Mimi na marafiki zangu hatuna hamasa na mechi ya tarehe 8 tena!

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Kutokana na maelezo ya wahuni fulani katika soka hasa wakizungumzia mikataba ya wachezaji wa Simba,ninaona dalili zifuatazo katika mechi ya watani wa jadi ya tarehe 8 may.

1. Kama walivyozoea kugombanisha wasanii wa bongo fleva Diamond na Kiba, wameanza kufanikiwa kuleta influence yao kwenye soka.

2. Kutokana na sababu hiyo hapo juu,wanajua ili ushindani uendelee, lazima yanga wapate mahali pa kupumulia.Walitaka ubingwa lakini dalili zinaonesha ubingwa bado ni mgumu kwao.Sasa sehemu pekee ya wao kutokea,ni mechi ya tarehe 8.Kuna nguvu kubwa inawekezwa hapo ili kutuliza mashabiki wa yanga na mambo ya akina GSM yasijadiliwe tena kama ambavyo sasa yanajadiliwa wakilaumiwa kwa kushindwa kuchukua ubingwa.

3. Kutokana ha hayo, mechi ya tarehe 8 itakuwa ni ya kisiasa za soka zaidi kuliko ushindani.Na siasa hizi zina lengo la kuibeba yanga.Kwa hiyo upo uwezekano wa matokeo kuwa upande wa yanga.

Mwisho ninatarajia kuachana na upenzi wa hivi vilabu vikubwa kwa sababu inaonekana matokeo yao yanaamuliwa na wahuni na sio uwezo wa mpira.

Ni bora nione Simba ikicheza na timu ya nje nitajua naangalia soka na si Simba na yanga ni ujinga na kuangalia usanii tu.

Shukrani kwa wachezaji wa nje ndio walionipa matumaini sana. Tuna wachezaji wa ndani lakini tatizo baadhi ni kutojitambua
 
Kitendo cha shaffih dauda kutoa siri nzto ambayo haijakanushwa hadi sasa ni wazi kuwa mechi imeuzwa ,kasema kwamba zimbwe na kapombe walishasaini pre contract utopolo which means walipewa kishika uchumba.

Tutarajie display mbovu kutoka kwa hao vijana hiyo tarehe 8. Na inavyoonekana kuanzia leo fujo zinahamia kwa kapombe sasa maana uongozi wa simba umekuwa dhaifu kweli kutohimili pressure za kijinga za kina dauda na rafiki yake herry mzozo.
 
Mkuu shauri tufanyaje kuondoka na huu uhuni. Binafsi unanikera sana,naona kama mijinga fulani inapewa attention ya kupiga propaganda
hata stimu ya kufatilia draw ya robo fainali keshokutwa ishakata kabisa ujinga mtupu tu unaendelea natarajia kuanzia leo nisikie vurugu za kapombe na manula maana zimbwe keshaonyesha njia ya kukodi wahuni wampigie debe mkataba ni mwendo wa matusi tu ya kina shaffih dauda huku mpunga unamwagika upande wa pili.
 
Aheri hata hawa walisaini pre -contract na ambacho ni kitu cha kawaida, Yanga walimchezesha "Wakili Msomi "kumbe kashamalizana na Simba siku nyingi. Na mechi za watani zina pressure nyingi, wajijecheza chini ya kiwango afu muanze kuwashutumu kuwa wameuza game.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Huu ni uhuni ulioasisiwa na akina Hans Pope.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Nyie kweli mbumbumbu ao wachezaji mpira ndio maisha yao, CEO wa Simba wachezaji anao wapenda alihakikisha mikataba yao anaiongeza mapema wale wachezaji anao waona wakawaida aliwa puuza.

Watu walipo hoji akadai Simba Kwasasa Ina angalia Mambo makubwa ya Klabu bingwa Afrika. Ina maana mikataba inayo kwisha yakina Zimbwe Kapombe n.k ni vitu vidogo Sasa ata Kama niwewe kwa Nini usi sain pre contract na timu inayo onyesha nia kwa maslahi ya kazi yako na maisha yako. Mchezaji anayejitambua awezi kufanya Mambo kishabiki mpira ni kazi.
 
