Mimi na kura ya hapana kwenye rasimu ya katiba mpya

Mimi na kura ya hapana kwenye rasimu ya katiba mpya

Joined
Aug 18, 2012
Posts
17
Reaction score
2
Tangu mwaka jana TUME YA KATIBA MPYA ilipoanza kukusanya maoni ya katiba mpya imekuwa ikibagua jinsi ya kukusanya maoni na mpaka hivi sasa kundi la wanafunzi wa vyuo vikuu halijafikiwa katika kukusanya maoni na wanasema kwamba wanajiandaa kuandika rasimu ya katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Maswali niliyojihoji Je kuna watu wana haki ya kusikilizwa kuliko watu wa makundi fulani? Je kuna watu wanahaki ya kuwasemea watu fulani katika katiba mpya? kama maswali haya yakipata majibu kupitia tume ya maoni ya katiba ntapiga kura ya ndio lakii yasipojibiwa najiandaa kushawishi watu wasipige kura ya ndio kwa ubaguzi huu wa TUME YA MKATIBA MPYA.
Japo tume hiyo imetoa njia nyingi za kutoa maoni ikiwepo kuandika, kupitia mtandao je walijua hizo njia ndo zitasababisha wasifikie makundi fulani ya kijamii na hizo hizo njia ndo ziwafanye watu wachache tu wachangie.
Mtu anaweza akasema tume ilipita maeneo ya karibu na vyuo lakini asilimia kubwa ya vyuo vya Tanzania wanafanya vipindi hadi jioni hivyo basi watu wa vyuoni walipaswa kutengewa muda wao maalumu wa kwenda kusikilizwa nini kinatakiwa.
Kama katika kukusanya maoni wanafunzi wa vyuo vikuu tumebaguliwa hainashaka hata michakato ya mbele kubaguliwa kwani umuhimu wa mtu huonekana tangu mwanzo na si mwisho kukamilisha matakwa ya watu fulani wanaopenda iwe hivo.
kWA KUKATAA KUTUMIKA KWA MATAKWA YA WATU FULANI NA KWA SABABU HAWAJAONA UMUHIMU WA MAWAZO YA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU IVO BASI NICHUKUE FURSA HII KUWAMBIA WANAFUNZI WENZANGU WA VYUO VIKUU KWA DHULUMA HII YA HAKI INATUBIDI TUPIGE KURA YA "HAPANA" KUONYESHA KWAMBA KUNYIMWA KWETU HAKI YA KUSIKILIZWA HUKU BADO TUNA NAFASI YA MAAMUZI SI JAMBO LA BUSARA HATA KIDOGO.
 
hamna lolote mtakalosema zaidi ya mikopo yenu itambuliwe kwenye katiba
 
hamna lolote mtakalosema zaidi ya mikopo yenu itambuliwe kwenye katiba

kuwa great thinker kama jina la mtandao. usiwe mvivu wa kufikiri kwa kila ufanyalo. shirikisha fikra zako watu wajue mawazo yako wakusomapo. hivo wanafunzi wa vyuo vikuu wanamchango mkubwa kwenye mchakato wa katiba. JIOJI mwenyewe je walitakiwa kubaguliwa kwa presumption tu. au wangewasikiliza ili wafanye kazi yao ya uchambuzi.
 
Back
Top Bottom