GoJeVa
Member
- Sep 15, 2021
- 41
- 60
Habari za muda huu, kifuatacho ni kisa cha kweli kuhusu madawa ya kulevya jinsi yalivyomtesa kijana Sulemani Gwakisa.
===
COCAINE/KOKENI.
Karne hii ya ishirini na moja dunia imekumbwa na wimbi kubwa la watu kutumia madawa ya kulevya. Katika utafiti wangu, nilifanikikiwa kukutana na baadhi ya wahathirika wa dawa hizo za kulevya nchini Tanzania. Katika andiko langu hili nitatoa kisa kimojawapo cha mwathirika wa dawa hizo. Nimatumaini yangu, hadhira itajifunza na kufahamu mengi kuhusu dawa za kulevya. SONGA NAYO;
JINA LA KISA: MIMI KATIKA DUNIA YANGU (SIMULIZI YA KWELI).
MLENGWA/MWATHIRIKA: SULEMANI GWAKISA (SIO JINA HALISI).
MSIMULIAJI/MWANDISHI: NISILE NOEL MWAKIPESILE.
Kwa jina naitwa Sulemani Gwakisa, japo watu wengi hupenda kuniita Sele yaani wakifupisha jina langu Sulemani. Nilizaliwa mwaka 1990, katika mkoa wa Dar es salaam kwa bahati mbaya naweza kusema nilizaliwa nikiwa mlemavu, upande wa mwili wangu wa kulia ulikuwa umepooza. Nilipofika umri wa miaka saba nilitembea kwa shida, kwani nilitembea huku mguu wa kulia nikichapia pia mkono wangu wa kulia ulikuwa umesinyaa hivyo muda mwingi nilikuwa nauweka kwa mtindo wa kuukunja. Nilipokuwa na umri wa miaka kumi na moja, ndipo nilianza kuelewa vyema hali halisi ya nyumbani kwetu, nililelewa na mama peke yake sikufanikiwa kumfahamu baba yangu. Maisha ya nyumbani kwetu yalikuwa na magumu sana, mama yangu alikuwa akijishughulisha na shughuli ndogo ndogo kama vile kuuza maandazi na vitumbua. Kutokana na izo shughuli ndiyo tulipata kodi ya chumba, chakula na mahitaji mengine.Tulikuwa tunaishi katika kata ya Mbagala.
Nakumbuka ilikuwa siku ya jumanne mida ya saa mbili asubuhi, mama alikuwa akifua nguo mbele ya uwanja wa nyumba yetu, alikuwa ametingwa na shughuli ya kufua, mimi nilikuwa nimesimama mlangoni nikimwangalia mama kwa makini huku nikiwaza mengi kichwani mwangu baada ya muda kidogo nikaamua kumsabahi kwani ndio nilikuwa natoka kuamka, alafu nikamuuliza;
“Mama, mbona wenzangu asubuhi huwa wanaenda shule alafu mimi sijawahi kwenda?”, mama akanijibu kwa uchangamfu huku akiendelea kufua;
“Mwanangu mwaka ujao nami nitakupeleka shule wala usijali.”
Mara nyingi nilimuuliza mama swali hilo lakini jibu lake lilikuwa lile lile, baadaye nilikuja kutambua kuwa mama yangu alipenda sana kunipeleka shule lakini alibanwa na hali ya uchumi,
****************************************
Baada ya kufika umri wa miaka kumi na tatu, kutokana na kushindwa kwenda shule nilianza kushinda vijiweni huku nikicheza draft na karata ilipofika jioni nilirudi nyumbani, namshukuru mama kwani alihakikisha licha ya kuwa na maisha magumu nyumbani chakula kinapatikana.Nilivyoendelea kushinda kijiweni nilipata rafiki aliyeitwa Jackson, huyu alikuwa kaka yetu pale kijiweni nilipokuwa nashinda, hivyo tulipenda kumwita kaka Jack. Kaka huyu alitokea kunipenda sana, hivyo tukawa marafiki japo alikuwa amenipita sana umri. Kuna siku kaka Jack aliniambia yeye anafanya biashara maeneo ya Ubungo msewe, hivyo alinishauri na mimi nitoroke nyumbani ili niende Ubungo nikafanye naye biashara. Kutoka na ushawishi wake jioni ya siku hiyo niliondoka na Jack hadi Ubungo msewe ambako ndio ilikuwa makazi yake. Hivyo kutoka siku hiyo nikawa nimetoroka nyumbani na kwenda rasmi kuishi na Jackson.
