea kuwa na Matumaini kama waliyokuwa nayo wale waliokuwa wanangojea barua kutoka FIFA.
 
demigod wewe acha bana, sisi tumo bado.


Mkuu ni vyema kuongea lile ambalo moyo unaamini. Ila sijapinga kuwa hatumo kwenye mbio za ubingwa. Nafsi yangu inaniambia tuwarahisishie AZAM FC njia kwa msimu huu...Tukimkazia Azam FC wale jamaa wa Bilioni 1.3 watafurahia sana
 
Yanga ilishawahi kumpa sare Azam ili Matopeni wakose nafasi ya pili.

Ni kweli tunapitia kipindi kigumu au tukiite cha mpito. Mabingwa wote wa kihistoria katika kila nchi hupitia kipindi kama hicho.

Tayari Simba wameishakosa Kombe la FA. Nafasi pekee ni ubingwa wa VPL ili washiriki mashindano ya CAF.

Azam anayo nafasi ya kuwa bingwa VPL. Kama ushindi wa Azam dhidi ya Yanga unawapa hiyo nafasi, bora iwe hivyo. I can not imagine kelele za Matopeni wakichukua ubingwa baada ya ukame mrefu.

Honestly, baada ya mechi za Mbao na Mwadui, sioni vipi Yanga tutatoboa msimu huu. Miracles do happen though.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…