SoC02 Mimi ni Meya wa Jiji

SoC02 Mimi ni Meya wa Jiji

Stories of Change - 2022 Competition

Tukuza hospitality

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2022
Posts
321
Reaction score
691
Meya ni neno linalotokana na neno la Kiingereza “Mayor”, ni cheo kinachotumika nchi nyingi duniani; hii ni nafasi ya juu kabisa katika halmashauri ya mji, manispaa au jiji.

Kwa mujibu waWikipedia” ya Dar es alaam, Dar es Salaam ni jiji kubwa kuliko yote nchini Tanzania, na mji mkongwe na wenye watu wengi zaidi katika Jumuia ya Afrika Mashariki. Jiji lina wakazi wapatao 4,364,541 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012, likiwa na eneo la mita za mraba 1,393.

Picha ya Angani ya Jiji la Dar  www.mwananchi.co.tz.jpg

Picha ya Angani ya katikati ya Jiji la Dar. Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Ramani ya Jiji la Dar  www.dcc.go.tz.jpg

Ramani ya Jiji la Dar. Chanzo: www.dcc.go.tz

Historia ya Dar es Salaam
Kwa mujibu wa Wikipedia” ya Dar es alaam, Jiji hili, zamani lilikuwa kijiji na kuitwa Mzizima. Sultani Seyyid Majid wa Zanzibar ndiye aliyechagua jina "Dar es Salaam" linalotokana na lugha ya Kiarabu دار السلام (Dār as-Salām) lenye kumaanisha "nyumba ya amani." Maelezo yanayopatikana mara nyingi kuwa maana ni "bandari ya salama" yanachanganya maneno mawili ambayo kimatamshi yanafanana kidogo katika lugha ya Kiarabu, yaani "dar" (دار = nyumba, makazi) na "bandar" (بندر = bandari). Hadi leo kuna majengo mawili yaliyobaki ya vyanzo hivi ambayo ni Boma la Kale na Nyumba ya Atiman House.

Dar es Salaam ilichaguliwa na wakoloni wa Ujerumani kuwa mji mkuu wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kwa sababu ya bandari asilia yenye mdomo mpana wa mto Kurasini. Hivyo kuanzia mwaka1891, Dar es Salaam ilichukua nafasi ya Bagamoyo kama makao makuu ya utawala.

Kama Meya wa Jiji, natambua Mameya 17 walioongoza jiji toka mwaka 1949 hadi 2020, kama wanavyooneka kwenye picha hapa chini:

Mameya wa Jiji La Dar toka mwaka 1949 hadi 1958  www.dcc.go.tz.jpg

Mameya wa Jiji la Dar toka mwaka 1949 hadi 1958. Chanzo: www.dcc.go.tz

Mameya wa Jiji La Dar toka mwaka 1959 hadi 1966  www.dcc.go.tz.jpg

Mameya wa Jiji la Dar toka mwaka 1959 hadi 1966. Chanzo: www.dcc.go.tz

Mameya wa Jiji La Dar toka mwaka 1967 hadi 1995  www.dcc.go.tz.jpg

Mameya wa Jiji la Dar toka mwaka 1967 hadi 1995. Chanzo: www.dcc.go.tz

Mameya wa Jiji La Dar toka mwaka 1996 hadi 2015  www.dcc.go.tz.jpg

Mameya wa Jiji la Dar toka mwaka 1996 hadi 2015. Chanzo: www.dcc.go.tz

Meya wa jiji la Dar  Isaya Chacha Mwita   www.google ..jpg

Meya wa Jiji la Dar, Isaya Chacha Mwita (2016 – 2020). Chanzo: www.google.com

Kama Meya natambua changamoto za jiji kama ifuatavyo:​

  • Makazi Holela: Kwa mujibu wa taarifa ya EATV ya Agosti 02, 2016, Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, imesema zaidi ya nyumba 430,000 ambazo ni zaidi ya asilimia 75 ya nyumba zilizojenjwa katika jiji la Dar es Salaam zimejengwa kiholela.
Hali hii inasababisha msongamano mkubwa wa watu katika maeneo husika, wenye athari hasi kwa mazingira na afya.

Makazi holela Dar .. www.eatv.tv.jpg

Picha ya Angani ya Makazi holela Jijini Dar. Chanzo: www.eatv.tv.

Picha ya Angani ya Jiji la Dar ..  www.gettyimages.ae.jpg

Picha ya Angani ya Jiji la Dar. Chanzo: www.gettyimages.ae

  • Msongamamo wa magari barabarani. Hii husababisha wakazi wengi kutumia hadi saa sita barabarani wakati wa kwenda kwenye maeneo yao ya kazi, na wakati wa kurudi majumbani kwao; ilhali wangetumia muda usiozidi nusu saa endapo kungekuwa hakuna msongamano.
  • Wimbi kubwa la watu kutoka mikoani kuja kufanya makazi jijini. Hii inasababisha msongamano, na kufanya huduma nyingi za jamii kuelemewa kila mwaka.
  • Uchache wa barabara zinazotoka na kuingia jijini.
  • Mafuriko ya kila msimu wa mvua, kiasi cha kufanya hata barabara za katikati jiji kujaa maji na kutatiza usafiri.
  • Huduma duni za usafi wa mazingira.

