Mimi sio mjuzi kabisa wa magari,nataka kujua kitu hichi

Uhuru24

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2015
Posts
4,112
Reaction score
4,361
Kwanini watu wengi hasa bongo hawapendi kabisa magari ya HYUNDAI,shida ni nini kufanya sio maarufu magari haya hapa bongo.
Ukiyatazama ni magari yanavutia sana kwa muonekano wa nje,kwa machache ninayoyaona yana muonekano wa upya kabisa.

Sasa shida ipo wapi kwa hii mikoko watu kutovutika nayo,unakuta mtu ananunua toyota hata aiyeleweki kuna wakati unakutana na gari barabarani mpaka unajiuliza huyu mtu kanunua au katunukiwa kazini.

Mwenyez Mungu akinijalia nikivuna pilipili zangu,ufuta na vitunguu nataka nijitwike hili dubwana.

Wenye uzoefu na hili dubwana tupeni changamoto zake kwanini watu wanazikwepa hizi gari.
 
Bei yake mkuuu. Hayona vifaa vyake sio yebo yebo Kama toyota
 
Nafikiri ni ile kasumba tu kwamba watu wamezoea Toyota. Pia upatikanaji wa vifaa vya toyota ni rahisi kulinganisha na aina zingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…