Mimi na BVM bhaasiii..!! Nahitaji ushauri wako wa kujenga na si kubomoa

Moyibi

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2012
Posts
1,054
Reaction score
701
Wasaalam...ndugu zangu wa Jf...kama mlivyoona kichwa cha habari hapo juu..nimeamua kupiGa hii kozi chini..coz naona sikupangiwa kumaliza hii kozi..anatoMy imenikimbiza kabisa...!! Na ingekuwa pouwa sana kama mngenisaidia majibu ya haYa maswali Yangu...

1. Utaratibu wa ku-post kozi kwa hapa sua ukoje
2. Mwaka huu na mpango wa kuomba biotechnlgY udzm..je still kuna muda au ndo ivYo tena mpaka mwakani?
3. Na vipi? Kuhusiana na bodi Ya mkopo nitawarudishia kiasi gani cha pesa ni ada tu au ni mpaka meal n accomodation?
4. Je nikiwarudishia pesa Yao..je kuna uwezekano wa kupata tena mkopo kwa mwaka huu..nikiwa nimekidhi viwango vYao..

Ni haYO tu !! Kwa leo ushauri wako unahitajika na c' kejeli... Ni kheri ukaenda kusoma miaka3 Ya biotech kuliko kusoma miaka zaidi ya 5...Ya BVM..!!
 
Kwahiyo wewe mpaka umeanza kusoma hiyo kozi ulikuwa hujua unachokitaka maishani...? Au wewe ni bendera fuata upepo...?
 
*Kwanza rekebisha uandishi wako wa maneno na pia kuweka kirefu cha BVM(Bachelor of Vetenary Medicine) ili uweze kueleweka vema, Kumbuka wewe ni msomi na hapa ni Jamii Forum na wala sio Facebook.

*Ndugu yangu hukuyaona hayo kabla mpaka uyaone sasa? Hakuna Course rahisi chuoni bali inategemea mtu mwenyewe zaidi, ndio maana wakati hiyo Anatomy huipendi, unakusumbua na unafeli kuna mtu hapo hapo chuoni inaipenda, anaimudu na anafauli.

*Suala la kuhairisha mwaka lipo vyuoni na ni rahisi, lakini nakushauri kwanza upate ushauri mahususi kutoka kwa walimu wako!, wanachuo waliokutangulia miaka ya masomo au Mshauri wa wanafunzi(Dean of Student) kwanza.
Lakini ni bora kurudia mwaka(If possible) kuliko kuhairisha masomo.
 
mkuu usikate tamaa kihivyo jitahidi kwa huu muda uliobaki unaweza kuleta mabadiliko
 
Wewe dogo mi nakushauri ubakie hapohapo SUA na BVM yako. Course zingine kwa sasa zinachangamoto kubwa ya ajira! Biotechology ya UDSM haina tofauti sana na BLS ya SUA. Wote waliomaliza bado Serikali haina mpango nao. Private sector ndo mara nyingi zinawajiri but ni ngumu kupata nafasi kwenye private sector. SIKILIZA MY FRIEND, HATA MIMI NIMEUA BLS HAPO SUA, na Ninamarafiki wengi wamemalza Biotech UDSM, wote bado hatujapata sehem maalum ya kujishikiza.
USHAURI WANGU.
*Nivema ukabaki BVM kama unampango wa kuajiriwa kwa urahisi.
*Punguza stress ili ufanye vzr kwenye Anatomy, coz ukitulia kila kitu kitakuwa poa.
*Jaribu kuwa karibu sana na Academic advisor wako, atakusaidia kwa kiasi kikubwa endapo hutamficha kitu.
NIHAYO TUUU!
 
Sijui BVM wanasoma anatomy gani ila hata mimi mwaka wa kwanza wa MD anatomy ilikuwa ngumu kwangu ila kuna prof akatufundisha siri ya kusoma anatomy :

Kwanza anatomy ni kumeza mwanzo mwisho...na akili ya kumeza inapatikana unapoamka asubuhi....yani kila unapoamka chukua anatomy soma kwa nusu saa then endelea na ratiba nyingine (of course baada ya kuoga na vitu vingine)...kesho yake ukimka soma tena nusu saa ukianzia pale ulipoishia.....watu wanakosea kusoma kichwa kikiwa kimechoka

Ukiachana na hiyo ratiba ya asubuhi...unatakiwa uwe na ratiba nyingine ya kupitia angalau siku mbili katika wiki.....yani katika hizo siku mbili unasoma angalau nusu ya siku au zaidi ila hakikisha umepumzika vizuri kabla ya kuanza kusoma

Mimi nilikuwa nasoma hivi....nikisoma mara ya kwanza mara ya pili nasoma kwa mbinu ya kufunga daftari....yani naangalia heading halafu najaribu kukumbuka kila kitu kuhusu heading hiyo pasipo kuangalia kwenye kitabu...mfano muscles of the leg...basi nafunga kitabu halafu najaribu kukumbuka muscles zote halafu ndio naangalia wapi nimesahau au kukosea..

