Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Hiki kitabu ninakisoma hivi sasa.
Bado sijakimaliza lakini nimejifunza mengi katika historia ya Makomredi wa Zanzibar na ushawishi wa Abdulrahman Babu katika fikra za siasa za mrengo wa kushoto zilizokuwa Zanzibar miaka ya 1950 hadi kufikia mapinduzi mwaka wa 1964.
Hashil Seif anaeleza toka mwanzo nia ya Makomredi kupindua serikali ya Zanzibar na kuweka utawala utakaofuata siasa za ki-Marxist.
Kwa ajili hii anaeleza namna Ali Sultan aliyekuwa kiongozi katika ZNP alivyofanya mpango wa mafunzo ya kijeshi kwa makomredi kwenda Cuba kujitayarisha kwa jukumu hili.
Kitabu kinaeleza msuguano uliokuwa ndani ya ZNP hadi kupelekea Babu kufungwa kwa kile Comarade Hashil anaeleza ni njama baina ya wahafidhina ndani ya ZNP na Waingereza.
Juu ya haya yote Hashil ameeleza kwa utulivu mkubwa haiba za wanasiasa wa Zanzibar kama Ali Muhsin ambae kamtaja kwa sifa yake ya "Zaim," yaani Kiongozi, Muhammad Shamte, Ahmed Mohammed Nassor Lemki, Khamis Abdalla Ameir, Badawi Qulatein kwa kutaja wachache ...naendekea kukisoma kweli hiki si kitabu cha mtu kukikosa...
In Shaa Allah nitarejea nikikimaliza.
Kulia ni Hashil Seif, Amour Dughesh na aliyekaa ni Mussa Maisara