Sitta amekuwa mtu wa kutilia shaka kwa mtu yoyote. Katika picha hiyo anaonekana akimkumbatia mtu anayeweza kutafisiriwa kama adui yake namba moja hasa kama ulifuatilia suala ugonjwa wa Mwakyembe. Yeye mwenyewe aliutangazia umma wa watanzania kwamba Mwakyembe alipewa sumu na kundi la mafisadi, leo hii anawakumbatia tena hadharani. Kwenye sakata hilo Sitta aliongea kuliko Mwakyembe mwenyewe.
Mwaka jana aliumbuliwa na Dr Slaa kwamba mwaka 2010 alikuwa mgombea wa Chadema kabla ya kula kona na kukubali kupewa uwaziri wa A. Mashariki. Kabla ya hapo alikuwa amejaribu kuanzisha chama chake huku akiwa bado mwanachama wa Ccm, lakini itakumbukwa jinsi alivyozima suala la Richmond lililoasisiwa na kundi lake. Hii ilikuwa baada ya kutishiwa kunyang'anywa kadi ya Ccm.
Binafsi simuelewi, labda katika uzi huu kuna watu wanamjua zaidi wanaweza kutuletea ushuhuda. Unajua jinsi ambavyo amekuwa akiikosoa serikali ambayo yeye ni sehemu yake? Je anafaa kupewa nafasi kubwa zaidi ya hizi alizonazo wakati haeleweki kama ni moto au baridi? Kuna wanaotafisiri kauli zake kama msimamo wake, je tuchukue msimamo gani?