Basi nilianza maisha mapya hapo nyumbani kwa Jack kila asubuhi tulijiandaa na kutoka hapo nyumbani, tulikuwa tunaelekea sehemu moja ambayo baadaye nilikuja kujua kuwa panaitwa kijiweni, Miami Jack aliniambia pale ndio ofisini kwake. Na kweli pale kijiweni walikuwa wanakuja watu mbali mbali, watu hao walikuwa wakifika pale kijiweni walimfuata Jack wao walitoa pesa na Jack aliwapa vitu ambavyo sikujua ni nini. Kuna siku moja baada ya kutoka kijiweni Miami na kurudi nyumbani tukiwa tumelala kaka Jack aliniita na kuniambia;
“Najua mdogo wangu upo gizani, kwani hujui nafanya biashara gani?” nikamjibu;
“Ni kweli kaka.” Jack akaendelea;
“Vitu ninavyowauzia pale kijiweni vinaitwa unga au madawa ya kulevya.” Tena akaongeza
“Mdogo wangu biashara hii ni nzuri sana kwani inanipatia pesa nyingi. Hivyo wewe utakuwa kijana wangu wa kusambaza mzigo sehemu mbali mbali hapa mjini.”
**********************
Baada ya kupita kama mwezi mmoja, siku moja usiku wa saa nne mimi na kaka Jack tukiwa tupo tunaandaa mzigo wa kwenda kuuza kesho yake kijiweni, Jack akaanza kunielekeza;
“Sele hapa tuna unga au cocaine kutoka Pakistani na afghanistani.”, akaendelea;
“Hii cocaine kutoka Pakistani na afghanistani inajulikana zaidi kama musharaf.” Nilikuwa namsikiliza Jack kwa makini sana, Jack akaendelea;
“Aina hii ya cocaine ni hafifu yenye kuuzwa bei rahisi.” Baada ya kuongea hayo aliinuka na kwenda kufungua droo ya kitandana na kutoa kiboksi cha baking powder alafu akaja nacho pale nilipokaa, akachukua cocaine ile aliyoiita musharaf na kuanza kuchanganya na baking powder huku akisema;
“Sele tunachanganya baking powder na hii cocaine ili kuongeza kiasi cha cocaine, hii inatusaidia kupata faida kubwa sana.”
Baada ya kumaliza lile zoezi Jack aliinuka tena na kwenda kufungua ile droo ya kitandana na kutoa cocaine nyingine ambayo ilikuwa ndani ya mfuko wa nailoni, baada ya kuchukua ile cocaine akarudi nayo pale nilipokaa na kuniambia;
“Huu mzigo ni kutoka Brazil, sisi watu wa unga tunauita pele au mchezaji.” Jack akaendelea;
“Hii cocaine toka Brazil ni gharama na inatumiwa sana na matajiri aina hii ya cocaine hatuchanganyi na baking powder.” akaongeza;
“Hatuchanganyi na baking powder kabisa kwa sababu cocaine hii haitaki uchafu wowote, cocaine hii kuna watu maalumu nawauzia wakihitaji huwa wananipigia simu na mimi nawapelekea.” Usiku huo Jack alinieleza mambo mengine mengi kuhusu biashara hiyo, baada ya kumaliza kuandaa mzigo wa kuuza kesho tukapanda kitandani na kulala.
***********************************************
Maisha yangu yalianza kubadilika, nikawa navaa na kula vizuri, kazi yangu ilikuwa ni kusambaza madawa ya kulevya(Unga) ndani ya Dar es salaam kwa watu mbali mbali wengine walikuwa ni matajiri wakubwa na wengine walikuwa ni wauzaji wadogo wadogo ambao nilikuwa nawapelekea mzigo na pesa alikuwa anakuja kuchukua mwenyewe kaka Jack. Kwa jinsi nilivokuwa na ulemavu wangu ilikuwa ni ngumu kuhisi kwamba nafanya kazi ya kusambaza madawa ndani jiji hili kubwa. Kadri muda ulivokuwa unaenda nilianza kujifunza kutumia madawa kidogo kidogo, japo Jackson alikuwa akinikataza sana ilo swala. Mwanzoni nilianza kwa kulamba na kuvuta kwa pua lakini baadae nikajifunza hadi kujidunga kwa sindano, mwisho wa siku nikawa mtumiaji mzuri wa dawa hizo hadi nikawa naleta hasara kwenye biashara ya kaka Jack. Baada ya kuona hasara inazidi Jackson alinifukuza nyumbani kwake na kwenye biashara, hivyo nikajikuta nimekuwa nalala mtaani tatizo kubwa likawa ni kukosa dawa za kulevya kwani mwili wangu ulikuwa tayari umeshazoea dawa hizo.