Ukizoea utashangaa nini kilikua kinakushinda......Pia nina uhakika kuna wanafunzi wengine wanaliweza hilo somo kwa hiyo jaribu kuchunguza mbinu zao.....

Kuna kozi sio za kuziachia kirahisi ndugu yangu hasa kama umetoka familia masikini na huna connections....sasa hivi watoto wa masikini ni Medical studies na Education ndio mpango mzima.

Ni hayo machache
 
kozi moja isikufanye ubadlishe chuo kaka cha msingi ni kujituma na kuomba ushauri kwa waliokutangulia jinsi ya kusoma antomy kwa ata mimi nasoma engineering nilikuwa nashndwa kusoma biochemistry baada ya kuonana na watu walionitangulia sasa nasoma kwa uzuri kaka
 
Hakuna utaratibu wa kupangiwa mentor ukiwa hapo chuoni? Kuna prof mmoja anaitwa melau, mtafute. He is very friendly na atakushauri nini cha kufanya na best ways za kufanikiwa. Binafsi sikushauri ukate tamaa. Komaa nayo hiyo shule, hata biotechnology mbona ngumu pia? Komaa tu utamaliza. Nakusikitikia kuhusu huo mkopo unaopata hapo. Kama wao wanaweza wana nini hata wewe ushindwe una nini?
 
Sijui BVM wanasoma anatomy gani ila hata mimi mwaka wa kwanza wa MD anatomy ilikuwa ngumu kwangu ila kuna prof akatufundisha siri ya kusoma anatomy :

Kwanza anatomy ni kumeza mwanzo mwisho...na akili ya kumeza inapatikana unapoamka asubuhi....yani kila unapoamka chukua anatomy soma kwa nusu saa then endelea na ratiba nyingine (of course baada ya kuoga na vitu vingine)...kesho yake ukimka soma tena nusu saa ukianzia pale ulipoishia.....watu wanakosea kusoma kichwa kikiwa kimechoka

Ukiachana na hiyo ratiba ya asubuhi...unatakiwa uwe na ratiba nyingine ya kupitia angalau siku mbili katika wiki.....yani katika hizo siku mbili unasoma angalau nusu ya siku au zaidi ila hakikisha umepumzika vizuri kabla ya kuanza kusoma

Mimi nilikuwa nasoma hivi....nikisoma mara ya kwanza mara ya pili nasoma kwa mbinu ya kufunga daftari....yani naangalia heading halafu najaribu kukumbuka kila kitu kuhusu heading hiyo pasipo kuangalia kwenye kitabu...mfano muscles of the leg...basi nafunga kitabu halafu najaribu kukumbuka muscles zote halafu ndio naangalia wapi nimesahau au kukosea..

Ukizoea utashangaa nini kilikua kinakushinda......Pia nina uhakika kuna wanafunzi wengine wanaliweza hilo somo kwa hiyo jaribu kuchunguza mbinu zao.....

Kuna kozi sio za kuziachia kirahisi ndugu yangu hasa kama umetoka familia masikini na huna connections....sasa hivi watoto wa masikini ni Medical studies na Education ndio mpango mzima.

Ni hayo machache

Fuata huu ushauri utakusaidia sana
 
Wewe dogo mi nakushauri ubakie hapohapo SUA na BVM yako. Course zingine kwa sasa zinachangamoto kubwa ya ajira! Biotechology ya UDSM haina tofauti sana na BLS ya SUA. Wote waliomaliza bado Serikali haina mpango nao. Private sector ndo mara nyingi zinawajiri but ni ngumu kupata nafasi kwenye private sector. SIKILIZA MY FRIEND, HATA MIMI NIMEUA BLS HAPO SUA, na Ninamarafiki wengi wamemalza Biotech UDSM, wote bado hatujapata sehem maalum ya kujishikiza.
USHAURI WANGU.
*Nivema ukabaki BVM kama unampango wa kuajiriwa kwa urahisi.
*Punguza stress ili ufanye vzr kwenye Anatomy, coz ukitulia kila kitu kitakuwa poa.
*Jaribu kuwa karibu sana na Academic advisor wako, atakusaidia kwa kiasi kikubwa endapo hutamficha kitu.
NIHAYO TUUU!

poleni Njoon huku
 
kuandika kwenyewe hujui, anatomy utaiwezea wapi? Wewe ni kilaza, hata kozi rahisi kama za polirical science na zenyewe utazikimbia
 
Na wasiwasi na matokeo yako ya kidato cha sita.Lazima ulinunua mtihani.
 
kuandika kwenyewe hujui, anatomy utaiwezea wapi? Wewe ni kilaza, hata kozi rahisi kama za polirical science na zenyewe utazikimbia

Bujibuji mbona unadhalilisha kozi za watu.Nani kasema Political Science ni rahisi?
 
Back
Top Bottom