Mimi na Afrika yangu: Usiku mkali,hatujali tulikotoka,hatujui tulipo,tunaelekea kokote

Mimi na Afrika yangu: Usiku mkali,hatujali tulikotoka,hatujui tulipo,tunaelekea kokote

GuDume

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2015
Posts
6,651
Reaction score
14,337
Safari imeanza masaa matatu yaliyopita ilikuwa ni mida ya saa mbili na robo usiku yaani 20:15 abiria wengi walianza kwa matumaini sana lakini imegauka kuwa ni safari ngumu yenye mashaka matupu.abiria tumepanda basi hili lakin nasi hatujui tuendako.nakumbuka dereva alipongia haraka alikamata usukan na kuingiza gia.gari likaanza kurudi nyuma...aliendelea kukanyaga mafuta zaidi mpaka abiria walipopiga kelele kuwa gari linarudi nyuma sana atagonga wenzie waliokuwa wamesimama kwa mbali wamemwachia na yeye aendeshe. wale madereva wenzie waliokuwa chini wanampungia mkono huku wakitabasamu.

Basi dereva hapo akasimamisha gari kisha akapuliza moshi mwingi hewani... abiria wengine wakaanza kukohoa kisha akatamka "haya sasa twendeni" abiria tukatizamana maana hatukuelewa anasema twende wapi...kiukweli hata mimi sikujua ninapoenda.nlidandia tu hili basi niende huko mbele.abiria mmoja akasema "baba twende tu" basi likaanza kuserereka kuelekea huko mbele. Wakat mwingine dereva akawa analiacha liserereke ye anakuja nyuma kudai nauli.abiria wanatoa shilling shiling nying na kummiminia dereva kwenye kikapu chake.anafoka "ongeza pesa "huku mate yakiruka.... Abiria mmoja mzee anasema " hiyo tu ndo ninayo baba..." dereva anamtizama kwa jicho kali toka juu mpaka chini.

Anagundua abiria kavaa msuli wa thaman anamwambia kwa ukali"toa hii nipe ama sivyo ntakushusha" abiria mmoja ananyanyuka toka nyuma na kumkemea yule mzee...
"we babu toa huo msuli unadhan kuendesha gari ni rahisi?toeni nauli"
naye anatoa zake zoote na kuiacha mifuko nje kuonesha hajabakiza kitu. Dereva anamwangalia halaf anakenua meno yake....nadhan yeye anamaanisha kutabasamu.anamwambia yule abiria "wewe sasa uwe konda."
basi anapewa nafasi ya kuwa konda kukusanya nauli mle ndani. Anakusanya kwa weledi sana akiwafokea na kuwapiga mateke abiria wanaochelewa kutoa nauli au wanaotoa kidogo .anaonekana akifurahia kazi na mara nyingine anamwambia dereva
"kula vichwa hivyo..."
dereva popote alipo anasimama.abiria tumeshikilia roho zetu mwendo anaoendesha dereva wetu ni wa hatari hata alama za barabaran hajali "ama kweli gari limepata dereva" naangalia pale juu mbele gari limeandikwa "kichaa karogwa tena". sijui maana ya maneno haya. mara dereva anasikika akisema
" mi napenda makonda kama wewe, haya sasa tuende wapi...? konda anamwambia
"kula kushoto baba kanyaga twende iende irudi" natizama nje tunapishana na basi lingine limeandikwa nyuma "kichaa kapewa panga, pasua roho zao"

abiria wengine wanashangilia sana.nawauliza
"wenzangu mmeshakumbuka mnaenda wapi?" Wanasema
"aaahh mwache dereva atiririke tu tunapenda mwendo kama huu tutawahi kufika" nawauliza "mtawahi kufika wapi?" wanajibu "huko huko tu tunakolekea"abiria wachache wanashtushwa na ule mwendo na uendeshaji wa dereva wanaposema dereva huu mwendo ni hatari...konda anamwambia
"simamisha tushushe kuna wanga wanatuletea giza huku"‎ dereva anasimisha gari na konda anarudi nyuma na kumkamata kija mmoja mpuuzi na mlalamishi anayetaka gari liendeshwe kwa kufuata sheria za uendeshaji.wanamburuta naye akipambana kutaka kubaki gari maana akitizama nje kuna kiza na ni porini. wanafanikiwa kumshusha wakimsukumia mateke na ngumi... dereva anaingiza gia anakanyaga tunaenda. mwendo ni wa kasi sana. na gari hili kuu kuu halina taa... na hata kusimama kwake ni kwa shida maana ni mpaka liwekwe kigingi ndo lisimame kabisa.