Hivyo nikajikuta naingia kwenye makundi ya uwizi ili tuu nipate hela ya kununulia dawa za kulevya. Muda mwingine nilikuwa napanda dala dala zinazoenda sehemu mbali mbali ndani ya Dar es salaam na kuomba msaada kama mgonjwa ninayehitaji wa pesa ili nikatibiwe, japo nilipata bughuza za makondakta lakini sikujali, siku nyingine nilipata pesa kwa hao abiria na pia siku zingine nilikosa. Nipopata pesa matumizi yangu makubwa ilikuwa na kununua madawa ya kulevya kwani seheme walizokuwa wakiuza nilizifahamu nyingi na chakula kwa kiasi kidogo, kutokana na hali hiyo nilijikuta nadhohofu sana kiafya na kwa jinsi nilivokuwa na ulemavu wangu nilitia huruma sana. Licha ya yote hayo wala sikuwaza kurudi nyumbani kwa mama Mbagala, hadi sasa sijui kwa nini nilikosa akili ya kurudi nyumbani.
Nakumbuka ilikuwa ni siku ya juma pili mchana, siku hiyo sikuwa na hela ya kununulia dawa za kulevya, nilianza kuhisi mwili kuchoka na kukosa nguvu ilinibidi nitafute sehemu nilale ilikuwa ni maeneo ya stendi ya mawasiliano, kando kando ya bara bara. Watu walikuwa wanapita kama hawanioni, maumivu niliyokuwa napitia yalikuwa makubwa sana meno yalikuwa yanataka kama kung’oka na mwili ulikuwa unatetemeka sana. Nilihisi haja kubwa inataka kunitoka pale pale nilipo lala, nilikuwa sina jinsi nilitegemea haja ingenitoka lakini cha ajabu nilihisi si haja tena bali ilikuwa kama nyama za ndani za haja kubwa ndio kama zinataka kutoka. Hali niliyokuwa naipitia nilishawahi kuambiwa na kaka Jack kuwa inaitwa Alosto, kutokana na maumivu kuwa makali nikajikuta napoteza fahamu.
**********************************
Nilijikuta nipo ndani ya chumba safi nikiwa juu ya kitanda safi, pembeni yangu kulikuwa na mzee wa makamo alijitambulisha kuwa anaitwa Nestory Kalinga ni mfanyakazi wa asasi mojawapo ya kuzuia na kupambana na madawa. Alisema kapigiwa simu na madakari wa hiyo hospitali kuja kunihoji na kunisaidia, aliongezea kuwa nililetwa hapo na wasamaria wema baada ya kuniokota kando ya bara bara. Baada ya mahojiano marefu na mimi pia nilitoa historia yangu ya maisha. Nilipopata ahueni na kuwa na hali nzuri mzee Nestory alinichukua hadi Mbagala kwa mama yangu na baada ya kupata ruhusu ya mama nilichukuliwa na kwenda kwenye vituo vya kutibu watu walioathirika na dawa za kulevya.
*Hivi sasa kijana Sulemani anafanya kazi kama mtoa hamasa kwenye asasi ya kuzuia na kupambana na dawa za kulevya katika kisiwa Unguja huko Zanzibari.
MAONI KUHUSU JANGA HILI.
Ni vizuri serikali ya Tanzania iboreshe namna za kusaidia waathirika wa madawa ya kulevya kwa njia zifuatazo;
*Kuunda asasi nyingi zaidi za kuwashauri na kuwatoa waathirika wa madawa ya kulevya katika dimbwi hilo. Nchi yetu ina wataalumu wengi wa ustawi wa jamii na afya hivyo tukiwashirikisha katika hili, kuna uwezekano mkubwa kupata matokeo chanya, kwani tatizo hili halichagui rika wala nafasi ya mtu. Pia serikali iongeze vituo vya kutibu watu walioathirika na janga hili.
*Pia, vyombo vya usalama viendelee kufanya juhudi zaidi kukabiliana na janga hili kwa kuwatia nguvuni wafanyabiashara,(wakubwa,wakati na wadogo). Hili pia kuna uwezekano mkubwa wa kufanikiwa kwa sababu vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vina watu wabobezi katika kazi hiyo.
*Jamii pia, tusiwatenge waathirika wa dawa za kulevya bali tuwasaidie kwa kuwashauri na kama kuna uwezekano kuwapeleka kwenye vituo vya tiba vinavyohusika na suala hili. AHSANTE.

Upvote
3