mzeelazaro
New Member
- Aug 25, 2022
- 2
- 2
Afya ya Akili.
Kwa mujibu wa shirika la afya duniani (WHO), afya ya akili ni hali ya kutambua na kuthamini afya ya hisia na mwili kwa ujumla ambavyo vinahusisha ubongo. Afya ya akili katika karne ya 21 imekuwa ni tatizo kubwa kwa jamii zetu hasa kwa upande wa vijana ambao ndio inaaminika kuwa ndio taifa la Kesho. Matukio mengi ya kutisha huripotiwa kila iitwapo leo na kusadikika kuwa tukio limesababishwa na mhanga uyo kuwa na tatizo la afya ya akili. Kulingana na takwimu kutoka shirika la afya duniani inaonesha katika watu 10 basi watu wawili wanatatizo la afya a akili. Hii ni idadi kubwa sana katika jamii yetu.
Tukizungumzia katika nchi yetu pendwa Tanzania vijana wengi wanahusishwa na tatizo hili na wengi wao kuingia katika misingi isiyo kuwa na maadali na baadae kuanza kuwalaumu wazazi kwa misingi ya malezi yasiofaa kwa vijana hao. Katika harakati za kutatua suala la afya ya akili kwa vijana hujiuliza maswali mengi wenda yakawa na majibu sahihi katika mtazamo wa hisia na akili pia
Je, vijana wengi wameyaharakishia maisha kabla ya muda wao?
Je, vijana wengi wanateswa sana na mapenzi?
Je, vijana wengi wamekosa ajira?
Je, vijana wengi elimu yao haiwasaidii chochote katika maisha?
Je, vijana wengi wako sehemu wasiohitajika kwa muda huo?
Je, vijana wengi wameshindwa kuiendesha teknolojia na badala yake inawaendesha yenyewe hasa katika mitandao ya jamii?
Katika mitazamo yote hiyo ya kujiuliza jamii bado inalibeza sana jambo ilo na kuliona ni jambo la kawaida sana ila kupitia sehemu au mihimili mitatu ya afya ya akili kuna jambo la kujifunza na kuweka sawa sehemu palipo na udhaifu uliopitiliza.
1. HISIA. kila binadamu ulimwenguni ameumbiwa hisia na katika vitabu vya dini inaeleza ni jinsi gani hisia ni muhimu katika kutatua mambo muhimu katika maisha yetu ya kila siku. Hisia za watu wengi katika jamii zetu zinakumbana na changamoto nyingi sana na kwa watu waliodhaifu sana ubongo wao hushindwa kutatua changamoto hizo na kufanya maamuzi yasio sahihi na ubongo wao kuona ndio uamuzi sahihi katika maisha. Katika mahusiano mengi ya vijana huonekana ndio chanzo kikubwa cha tatizo la afya ya akili kwa sababu vijana wengi uingia katika mahusiano na mtu ambae hawajaridhiana kwa sababu tu mtu huyo ana kitu ambacho unakipenda katika mwili wake. Hii inatokea sana kwa wanawake hasa anapoingia katika mahusiano na mwanaume kwa kuwa tu mwanaume huyo ni mrefu ana ndevu na pia anamwili unaovutia pasipo kuangalia ni namna gani wanavyoweza kuhitajiana Zaidi au kupeana muda wa kuchunguzana tabia zaidi hivyo mwisho wa siku wanahumizana ki hisia na kusababisha afya ya akili kujeruhiwa. Waathirika zaidi wa hili ni wale wanaoingia pasipo misingi mizuri ya mahusiano.
Pia kwa mtazamo wangu ingependeza misingi ya mahusiano ingefundishwa na kuingizwa katika mitaala ya shule zetu na kufundishwa mashuleni ili kumnusuru kijana na tatizo la afya ya akili. Watu wengi hufikilia mahusiano ni baina ya wapenzi ila katika afya ya akili tunazungumzia mahusiano yote ata pia mahusiano ya baba na mtoto. Kwa kitendo cha mtoto kumuogopa Baba yake mzazi pia uathiri afya ya akili ambapo familia nyingi baba anapofika tu nyumbani kutoka kazini basi Watoto husambaa kutoka sebuleni na kwenda katika vyumba vyao na kumuacha baba sebuleni hii huzoofisha mawasiliano mazuri baina ya wazazi na Watoto na kujenga nidhamu ya uoga.