naanza kuwaza... nawaza sana tunaelekea wapi? je tutafika? na tukifika tutakuwa salama? abiria tuna mgagaiko wa mawazo kuna wanaosema huu ndo mwendo sahihi tumechelewa sana maana yule dereva aliyeshuka kule mwanzo yeye alikuwa na yake. ni kweli yeye aliendesha kwa mwendo wa kinyonga wakati mwingine alikuwa anasimamisha gari anashuka anaenda kuwasilia akina bi mdogo wote waliokuwa pembezon mwa bara bara ile.

ilikuwa si ajabu akasimamisha gari na kusema tumpe nauli ili akanunue zawadi za kwenda kumpa hawala yake kijiji kijacho. naye alikuwa na yake.ila kashuka ... kashuka kampa dereva huyu atuwaishe. tuwahi safari hii iliyochelewa sana.kila mtu anaonekana kujawa na mawazo, lakini si haba kuna wanaoshangilia tena ni wengi.. wakisema
" pasua baba pasua anga.... haina kulala hii " ni usiku wa kiza kinene... hata ndani hakuna taa.. watu wanapapasana kutafuta pa kushika. mara inasikika sauti
" heeeh we kaka vipi ndo unanishika wapi huko" ni dhahiri hii ni sauti ya kike ingawa kuna kelele lakini nasikia ni sauti ya kike..inajibu nyingine ya kiume
" acha hizo wewe ungetaka usishikwe ungapanda taxi, yaani kwa akili yako tulivyojaa hivi unataka bado usiguswe we nani?kama vipi shuka tuache sisi twende" abiria wengine wanacheka. hali ya hewa kwenye gari nzito sana... kila harufu inasikika huku wengine wakilalamika
" unanikanyaga bwana we vipi hutulii kama kuku anayetaka kutaga!" aliyekanyaga anajibu kwa jeuri.
"unajua kukanyagwa wewe? ukikanyagwa utasema"

hapo nainamisha kichwa chini na kuanza kusali... maana nawaza ikitokea tumepata ajili nimefariki basi angalau kwenye list ya kwenda mbinguni nisikosekane. siti niliyokaa inanipa shida kwa hili gari si ajabu ukakaa siti ya pili kutoka mbele lakini badaye ukajikuta umehama mpaka nyuma..ni gari kuu kuu sana. ukikaa kwenye siti inabidi ujishikilie wewe na siti wote msihame hivyo inasadia usilale...maana ukilala unaweza jikuta upo chini au nje kabisa ya gari. barabara ni mbaya na wakati mwingine tunafika sehemu kumewandika "dead end" basi tunarudi tena kutafuta barabara halafu tuendelee kwenda huko tunakotiririka na hili gari....
 
Haha tutafika tu hata kama in vipande vipande
 
Mkuu ,Saluti kwako kwa Tafsida uliyoitumia ili kufikisha Ujumbe.Kuna Watu watatoka patupu hapa wakidhani ni Hadithi ya 'Paukwa na Pakawa'..

Homgera sana ,ila hii Safari Mhhhh !!..
 
Dereva aliyepita huko aliko nahisi anakenua meno tu , kuwa sasa anaonekana alikuwa dereva mzuri na anayesikiliza abiria wake.
 
Mahali tutakapogikia ni salama,maandalizi yamekamilika
 
Dereva anatuhakikishia abiria wake kuwa "we are in the right truck" in his original voice.
 
Kweli hili gari ni kuomba tu Mungu maana kwa sifa za Huyo dereva tunaweza ishia njiani wote.
 
Maisha yangu yanabadirika kuwa better nashukuru Mungu. Na siasa nmeanza kuandika miaka mingi sana.labda tu kama ulikuwa hujanisoma rudi nyuma threads zangu za tangu na tangu... Sehemu nyingi nazungumzia siasa kwa namna nyingine.ila kwenye hii thread nmeazungumzia hadith tu ambayo nmekaa nikaifikiria.

Bro siku hizi unatiririsha sana nyuzi za siasa, vp Maisha yashaanza kubadilika nini?
 
Back
Top Bottom