Mr godwin
New Member
- Jul 29, 2021
- 2
- 1
MIMI NI NANI?
Naishi maisha katika giza kila nifanyalo haliendi likienda sifikii malengo niliyojiwekea
MIMI NI NANI?
Marafiki wananipoteza sioni ubaya katika wema kila ninaloishi leo ni katika kufurahisha watu ilihali mambo yangu hayaendi
MIMI NI NANI?
Nilienda chuo kusoma kitu ambacho sikuwahi kujua kinahusiana na nini zaidi ya kuangalia mitandaoni mwisho wa siku nimeishia kuzunguka na vyeti mitaani kama mtu niliokosa mwelekeo
MIMI NI NANI?
kichani kwangu nawaza niweke shilingi mia tano kwenye mchezo wa kubashiri ili nimle muhindi milioni mia tano
MIMI NI NANI?
familia yangu inanitegemea hakuna zaidi yangu wakuwatoa katika umasikini stress zinaniandama umri unakatika sina mke wala mtoto
MIMI NI NANI?
utandawazi umenitafuna hapa nilipo nimebaki mifupa ujanja kwangu nikuwa na wasichana wengi,kupiga picha na kupost mitandaoni
MIMI NI NANI?
siioni kesho yangu katika mimi siioni leo yangu katika mimi maisha yangu nikama nabahatisha sijui mwisho wangu ni nini
MIMI NI NANI?
marafiki nilio soma nao wengi wao wamefanikiwa hata kujilipia kodi mimi bado nipo home kila nikiamka nawaza ni mkubwa kapika nini
MIMI NANI?
kila nikiona wenzangu wamefanikiwa nahisi ni nguvu za giza sioni kama watu wanaweza kufanikiwa na jitihada zao
UJUMBE
Tubadilishe mitazamo ya fikra zetu still tuna nafasi yakupambana kama vijana wa taifa la kesho tusikate tamaaa

Upvote
2