Ningekuwa na uwezo wa kuwakusanya waumini wa dini za Kiislam na Kikristo ningewalaumu kwa kugeuka kuwa watumwa wa dini kiasi cha dini kuwapelekesha kinyume na kusudi la Mungu kuhusu uumbaji wa mwanadamu. Kama dini hizi ni za kweli na Mungu Muumba mbingu na nchi anazithamini dini hizi basi tuzitumie kumwomba mahitaji ili atujalie. Yeye anaweza kushusha moto, kuleta amani, kunyamaza ili watu wake wajifunze jambo fulani, kuruhusu jaribu hata kama ni vifo; kwa kifupi Mungu anajua yote anaweza yote. Je, sisi na dini zetu hizi mbili zilizogeuka janga la dunia tunaweza kumsaidia Mungu kwa kuuana ili baadaye tumwone Mungu?
Ninawasihi watanzania waumini wa dini hizi tuishi kwa kuzingatia uhalisia ulivyo; dini hizi tumezitengeneza na kuzistawisha sisi. Tusije tukasaidia kuchipusha mbegu ya chuki ambayo adui anaipanda kwa ujanja mkubwa kupitia dini. Tukumbuke kuwa Mungu alituumba ili tumwabudu yeyesiyo dini zetu. Tujiulize dini hizi zilianza lini? Je, waliotutangulia ambao tunawaita baba/Babu zetu wa imani: Adam, Eva, Nuhu, Ibrahim, Lutu, Daudi na wengineo walikuwa waumini wa dini gani? Je, Ukristo au Uislam ulikuwepo? Tukataeni propaganda za watu wanaotaka kukaa madarakani milele. Tatizo la nchi yetu siyo dinifulani au chama fulani cha upinzani.
Kama kweli tunaipenda nchi hii tuitendeeni haki kwa kukipa kura chama cha upinzani ili tuweze kufanya tathmini ya mfumo huu wa vyama vingi kama unafaa au haufai. Tukiendelea kukilea CCM tutakuja kujuta baadaye kwa sababu hata CCM hawaelewi kwa nini hali ya Watanzania ni taabani kwa sababu wao hawafikirii watakula nini bali wanawaza kuwekeza kwa ajili ya vitukuu wakati watanzania tulio wengi tunawaza tutakula nini leo. Tusichonganishwe kwa dini wala kabila; tuwwalaani watu wanaohubiri chuki kwenye majukwaa ya siasa na nyumba za ibada. Mbarikiwe watanzania wenzangu na Mungu awape kufahamu kinachotakiwa kufanyika 2015