LGE2024 Mimi ni mpiga kura huru. Sina chama; nasubiri kuridhishwa na sera za wagombea wa mtaa wangu

LGE2024 Mimi ni mpiga kura huru. Sina chama; nasubiri kuridhishwa na sera za wagombea wa mtaa wangu

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Don Gorgon

Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
35
Reaction score
68
Mimi ni mpiga kura huru. Kama wewe una chama sikudharau wala kukuona huna maana. Kila mtu na kile anachokiamini. Usinidharau pia. Ni dunia huru hii na kila mmoja anapaswa kufanya anachojisikia.

Niliwahi kushawishiwa kujiunga na vyama fulani ila sikutaka ndoa ya hivyo. Sikutaka ndoa ambayo ingenilazimu niitetee na kuitumikia hata kama ina mbilingembilinge zisizovumilika. Nilichagua uhuru wa kupima hoja na kuzisapoti au kuzipinga.

Nimejiandikisha na nitapiga kura Uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27, Novemba, 2024. Naendelea kufuatilia wagombea wanachokisema.

Ingawa natatizwa na utekelezaji wa baadhi ya sera zinazowasilishwa, ila nimepata wagombea kadhaa ambao wamefanikiwa kuukonga moyo wangu kuhusu masuala yanayotukabili mtaani.

Sina chama nilichokibeba moyoni, ila kuna sera zinazonipa burudani pomoni. 😄

Jamani, tukapige kura, ila tusiwape kula.

#TukutaneKituoni
 
Back
Top Bottom