Minazi kupunguza gharama za mbao za ujenzi

Andres

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2013
Posts
502
Reaction score
815
Wakuu Habari za muda huu?

Miaka kadhaa kidogo kuna mdau alitoa ushuhuda wa namna ambavyo minazi hutumika kupunguza gharama za mbao kwa ajili ya ujenzi. Kwa maana ya kwamba, kuna maeneo sikumbuki vizuri lakini ni njia ya kusini, mbagala kule. Watu hununua minazi kwa wamiliki wa mashamba na kukata mbao huko kwa gharama nafuu especially kwa wenye ujenzi mkubwa kidogo. Gharama zake hupungua hata nusu ya bei ya kawaida ya mbao.

Sasa basi Nimeutafuta huo uzi bila mafanikio, na nahitaji kweli hiyo huduma.

Naomba mwenye ufahamu wa hii njia mbadala ya kupunguza gharama za mbao za ujenzi anifahamishe [emoji1431]
 
mkuu, rahisi aghali, nimepata kuona milango na frem zake zilizotengenezwa kwa mbao za minazi

sikushauri, zinapukutika tu na zina miaka haizidi 6
 
Ni kweli mkuu milango au mbao za mnazi hupukutika na kuwa Kama vumbi jepesi la maranda
 
U

Usithubutu Mkuu utajuta mbao hizo za mnazi hupukutika na kuwa Kama vumbi jepesi la mbao
 
Mkishindwa gharama za ujenzi hakikisha unapanga kwenye makazi bora
Watu wanaogopa bure bei za pango
Ila nakwambia gharama za kujenga sio za kubip
Kwanza ni huku Africa tu watu ndio wanajenga jenga sehemu zingine ni kodi za pango tu
 
Ni kweli mkuu milango au mbao za mnazi hupukutika na kuwa Kama vumbi jepesi la maranda
mkuu, rahisi aghali, nimepata kuona milango na frem zake zilizotengenezwa kwa mbao za minazi

sikushauri, zinapukutika tu na zina miaka haizidi 6
Ukiona mbao za mnazi zinapukutika basi jua mti wake ulivunwa kabla haujakomaa..tena Kama ni huku DSM kuuziwa mbao za Aina hiyo ni kawaida sn maana watu wapo after money zaidi

Mkuu Andres Mimi nimejenga nyumba kijijini na mbao za kenchi nilizotumia kuezekea bati ni za mbao za mnazi na watu wote siku hizi huku kijijini nilipojenga ndy mbao wanazotumia na ni imara sn kuliko mbao za Aina nyingine

Masharti ya mbao za mnazi Kama unahitaji Kwa ajili ya kuezekea bati(kenchi):

1.Hakikisha umekamilika Kwa kila kitu kisha ndiyo unavuna mti wa mnazi kupata mbao then unagongelea bati wiki moja baada ya kuvuna au isizidi mwezi

Why?
Kwa sababu mbao za mti wa mnazi uliokomaa ukivuna kisha zikakaa ndani zaidi ya mwezi zikianza kukauka zina Tabia ya kusinyaa,na zikishasinyaa ukiweka bati kisha ukapiga msumari,msumari unapinda au haupiti kabisa maana zile nyuzinyuzi zinakuwa zimeshikana kisha kupelekea kutoacha nafasi

3.Siku ukiamua kuezua bati kwenye nyumba iliyoezekwa kenchi za mbao za mnazi bati zinaharibika sn

Why?
Kumbuka siku uliyoezeka bati zako mbao za kenchi zilikuwa mbichi ili kurahisisha misumari ipite.Sasa baada ya mbao kukauka,misumari inakuwa imetaitiwa sn maana mbao zilinywea(kumbuka mbao za mnazi zina nyuzinyuzi na ndy upelekea msumari kutopita endapo utagongwa mbao ikiwa imeshakauka)
Kwa hiyo siku ukiamua kuzitoa bati juu misumari inakuwa imeshikilia sn kwenye kenchi na kupelekea ugumu wa kuing'oa,hivyo bati kuharibika,tofauti km zingewekwa mbao za Aina nyingine

NB:Mimi siyo mtaalamu Ila nimeongea Kwa experience niliyoipata baada ya kuwa karibu na mtu wa mnazi na kuutumia kwenye nyumba yangu
 
Wakuu Habari za muda huu?

Miaka kadhaa kidogo kuna mdau alitoa ushuhuda wa namna ambavyo minazi hutumika kupunguza gharama za mbao kwa ajili ya ujenzi. Kwa maana ya kwamba, kuna maeneo sikumbuki vizuri lakini ni njia ya kusini, mbagala kule. Watu hununua minazi kwa wamiliki wa mashamba na kukata mbao huko kwa gharama nafuu especially kwa wenye ujenzi mkubwa kidogo. Gharama zake hupungua hata nusu ya bei ya kawaida ya mbao.

Sasa basi Nimeutafuta huo uzi bila mafanikio, na nahitaji kweli hiyo huduma.

Naomba mwenye ufahamu wa hii njia mbadala ya kupunguza gharama za mbao za ujenzi anifahamishe [emoji1431]
Huku Kisarawe wanatumia huo lakini wanachanganya na 2*2 Kama papi maana ukigusa maji unaoza so Inapopita misumali Wanaweka surplus.Siku ukigusa maji jiandae kwenda milembe.
 
Mkishindwa gharama za ujenzi hakikisha unapanga kwenye makazi bora
Watu wanaogopa bure bei za pango
Ila nakwambia gharama za kujenga sio za kubip
Kwanza ni huku Africa tu watu ndio wanajenga jenga sehemu zingine ni kodi za pango tu
Huko sehemu nyingine za dunia, halmashauri za Wilaya zinakua na nyumba za kupangisha wasio na uwezo wa kumiliki nyumba zao. Lengo ni kuhakikisha kila raia anaishi katika mazingira bora.
 
Kuna soko kubwa katika kupanda miti ya mbao. Mitiki huchukua miaka kumi tu kupanda hadi kuvuna. Ukiwa na ardhi ya eka mbili ukipanda mitiki 200 baada ya miaka kumi umeuaga umaskini.
 
Back
Top Bottom