Mimi ni mwana CCM - Ninauliza kuwa Ilani ya CCM iliandikwa kufuata utaratibu gani?

koryo1952

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2023
Posts
1,289
Reaction score
2,199
Kama nilivyoeleza hapo juu mimi ni mwana CCM na juzi niliona ilani ya CCM ikiwasilishwa mbele ya Mkutano Mkuu kule Dodoma.

Kwa kawaida na kwa utaratibu ilani inatakiwa ianzie kwenye ngazi za chini (grassroot) wakiulizwa maoni yao na hii inatakiwa iwe kwa nchi nzima na baadaye maoni haya yanajumuishwa kwa pamoja na kupitiwa na watalaam na baadaye Ilani Kuu inapatikana. Taratibu zote zinatakiwa kufuatwa kama ilivyokuwa kwenye Dira ya Taifa.

Mimi ninauliza kama Ilani haikuchukua mawazo ya wanachama na imeandikwa na watu wachache tu. Kwa nini wasingetumia utaratibu wa kujumuisha wanachama kuanzia ngazi za chini ili pia wapate mawazo yao?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…