Mimi sio kichaa! Kama CCM watatoa fomu moja ya urais 2025 na wakampa mmoja tu - Nitakwenda mahakamani!

Mimi sio kichaa! Kama CCM watatoa fomu moja ya urais 2025 na wakampa mmoja tu - Nitakwenda mahakamani!

Mganguzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2022
Posts
1,604
Reaction score
3,715
Kutangaza nia sio kosa kisheria, na demokrasia tuliichagua ili tuifuate. Sasa kama chama changu CCM, kitaninyima haki ya kugombea 2025!

Na mwenyekiti akaruhusu fomu iwe moja tu! Na wakampa mmoja tu! Basi kwa mara ya kwanza nitakwenda kudai haki yangu ya kikatiba mahakamani, taratibu za chama sio katiba ya nchi, nitapewa fomu ya urais kupitia mahakama kuu!
 
Paskali Mayala anahusikaje na hii move yako?
 
Paskali anataka kugombea tena??? Jamaa hajui kukata tamaa kabisa.....japo ccm wanamkata ila hakatiki
 
kutangaza nia sio kosa kisheria, na demokrasia tuliichagua ili tuifuate. sasa kama chama changu c.c.m, kitaninyima haki ya kugombea 2025! na mwenyekiti akaruhusu fomu iwe moja tu! na wakampa mmoja tu! basi kwa mara ya kwanza nitakwenda kudai haki yangu ya kikatiba mahakamani., taratibu za chama sio katiba ya nchi ,nitapewa fomu ya urais kupitia mahakama kuu!
Japokuwa sipendi siasa lakini wewe huna sifa za kuwa Mgombea wa chama chochote hapa Tanzania achilia mbali urais hata udiwan

Ikifika 2024 gombea Uenyekiti was vitongoji/Kijiji huko waweza Kupata.
 
Kutangaza nia sio kosa kisheria, na demokrasia tuliichagua ili tuifuate. Sasa kama chama changu CCM, kitaninyima haki ya kugombea 2025...
Amka usingizini, na ndoto hii ikikupeleka chooni, usinye utajinyea haupo chooni, unaota.
 
Hiyo ni jadi ya chama. Mbona chama fulani akijitokeza mtu anaetaka kugombea nafasi ya uenyekiti huitwa na wazee ili kumshawishi aache mpango huo kwa madai kuwa atakigawa chama? Na bado hukuwahi kuhojo hilo mahakamani!!
 
2025 CCM itapitia wakati mgumu, maana utaratibu ni kwamba lazima makada wajitokeze kugombea nafasi ile.

Kumpinga Mwenyekiti wa CCM waziwazi kuwa unataka kiti chake ni mtihani mkubwa. Refer ya Membe 2020.

Japokuwa hii scenario ni mpya. Maana Rais aliyepo ni kutokana na matakwa ya kikatiba, ukakasi ni huu, Mzanzibari, Mwanamke.

Wa kuiokoa CCM 2025 ni wafuatao, Abdulrahman Kinana, Mstaafu Kikwete, Dr. Shein wa Zanzibar, Mstaafu Mangula, Mstaafu Pinda, Mstaafu Msuya, Mstaafu Mwandosya. Hawa lazima watoke hadharani na kuweka msimamo ili CCM ibaki kitu kimoja. Makada wanaoota Urais lazima wapewe maelekezo vinginevyo...
 
2025 CCM itapitia wakati mgumu, maana utaratibu ni kwamba lazima makada wajitokeze kugombea nafasi ile...
Hivi ukichukuwa fomu ni kikao gani kinachojadili na kuchuja na kukaa wagombea?

Ukipata jibu la swami hili usinijibu, maana Tanzania INA wajinga wengi Sana.

Samia ndio Mwenyekiti wa Ccm, inawezekana wengi humu hamjui nini maana ya Mwenyekiti na Amiri Jeshi mkuu.
 
Kwanza kitendo tu cha kuchukua fomu ya kugombea nafasi na Mwenyekiti wako tayari ni kutangaza vita.

Suala la yeye kujadili au kutokujadili majina ni suala la kikanuni lipo wazi kabisa, kikanuni ukiwa unagombea nafasi hutakiwi kuwajadili wengine. Ila influence ya Mwenyekiti inajulikana, hasa kofia ya Urais aliyonayo.

Abdulrahman Kinana hayupo hapo kwa bahati mbaya. Mtihani wake ni 2025.
 
2025 CCM itapitia wakati mgumu, maana utaratibu ni kwamba lazima makada wajitokeze kugombea nafasi ile...
Hivi kule chadema hakuna wazee wastaafu wa kushauri, mbona unataka ushauri kwa ccm tuu?
JamiiForums2014173048.jpg
 
2025 CCM itapitia wakati mgumu, maana utaratibu ni kwamba lazima makada wajitokeze kugombea nafasi ile...
Huyo mzanzibar unayemzungumzia anamalizia awamu ya 5 aliyorithi, hakuchaguliwa popote wala hakupitia huo mchakato wa chama wa kuchuja wagombea. Iweje mtake mchakato wa kutopingwa ufanyike kwa mtu aliyerithi?

Walikimbilia kuiita awamu ya 6 kimkakati kabisa ilhali kiuhalisia hii ni awamu ya 5. Hao ccm wasitake kutuvurugia nchi maana watu watauana wasipolipatia hili swala muafaka. 2025 makada waachwe huru wagombee, watu wamchague mtu wao wanayemtaka.

Huyo Mzanzibar kama kanogewa sana naye agombee na wanaume wa bara ndani ya chama aone kama watu wanamtaka aendelee kuwaongoza au la, ila kulazimishiwa kiongozi kwa ajili ya maslahi ya kakundi kadogo hatukubali asilani.
 
Mahakama haiwezi kuingilia taratibu za ndani ya chama, cha kufanya ungedai haki ya mgombea binafsi ili ukinyimwa hiyo haki huko chamani usimame kama mgombea binafsi au uhamie chama kingine........ukiritimba wa madaraka umekuwa mkubwa nchi hii, ndo hapo taasisi zetu zikiwemo mahakama, taasisi za kusimamia siasa, demokrasia na uchaguzi, zinatakiwa kuwa huru na kuendeshwa kwa taratibu na sheria.​
 
Utapoteza muda na fedha zako bure. Kwasabb mtoa hukumu huko mahakamani ni huyo huyo aliyepewa fomu moja. Mahakama hutumika tu kama toilet paper yake
 
Kutangaza nia sio kosa kisheria, na demokrasia tuliichagua ili tuifuate. Sasa kama chama changu CCM, kitaninyima haki ya kugombea 2025!

Na mwenyekiti akaruhusu fomu iwe moja tu! Na wakampa mmoja tu! Basi kwa mara ya kwanza nitakwenda kudai haki yangu ya kikatiba mahakamani, taratibu za chama sio katiba ya nchi, nitapewa fomu ya urais kupitia mahakama kuu!

Siku hiyo ndio utajua hakuna mahakama huru hapa Tanzania, bali majengo ya mahakama yanaendeshwa na Makada wa CCM wanaotii watawala.
 
Back
Top Bottom