Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
KUTOKA DHUHR HADI ALASIRI NA MASUDI ''MTU SPECIAL'' KIPANYA
Leo ilikuwa siku makhsusi yaani special sana kwangu kwa kuwa katika chumba kimoja na Masudi Kipanya na vijana wake ''sharp'' wa Clouds Plus.
Hiki kwa hakika si chumba kwa maana ya chumba kama tulivyozoea bali ni Maktaba ya Elite Bookstore Mbezi Samaki.
Masudi Kipanya alinikaribisha ndani ya Maktaba hii nadhifu sana si kwa kuangalia na kusoma vitabu bali kwa ajili ya kufanya kipindi cha televisheni.
Mvua kubwa iliyonyesha kipindi cha adhuhuri kwa kiasi cha saa moja hivi ilitosha kunionya kuwa ile ilikuwa tahadhari kwangu kwa mfano wa ''thunder and lightning,'' (radi na kimulimuli) katika mchezo wa Mcbeth kuwa mchana wangu hautakuwa wa kawaida.
Kwa muda wa saa mbili Masudi Kipanya akitembea katika mengi niliyopata kuandika katika historia ya Tanganyika alinirudisha nyuma miaka 100 hapa hapa Dar es Salaam ya 1920s akitaka kujua maisha ya wazee wangu waliosukuma gurudumu la historia ambayo si wengi wanaifahamu.
Masudi Kipanya kama ni mchezo wa masumbwi nitamwita, ''South Paw,'' kwa jinsi alivyonitaabisha na maswali ya kushtukiza na wakati mwingine kunibana nisema nisiyopenda kusema na wakati mwingine kunitoa kwa haraka katika niliyodhani yangefaa kusemwa.
Muda ulikwenda kwa haraka sana jua likazama nikiwa sina habari na hatujamaliza safari yetu ya miaka 100.