Kwa miaka mingi sana Tanzania imekua ikipambana na watu wenye imani potofu juu ya watu wenye ualbino( albinism). Watu wanatakiwa kujua kwamba albino ni sawa na binadamu wengine ikiwa tu yeye amekosa au ana upungufu wa madini ya melanin, Albino ana haki sawa kama mtu mwingine mwenye ngozi ya kawaida.
Matukio ya kujirudia ya mauji ya watu wenye ngozi za albino yamekua yakishamiri maeneo mbalimbali ya Tanzania, kama vile Kagera, Mara, Sumbawanga, Tabora na Mtwara. Albino pasi na kuwa na hatia wamekua wakiuwawa na watu wenye imani za kishirikina uku wakichukua viungo vyao na kudai kuwapatia utajiri.
Tanzania ya miaka 5 ijayo inawezekana bila mauaji ya Albino kwa kuwatetea, kuwalinda na kuwapigania kwa kufanya mambo yafuatayo:
Elimu kwa umma, hii itasaidia sana kupunguza changamoto hii hususani maeneo ya vijijini. Watu wanatakiwa wapewe elimu kuwa watu wenye ualbino ni sawa na watu wengine kwahiyo wana haki ya kuishi kwa uhuru bila hofu, elimu hii inatakiwa itolewe kwa njia mbalimbali ikiwemo madarasani, kuanzisha matamasha, bonanza, kuanzisha programu za kusaidia wengine kujua umuhimu wa albino kama vile niwezeshe app, binti programu na pink programu ambazo huzaidia kutoa elimu kwa watu. Hii elimu ikitolewa kwa vijiji, tarafa, kata na vitongoji itawafikia watu wengi na kutoa uelewa kwa watu wengi zaidi ambapo wataacha imani za kishirikina na kupunguza vitendo vya kikatili.
Kuweka sheria kali, sheria zinatakiwa kuwekwa na kuzingatiwa ipasavyo kwa watu ambao watakutwa na hatia ya mauaji ya albino. Hii itasaidia watu kupunguza vitendo hivi vya kikatili kwa kuogopa sheria ambazo zimewekwa, kwa mfano wauaji wakikamatwa pamoja na waganga wanaowatuma wapewe adhabu kali ikiwa ni pamoja na kifungo cha maisha au kunyongwa hadi kufa kwasababu ya kuua kwa kukusudia na hii itapoozesha wengine wanaotaka kujaribu kuua. Hivyo basi vitendo vitapungua kwa asilimia kubwa sana ikiwa tu sheria zilizowekwa zitafatwa bila kusuasua.
Kutoa fursa za ajira, asilimia kubwa ya watu ambao wanaua albino ni kutokana na umaskini walionao ambapo matajiri wakiwapa pesa ili waletee viungo vya albino hupokea pesa izo ili kukidhi maisha yao. Kwahivyo serikali inatakiwa kupunguza idadi ya watu ambao hawana ajira na kutoa wimbi la umaskini ili kuwapa fursa ya kuingiza kipato chao kwa siku ambacho kinaweza kujikimu kwa maisha ya kila siku. Kesi za watu ambao wamekua wakikamatwa na viungo hivyo wamekua wakisema kuwa vinatumika kuwapatia utajiri, kwa hali hii wanatakiwa kupata ajira wezeshi ili kuwafanya wawe bize na kazi na kujichanganya na watu wenye maarifa makubwa. Hii itasaidia kupunguza mauaji ya watu wenye albino kwa asilimia kubwa.
Kuwapa adhabu waganga wa kienyeji, maeneo mbalimbali waganga wa kienyeji wamekua wakiwatuma watu kuwaletea viungo vya albino ili kuvifanyia kazi na kuwapatia utajiri. Waganga hawa wa kienyeji wamekua ni tishio maeneo mengi hususani vijijini, kwa mfano katika mkoa wa Kagera, mwaka 2024 mwezi wa 6 mtoto Asimwe( pichani)alikutwa ameuwawa na watu wenye imani potofu kwa kukatwa mikono na ulimi kisha mwili wake kufungwa na kutupwa (pichani). Watu hao wakidai kuwa walitumwa na mganga wa kienyeji kuwapatia utajiri.
Pichani( ya 1) ni mtoto Asimwe enzi za uhai wake na picha ya pili(2) ni baada ya kuuwawa na kutupwa.
Kutoa taarifa kwa vyombo vya kiusalama, watu wengi wamekua waoga kutoa taarifa kwa vitendo viovu kama hivi. Mtu yoyote anatakiwa kutoa taarifa mara tu anapoona kiashiria chochote cha kitendo cha ukatili ikiwa ni pamoja na kufatiliwa na watu wasiojulikana, kutishiwa maisha, kunyanyaswa kufedheheshwa kwasababu ya rangi na kubaguliwa. Mtu huyu anatakiwa kutoa taarifa kituo cha polisi au sehemu ya usalama ili kupatiwa usalama zaidi, pia watu wake wa karibu wasiogope kutoa taarifa wanapoona hali hii imejitokeza ili polisi waimarishe ulinzi na kuwakamata mara moja watuhumiwa. Hii itapunguza vitendo vya kiukatili juu ya watu wenye albino.
Kugawa vifaa vya albinism, ngozi ya albino huwa ni tofauti sana na ngozi ya kawaida ikiwa ni kwamba albino anahitaji mafuta kupunguza kuungua kwa ngozi kutokana na mionzi ya jua ambayo husababisha vidonda, pia kofia na miwani maalumu. Mauaji ya albino huanzia ndani ya familia na hii ni kutokana na mwanafamilia kushindwa kukimu vifaa vya albino kwasababu ya bei kuwa kubwa hivyo kupanga njama na watu za kuuwa albino huyo. Hivyo basi vifaa vya albino ni muhimu ili kupunguza ongezeko la mauaji haya.
Kutokomeza tamaduni na mila potofu, maeneo mengi wamekua na mila potofu juu ya albino ikiwa ni pamoja na kuona kuwa viungo vya albino ni mali kwamba huwapatia utajiri, lakini pia imani nyingine potofu ni kuwa mtoto akizaliwa mwemye albino katika familia fulani basi familia hiyo huonekana kama imelaaniwa na hivyo mtoto huyo anatakiwa kuuwawa mara moja ili kuondoa mikosi, nuksi na laana kwenye familia hiyo. Tamaduni hizi zinafaa kukomeshwa mara moja kwa njia mbalimbali kama vile kutoa elimu, kuwatembelea wazee wa familia na kuwapa umuhimu wa albino kwamba ni sawa na watu wengine, kutoa adhabu. Hii itapunguza na kufanya miaka ijayo kuwe hakuna mauaji ya albino.
Hitimisho
Albino siyo ulemavu, siyo ugonjwa, siyo laana. Albino ni watu kama watu wengine ni wazuri wapewe heshima yao wasidharaulike wala kunyanyaswa. Tanzania ya miaka ijayo bila mauaji ya albino INAWEZEKANA.

Upvote
5