Mimi ninaamini, nyuma ya migogoro mingi ya Muungano inayoibuliwa na Wazanzibar, kuna kitu kimejificha!

Mimi ninaamini, nyuma ya migogoro mingi ya Muungano inayoibuliwa na Wazanzibar, kuna kitu kimejificha!

Nsanzagee

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2023
Posts
2,209
Reaction score
4,769
Kero nyingi za Wazanzibar kuhusu muungano, huibuliwa na kuchochewa na wanao kaa nje ya Zanzibar yaani wapo Ughaibuni huko, sisi tulioko huku tutawaaminije kama hawakutani na kutumwa na maadui wa muungano wetu na wenye masilahi binafis?

Badala ya kurahisisha tu kwamba muungano uvunjwe au wabara ili wafike Zanzibar ni lazima wawe na paspot za kusafiria, kunahitajika uchunguzi maalumu kubaini hizi kero na kelele nyingi zinazoibuliwa na upande wa Zanzibar kwa uchunguzi maalumu

Kwa masikio yangu, naona kipindi hiki ndio kimeongeza saana kero za watu hasa Wazanzibar kuuchokonoa muungano

Kwa kipindi hiki hasa kutokea Kwenye kubinafisisha Bandari za Bara, kumekuwepo na mipasho mingi na kutupiana mipira kuhusu hilo na sasa tunaendelea kusikia maneno maneno ya kwa nini muungano??

Mambo haya ba hiyo nguvu inayotumika inatoka wapi?

Tukiondoa hizo kelele, ni nani anayenufaika zaidi kupitia muungano huu kati ya Bara na Zanzibar?

Hizi kelele za muungano kuongezeka na kuzizidi sana, zinatoka wapi? ni mhimu kujiuliza zinatoka wapi na kwa faida ya nani

Mimi naamini, Bado hata Wazanzibar wanauhitaji muungano kwa walio wengi ukiondoa hao wanasiasa wenye uchu wa kujinufaisha wao na watoto wao.

PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?
 
Kwa kifupi huu Muungano unalindwa kijeshi,si kwa matakwa ya wananchi wa pande zote! Wananchi wengi walishaukataa hasa wa upande ule!
 
Hawataki muungano wa shuruti, nini hakieleweki hapo?
Muungano wa shuruti kulindwa na mabunduki, ni muungano wa viongozi Kula nchi na kugawana vyeo wao na familia zao,
Atakayejaribu kuuvunja Muungano atavunjika yeye nukuu ya Hayati Magufuli
 
Mkuu una maana watanganyika au wazanzibar hawana uwezo wa kufikiri na kuona changamoto za muungano. Haya Mkuu ni matusi kwa watanzania, tena ya reja reja!!
 
Hakuna muungano duniani wa kipuuzi kama huu wa Tanganyika & Zanzibar.waliouunganisha walikuwa na udumavu wa akili.walikubaliana watu wawili tu na kuuita muungano.Muungano unatakiwa upigiwe kura na wananchi siyo watu wawili tu wanakaa mezani kunywa kahawa na kuunda Muungano.
 
Kero nyingi za Wazanzibar kuhusu muungano, huibuliwa na kuchochewa na wanao kaa nje ya Zanzibar yaani wapo Ughaibuni huko...
Ndugu yangu skia,

Katika kipindi hiki ndicho tumefanikiwa kupata viongozi wengi ambao matendo na kauli zao zinaleta mashaka makubwa kuhusu uwezo wao wa akili na hekima. Hawana wanalolisimamia zaidi ya kuhakikisha wanasalia madarakani hata kama itagharimu nusu ya damu za watanzania wasio na hatia.

Usitegemee, akili za kusifia sifia na kujipendekeza zinaweza kuleta busara ya kuimarisha Muungano zaidi ya kuusifia uliopo na mapungufu yake. Inaleta simanzi kubwa sana kwa uwezo huu duni wa viongozi wetu. Inaleta mashaka sana kwa sababu asilimia kubwa ya wateuliwa wameonesha uwezo wao mdogo ama kukosa kabisa uwezo wa kutatua changamoto za jamii. Kama inafikia mahala Waziri anatoka ofisini na kwenda kusimamia maamuzi ya serikali kwenye migogoro ya ardhi ndo ujue kada kubwa ya viongozi hawatoshi kukabili na kutatua changamoto za jamii yetu.

Muungano una changamoto nyingi sana. mojawapo ya changamoto hizo ni muundo wa serikali na utambuzi wa mipaka ya nchi zilizoungana. pia issue ya Katiba ya Muungano nayo ni utata utata ndo maana viongozi wanatumia kauli za vitisho kwamba wataulinda Muungano kwa gharama yeyote. Kwa mtu unayemuona wazi kabisa hana uwezo mzuri wa kimaamuzi anapoapa kutumia gharama yeyote kuulinda Muungano ni lazima tuweke kiulizo hizo gharama kama hazitagharimu maisha ya wanaouhoji na kuukosoa.

Kiufupi mimi naona kilichopo nyuma ya haya ni UGAI GAI wa viongozi wetu na wale wenye maslahi ya moja kwa moja na Muungano
 
Wazanzibar wanafaidi gawio lao na upande wa pili wanafaidi gawio Tanzania yote ambayo wao pia ni watanzania, watanganyika sisi tunafaidikaje nje ya hilo gawio la muungano ambalo wazanzibari pia wanalifaidi kwenye muungano na kwenye uzanzibari!?
 
Wazanzibar wanafaidi gawio lao na upande wa pili wanafaidi gawio Tanzania yote ambayo wao pia ni watanzania, watanganyika sisi tunafaidikaje nje ya hilo gawio la muungano ambalo wazanzibari pia wanalifaidi kwenye muungano na kwenye uzanzibari!?
Hawa wazanzibari wamebakiza kutushika makalio tu
 
Back
Top Bottom