Minziro awa Kocha wa Kwanza Kubwaga Manyanga

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
[h=1]BREAKING NEWS: BAO LA MAGURI, MINZIRO ATANGAZA RASMI KUJIUZULU KAZI YAKE JKT[/h]





Kocha wa JKT Ruvu, Fred Felix Minziro, amebwaga manyanga.


Minziro anaondoka, mechi yake ya mwisho ikiwa ni dhidi ya Stand United waliolala kwa bao 1-0 lililofungwa na straika nyota wa zamani wa Simba, Elius Maguri.



Minziro ameachia ngazi katika nafasi yake hiyo baada ya kuona mwenendo wa kikosi chake si mzuri katika Ligi Kuu Bara.




Kocha huyo ameamua kuachia ngazi saa chache baada ya JKT kupokea kipigo cha bao 1-0 dhid ya Stand United tena JKT wakiwa nyumbani, jana.


Katibu Mkuu wa JKT, Ramadhani Madoweka amesema kweli Minziro ameachia ngazi.


“Kweli Minziro ameachia ngazi, timu sasa iko chini ya Greyson Haule,” alisema.


JKT iko njiani kwenda mkoani Tabora ambako ina kibarua kingine kigumu dhidi ya Kagera Sugar ambayo inatumia Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.


Hadi Minziro anaondoka alikuwa ameongoza timu hiyo katika mechi nne, akianza ugenini dhidi ya Majimaji mjini Songea ambako walilala kwa bao 1-0.
 
Team za majeshi ni tatizo wabadili mfumo wao wa kiutawala vinginevyo hata akija kocha kutoka wapi itakuwa ni kazi bure na team za majeshi zitakuwa wasindikizaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…