Angaika na upotolo yako Nyonzima alisign Simba akiwa free, Gadiel na Ajib vilevile halafu umekaa kukashifu viongozi wa Simba.
 
Mkuu shauri tufanyaje kuondoka na huu uhuni. Binafsi unanikera sana,naona kama mijinga fulani inapewa attention ya kupiga propaganda
Viongozi wawe makini, Manara ni sehemu ya menejimenti lakini anaongea kama shabiki maandazi achague moja kuwa msemaji anayefata maelekezo au abaki shabiki oyaoya.

Kuna wachezaji kama Gadiel Michael ni wazuri hawapewi nafasi kocha aanze kuwapa nafasi pia Simba imwangalie Bryson wa kmc ni mchezaji bomba
 
Nyie mtaishia tu kuwaita washabiki wa Simba mbumbumbu ila kwenye kila tukio nyie ndio mnakuwa mbumbumbu square, uongozi wa yanga hasa GSM wako vizuri Sana kwenye kutengeneza propaganda ili tu iwapumbaze mashabiki wao.

Mlianza na Morrison, mkapelekwa weee km kuku ana mdondo mkatukana matusi yote, Ila mwisho wa siku nyie ndo mkawa mbumbumbu square.

Likaja la chama mkaaminishwa nanyie mkaingia kingi, mwisho wa siku makawa vilaza tena, mkaja kwenye FCC na bado huko Hali sio nzuri.

Likaja la kuwapa lawama tff mwisho wa siku vilaza mkatoka kapa tena,likaja la waamuzi mkatoka kapa tena, mkahamia kwa makocha bado mkatoka kapa na hiyo yote ni janja janja ya GSM kutaka kuwasahaulisha kuwa wao ndio tatizo pale yanga.

Hakuna taaisi rahisi kuiongoza kama yanga akili zenu zipo kwenye Huo mwiko mliouchomeka huko Nyuma, siku mkiutoa ndio akili zitawarudia, Kwa sasa wachezaji wote muhimu Simba hawawezi kuondoka Simba kwenda yanga kuamini hivo ni matumizi Mabaya ya akili, Simba ikiacha mchezaji ujue imeona hawana mchango Kwa club.
 
Wamezusha story tusizungumzie kipigo cha Yanga dhidi ya Azam
 
Wamezusha story tusizungumzie kipigo cha Yanga dhidi ya Azam
Ndio kawaida Yao kila kunapokuwa na tukio la aibu Kwa yanga itaibuka story, kama ya juzi hapa kumuhusu Kwasi, media zetu ni rahisi Sana kutumika na hivi vilabu viwili, tusubiri litazuka lingine lipi baada ya game ya trh 8 kama mambo yatakuwa Mabaya kwao.
 
Mbumbumbu fc wana kauliyao wao ni next level lakini wacheza wengi tena waandamiz mikataba inaekea ukingoni, Yaani mchezaji mkataba unakwisha alafu meneja na mchezaji wake wasubirie huruma ya Simba?
Next level club haijui msingi wa mafanikio ni pamoja na kujali maslai ya watumishi wako, yaani CEO Lipstick mdomoni kuubwa, Kila siku anapiga picha na watu maarufu lakin hajui majukumu yake!!!
Yaani mmeshindwa kuongeza mikataba kwa wakati alafu lawama watupiwe GSM.

Kubalini mapungufu ya uongozi wenu msitupie watu Lawama. Uongozi wa Simba hasa CEO aache Show off , afundishwe namna mpira inavyo endeshwa asifikiri Bado yupo kwenye kusimamia mafuta ya kupikia na Juis za MO.
 
Huyo senzo ambae Hana show off huko upande wa utopoloni unaweza kutuambia amefanya yapi mkuu kuliko huyo mpaka lipstick wa Simba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…