Mimi Ni binadamu nisiye na mapungufu

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Nimekuwa nikisikia sikia Huku na huko kwamba kila mwanadamu ana madhaifu yake aidha ya kimwili,au kiakili au kitabia.kwangu Mimi Ni tofauti Sana kwani nimejichunguza kwa muda mrefu nimejijua Sina mapungufu yoyote,sifanyi makosa kwa uzembe,nafuata kanuni zote za afya Bora mfano nazingatia ulaji mzuri na wa kiasi ,Nina imani thabiti,natambua uhitaji wangu wa kiroho,najua kuzungumza vizuri,Sina mazoea mabaya,napenda Sana watu na ndo maana Nina furaha sana .sina kasoro hata moja.mnaosema nobody is perfect mlikosea mlidhani sote tuko sawa Kuna wengine hatujui roho mbaya Ni kitu gani,mwenzenu kila nalolifanya Ni Bora.Mimi huyo nawatakia jumamos njema.ndo nishamaliza
 
Mwandiko wako tu unatoa hukumu. Labda kama unarusha dongo kwa mwajina wako Chattle Beer
 
kwakuandika tu huu uzi inaonesha una mapungufu ya KUJIKWEZA
 
Kwa kutotambua hauna mapungufu NDIO upungufu wako.
 
Kuandika mada hii ni mapungufu tosha
 
Asiye na mapungufu ni MUNGU pekee,
Ila kila binadamu ana mapungufu,
Brother pengine hujui wala hujaambiwa mapungufu yako, na hiyo isiwe sababu ya ww kusema huna hayo mapungufu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…