SoC02 Mimi ni USAILI/INTERVIEW''; Kilio cha Usaili. Je, Wapi nakosea?.

SoC02 Mimi ni USAILI/INTERVIEW''; Kilio cha Usaili. Je, Wapi nakosea?.

Stories of Change - 2022 Competition

Funa the Wild

Senior Member
Joined
Aug 1, 2022
Posts
167
Reaction score
282
Miongoni mwa jambo pasua kichwa kwa watafuta ajira wengi wenye vyeti vilivyoosheni GPA zenye vigezo vya mtu kupata nafasi ya kuwajibika eneo husika basi kuhusu USAILI huwezi kuacha kuzungumzia. Kuna haja ya kuliangalia hili swala la mfumo wa umimi/ubinafsi katika mfumo mzima wa usaili. Ukatishwaji tamaa unaongezeka siku hadi siku na kuzidi kuwalaumu wenye vyeti vyao vyenye vigezo kuwa hawajitumi na ni wakaa bure tu.

Mfano, Maeneo mengi ya kazi huwa yanahitaji watu wenye sifa na vigezo kadhaa, kupata nafasi ya kazi kwenye eneo husika huwa kunakuwa na utaratibu wa kufanya usaili na idadi kubwa ya watu huwa inajitokeza. Lakini nyuma ya usaili huwa kuna siri kubwa sana imejificha, Idadi ya watu wanaohitajika huwa inatangazwa lakini asilimia kubwa ya hao watu wanaohitajika wanakuwa tayari washaandaliwa nafasi katika eneo husika nikimaanisha kujuana kunachukua nafasi kubwa sana, na wao huwa wanafika eneo la usaili kama ushahidi. Je, huwa kuna haja gani ya kutangaza nafasi za kazi wakati mnajua dhahiri mshaandaa mipango yenu binafsi?. Je, huwa mnawafikiria na wale wasiojulikana wanaotumia mda wao kusafiri na kufika eneo husika?.

Je, ni kwa nini wahusika wenye izo nafasi wakapigiwa simu wakaja wao tu?. Majibu yapo katika vichwa vyenu. Kuna mambo ya kuyaangalia na kuyabadilisha yasizidi kukatisha tamaa kwa wenye nia ya uhitaji.

KUONDOA UMIMI/UBINAFSI, Huu ni miongoni mwa mfano ulio hai, Mwezi uliopita kulikuwa na usaili wa kuhesabu watu na makazi, kuna mambo yalikuwa yakifanyika yalikuwa yakiacha mdomo wazi, waulizwaji walikuwa wakiulizwa maswali lakini wakimaliza kuulizwa waulizaji walikuwa hawanukuu taarifa zozote za mulizwaji na mwisho huambiwa wasubiri majibu. Hii inafikirisha sana na kuonesha picha kwamba UMIMI bado unazidi kukua. Na cha ajabu zaidi baada ya majibu ya usaili kutoka wale waulizaji maswali majina yao yalikuwemo kwenye miongoni mwa watu watakaohusika kufanya shughuli hizo.


KUHUSU UZOEFU ISIWE CHANZO CHA KUMYIMA MTU NAFASI, Ndiyo uzoefu wa kazi ni muhimu sana katika kufanya kazi husika kwa ufasaha zaidi. Lakini pia huwezi ukaanza juu ukawa unashuka chini, ni lazima uanze chini ili upande juu. Unamfanyia mtu usaili na kutaka awe na vigezo vya uzoefu. Mtu anapokuwa anaomba nafasi juu ya nafasi ya kazi basi huwa kuna mengi anatarajia kujifunza na kuzidi kupata uzoefu wa kazi na utendaji wa kazi kuongezeka. Lakini pia hili inatakiwa liangaliwe kwa upande wa pili kwa watafuta ajira pia.

Degree husomwa kwa miaka mitatu, minne hadi mitano, ndani ya miaka iyo kuna mafunzo ya vitendo huwa yanafanyika (Field practical training), kupitia mafunzo ya vitendo wengi hupata mafunzo na ujuzi juu ya taaluma wanayosomea. Ilo pia lizingatiwe kwenye vigezo.

Mfano, Nilishawahi kutembelea mkoa wa ruvuma katika wilaya ya Tunduru kwenye kijiji cha Nakila, pale kulikuwa na mzee jina lake nalihifadhi alikuwa akitueleza mambo mbalimbali juu ya changamoto wanazokumbana nazo juu ya ugomvi wa wananchi na wanyamapori wanaoharibu mazao ya wananchi. Kuna Mengi tulimuuliza hasa kuhusiana na uzoefu wa izo kazi, alichojibu ni kwamba, yeye alizidi kupata uzoefu kadri alipokuwa akifanya kazi kwenye lile eneo.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom