OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Huyu dogo ana kipaji nina hakika hapa Simba Sc anapita tu kama njia. Ukimtazama kwa jicho la karibu utaona mpira mkubwa anaocheza. Mechi ya Asec aliupiga mpira mkubwa sana pamoja na kukosa magori kadhaa. Jana nilimfuatilia kwa karibu sana nimebaini ana madini mguuni.
Huyu akipata striker mtambo anayelijua goli atafanya fujo sana kiwanjani.
Mimi na mashabiki wenzangu wa Simba na Yanga na timu zote duniani tumekubali huyu dogo ni fundi. Kocha aendelee kumuamini ili atupe burudani.