Radium
JF-Expert Member
- Aug 5, 2022
- 489
- 869
Kikwazo kikubwa kabisa cha kuufikia uelewa wa mtu binafsi na maisha ya furaha, ni uwezo wa upande mmoja wa ubongo kuudanganya upande mwingine. Tunajidanganya kwa sababu ambayo inaweza kuonekana kama sababu ya msingi mwanzoni, KWASABABU TUNATAKA KUEPUKA MAUMIVU. Lakini kwa kufanya hivyo tunaharibu sana chance za kuwa na furaha.
Nitaongelea mambo manne ambayo sanasana watu hujidanganya kuhusiana nayo kila yanapokuja kichwani.
#1. Tunajidanganya kuhusu kila jambo ambalo ni tatizo ndio ila ikija swala la kulibadilisha au kuliacha jambo hilo, ni vigumu mno na litahitaji nguvu kubwa.
KAZI MAHUSIANO AFYA TABIA NA MITAZAMO(IDEA)
#2. Tunadanganya kwa sababu tunataka kujifikiria vyema na kujiona sawa, hivyo bongo zetu zimeshikamana na wazo la kuwa tuko sahihi. Hatuna chuki za ajabu, hatupendi vitu vya kipuuzi na wala hatuna mawazo ya kishetani bwana😏.
#3. Tunadanganya kwa sababu hatutaki kujisikia kama hatutoshi na hatujakamilika, na yote ni kwa sababu tulivyoumbwa tumekosa mengi mazuri.
#4. Tunadanganya kwa sababu tunachukizwa na tunakerekwa na watu ambao ni wazi kabisa tunatakiwa kuwapenda. Na tunadanganya kwa sababu kinachotukera kinachotufanya tushindwe kuwapenda ni kitu cha kipuuzi kwa mtu mzima kujali😖.
Juu ya uhalisia wa jinsi ukweli utakavyotuchoma, imebidi tujifunze kuwa watabe kwenye udanganyifu. Mbinu zetu zinatofautiana, za kijasusi na mara nyingi huwa ni za kufikirika.
Mbinu zinazoongoza kutumika kukamilisha suala zima la kuudanganya ubongo na kufunika pazia zito mbele yetu ili tusione ukweli ni nyingi na hizi ndizo zinazoongoza.
#1. DESTRUCTION/ADDICTION.
Tunatafuta kitu ambacho kitatuweka ufukweni mwa bahari ya mawazo na ukweli uanotusibu hivyo hakuna nafasi au muda wa kuvifikiria.
1.ONLINE PORNOGRAPHY
2.TAARIFA NA MIJADALA
3.POMBE
4.KAZI
Hatuvipendi vitu hivi binafsi, tunavipenda kwa uwezo wake wa kutuweka mbali na tunayoyaogopa.
#2. FURAHA KUPINDUKIA.
Sisemi hatuna haki sasa ya kufurahi wakati wa kutafuta furaha, ninaongelea ile mtu anakuwa manic cheerful. Yani mtu anakuwa na furaha sio kawaida , full vicheko kwenye kila kitu utani na kila mtu na hakuna muda wa kuboeka. Hatuna na hatutakuwa na furaha kiasi cha kukosa jambo lakutufanya tuhuzunike hata kidogo. Yote ni kujilisha upepo na kuficha mateso underground. Mtu huyu ukimuuliza vipi utasikia "kila kitu kipo shwari" "oya wee unyama sio poaah" kwa sauti bashasha na vicheko(sio kawaida). Ukikaa kimya ataongea yeye asiache nafasi yoyote ya kufikiria.
#3.POVU.
Hasira yoyote iliyofichwa au kukanushwa mara nyingi kama si zote huibuka kwa mbadala wa povu kwenye kila kitu. Uongo tuliouset ndani ya vichwa unafanikiwa hata kiasi cha kushindwa kujua nini hasa tatizo letu. Inakuwa ni mwendo wa kufoka tu, "inakuwaje kuna mayai mawili tu ndani ya friji na limejikalisha tu pale" "sukari imeisha tangu jana ndo mnasema leo kwani hamkuona wakati mnaimalizia, ekeni chumvi😠" "nimeita mara zote izo hasikii, hizi dharau ni kutafutiana kesi" au hata mama zetu wanaposema "si hamtaki kufungua mngeacha niliwe na mambwa" "na mtanipa maelezo zile risiti za bill na ada mmezipeleka wapi"
Kila kitu kinazidi kutuchafua nafsi na nyumba inawaka moto watoto wanawahi kulala. Bongo zetu zimejaa masikitiko na hatutaki kutulia na kufocus na mawazo yanayohuzunisha.
#4. KUKANUSHA.
Tunajiambia kwamba kiuhalisia wala hatujali kuhusu kitu fulani na wala sio kipaumbele chetu.
Mapenzi ni upuuzi tu, siasa zitanisaidia nini, kazi...masomo....yule mwanafunzi mrembo au nyumba ambayo infact tumeshindwa kufika bei(kwasababu ya ccm tunasema😐).
Tuna bidii kubwa sana ya kuonyesha kiasi ambacho wala hatuna mpango na upuuzi huo. Tunaenda mbali zaidi kuweka wazi wazi kwa wengine na kwetu wenyewe ni jinsi gani vitu hivyo havitushtui kabbisakabisa na kama havipo au hatuvijui.
#5..
Kwanini kujidanganya ni tatizo?
Tunapaswa kujiambia ukweli kwa kiasi chochote kile kwa sababu huwa gharama za utulivu wa muda mfupi ni kubwa mno. Tunakosa nafasi za kukua na kujifunza, sio raha hata kwa watu kuwa karibu yetu, tunakuwa harmful kwetu na kwa wengine. Na bado ukweli utaibuka tu, tukiuficha utaibuka kwa matendo tu(involuntary physical symptoms)
*Insomnia(kushindwa kulala vizuri) *Impotency(kushindwa kusimamisha) *Unakuta mtu mkono au jicho moja linatetemeka *kigugumizi *kupiga mayowe na kuongea usingizini *low energy ma depression.
*WE OWE IT TO OURSELVES TO DARE TO START TO CONFRONT OUR REAL NATURE.