2. AKILI. kila binadamu anafanya maamuzi anayoona ni sahihi kulingana na akili iliyotafakari na kufanya uamuzi huo. Je, akili zetu hufanya maamuzi sahihi kila tunapoipa nafasi ya kufikiria mitazamo yetu? Na jibu ni hapana hasa kwa vijana wengi maana hisia hupewa kipaumbele Zaidi kuliko akili hivyo husababisha mfulugano wa maamuzi na mwisho kuwa ni Zaidi ya moja ila maamuzi yaliyo na nguvu Zaidi ni yale yaliyobebwa na hisia. Inashauriwa Zaidi kwa mtu yeyote akili inatakiwa kuwa ni Zaidi ya hisia katika maisha. Thamani ya akili hupimwa katika kutatua changamoto za maisha hivyo mtu akishindwa kutatua changamoto zake za maisha husababisha akili, hisia na mwili wake kujihisi ni dhaifu sana na kutokujali kuwa ana muda mwingine Zaidi wa kujitafakari kabla ya kuchukua maamuzi yasiofaa katika maisha.
Mwili wa binadamu unatakiwa utawaliwe na akili na sio hisia ili kujenga mwili wenye afya na wakuweza kufanya uzalishaji uliokamili. Katika mahusiano pia fanya akili yako iongozee kila kitu hasa kwa vijana wanaoingia katika mahusiano ya kimapenzi wengi wao hufikilia Zaidi juu ya upendo baina ya wawili hao hasa mmoja akiwa anampenda mwingine kuliko mwenzake hii hujenga mgogoro wa nafsi na kuhisi unaonewa na mara nyingi watu hawa huwa na utofauti mara kwa mara na pasipo kutumia akili Zaidi ya kusoma tabia za mpenzi wako wengi huangukia katika matatizo ya afya ya akili.
HASARA
Jamii inapokea hasara kubwa sana katika hali hii ya afya ya akili inavyokumba vijana wengi baadhi ya hasara hizo ni watu kuchukua maamuzi ya kujinyonga kwa sababu ya migogoro ya kifamilia, kujiingiza kwa vijana katika matumizi ya madawa ya kulevya na ukabaji kwa kisingizio cha usefu wa ajira wa vijana waaomaliza elimu, kupunguza nguvu kazi ya taifa maana kijana aliejeruhiwa na afya ya akili hukosa umakini katika kufanya kazi kwa ukamilifu unahitajika na mwisho ni kusambaza udhaifu wa wenzi wao baada ya kuachana na kupelekea kufedhehesha familia na jamii kwa ujumla.
USHAURI
Jitahidi kumshirikisha ndugu, jamaa na marafiki unaohisi unawaamini sana katika mambo yako ili waweze kutoa maoni yao pale unapohisi maoni yako katika misingi ya matamanio yako hayajitoshelezi. Pia jenga tamaduni ya kujiweka bize na harakati tofautitofauti na kujiepusha na muda mwingi kutaka kukaa peke yako ambako kunakufanya kuwaza sana vitu vingi vinavyopelekea kujeruhi afya yako.
Pamoja na hayo yote vijana wanapaswa kupunguza matarajio makubwa kuliko uhalisia. Pengine vijana wengi mtaani huwa na matarijio makubwa sana na yanaumiza sana hisia zao pale wanapoona hayatimii kwa muda waliopanga wao na kupelekea kuchukua hatua za kujinyonga na kufanya matukio mengine mengi yasiofaa katika jamii zetu.
Mwisho, pengine unaona kuna jambo linakugusa na unaona linaweza kupoteza furaha na amani ya moyo wako tafadhari fika hospitali na onana na mwanasaikolojia na upate ushauri mzuri utakao kujenga Zaidi katika maisha yako. Epuku msukumo rika katika kufanya maamuzi.
Mimi nimepona afya ya akili. Wewe je?
Naomba kuwasilisha. Asante.

Upvote
0