Mimi kama Meya wa Jiji nitafanya Nini?
  • Nitatumia siku tatu kila wiki kutembelea mitaa ya jiji. Zoezi hili nitalifanya kwa miezi minne hadi sita, kuhakikisha nafikia mitaa yote na kufahamu chagamoto zake kwa kina. Baada ya kipindi hicho, nitakuwa na ratiba endelevu ya kutembelea mitaa mbalimbali mara mbili kwa wiki.
  • Baada ya kutembelea kila mtaa, nitakaa na wataalamu wangu, kujadili hali ya jiji, na nitawaagiza kupima maeneo yote holela na kubuni miji mipya ambayo itakuwa na nyumba za ghorofa kumi na kuendelea; viwanja vya michezo; maeneo ya utalii; maeneo ya burudani; shule/vyuo; vituo vya ulinzi na usalama; hospitali/vituo vya afya; maeneo ya ibada (dini zote); masoko; maeneo ya makaburi; maeneo ya akiba (“Reserve areas”); mashamba madogomadogo kwa ajili ya kilimo cha mjini (“Urban Farming”); mitambo ya kuchakata vinyesi – kuzalisha gesi (“Bio-Gas”), itakayotumiwa na wakazi kama nishati majumbani; maeneo ya viwanda (vikubwa, vya kati na vidogo); maeneo ya kutupa taka; na maeneo mengine kwa ajili ya huduma nyingine kadri ya mahitaji ya wakazi. Mwaka wa kwanza, nitajenga majengo matano (moja kila wilaya ya jiji), ambapo kila jengo litabeba kaya zisizopungua 200. Majengo yakikamilika, familia husika zitahamishiwa huko, na nyumba zao zitabomolewa. Ujenzi wa majengo utaendelea, na wakazi kuhamishiwa huko, huku nyumba (kwenye makazi holela), zikiendelea kubomolewa hatua kwa hatua; na kasi itaongezeka kila mwaka. Wamiliki wa nyumba zilizopo kwenye makazi holela, watamilikishwa makazi (“Apartments”) kwenye majengo mapya, na makazi ya ziada yatauzwa na/au kupangishwa kwa wakazi wengine.
Miji hii itapendeza kama jiji la California, nchini Marekani, kama inavyoonekana kwenye picha hapa chini.

Jiji la Califonia USA Aug 2022   www.gettimages.dk.jpg

Picha ya Angani ya Jiji la Califonia, USA. Chanzo: www.gettimages.dk
  • Ujenzi wa miji mipya utakuwa ni programu ya miaka 15. Hii itakuwa miradi shirikishi, yaani serikali (Wizara ya Ardhi, Ujenzi, na Jiji) na watu binafsi (“Private Public Partnership – PPP”), na sitahitaji uwekezaji kutoka nje ya nchi!
  • Kwa kushirikiana na wizara husika, nitahakikisha huduma za umeme, maji, na gesi asilia zinafikia watu wote. Pia nitashirikiana na wizara ya ujenzi kuhakikisha barabara zinaongezwa na kuboreshwa, na huduma za garimoshi jijini zinaongezwa.
  • Nitawaagiza wataalamu wangu kuandaa michoro ya reli za chini ya ardhi (“Subways”) kwa ajili ya utekelezaji wa miaka ijayo.
  • Nitakaa na Mameya wa majiji mengine nchini, na kuwashauri waanzishe programu kama hii, ili kupunguza wimbi la watu wake kuja kusongamana jijini kwangu. Mwanza ni mfano mzuri, watu wengi wanaishi makazi holela, hasa vilimani!
Picha ya Angani ya Jiji la Mwanza  www.gsengo.blogspot.jpg

Picha ya Angani ya Jiji la Mwanza. Chanzo: www.gsengo.blogspot

Pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa miradi hii, utajibu changamoto zote, kama zilivyoanishwa kwenye makala hii.

Hitimisho
Mimi ni Meya, nitakayefanya jiji kuwa kivutio duniani kote, na hivyo kuwezesha nchi kupokea watalii wengi kote ulimwenguni, watakaoongeza pato la taifa.

Marejeo
EATV (Agosti 02, 2016), Nyumba 430,000 zimejengwa kiholela, DSM

Wikipedia” ya Dar es alaam

www.worldpopulationreview.com

Muhimu: Makala haya nimeandika kwa lengo la kuwafanya viongozi wa ngazi mbalimbali kutimiza wajibu wao kwa wananchi, na wananchi kujua wajibu wa viongozi wao, na kuweza kuwawajibisha pale wanaposhindwa kutimiza wajibu wao kwao; na sii vinginevyo!
 
Upvote 9
Kulipanga jiji mpaka liwe vizuri kama California itachukua muda mrefu lakini naamini inawezekana kabisa kama tukipata viongozi wawajibikaji.
Inawezekana kabisa! Siri ya mafanikio ya kila kitu ni KUANZA! Jambo la msingi kwa viongozi ni kuwa na MAONO (ambayo hayahitaji fedha), na mengine hufuata!
 
Wamarekani wanapenda nchi yao popote wawapo duniani, kwa sababu walipanga miji yao mapema. Tunaweza kuanza kupanga majiji na miji yetu sasa!
 
Tukiondoa kasumba ya kwamba kila mradi mkubwa wa .jamii ni lazima kuwe na , mkono wa mzungu, tutanya makubwa sana, ikiwa ni pamoja na kupanga vyema majiji yetu.
 
Miji ikipangwa vyema, maradhi ya kuambukiza na yasiyoambukiza yatapungua kwa kiasi kikubwa!
 
Back
Top Bottom