Miongoni mwa mambo yanayomkera mwanamke!

Yaani nimecheka hadi basi! Hapa ninapoishi kuna mwanaume mmoja alikuwa anamtongoza binti mmoja ambaye yuko sekondari form 5 anamkataa. Mwanaume alikuwa akijisifia pesa, mali na kutoa ahadi kem kem lakini binti hakujali kabisa. Siku moja aliendelea na kumbembeleza huyo binti bila mafanikio yoyote na binti alitishia kumwambia mkewe(yaani huyo jamaa ameoa). Jamaa akajivuta pembeni kidogo, simu yake kubwa ya kichina akaiweka sikioni akajifanya anaongea na mtu. "halo, kama nilivyokwambia, uniletee milioni 3 tu, zingine 11 uniwekee benki" "halafu hivi ule mzigo mliokusanya unatosha SCANIA moja? Haya kesho pakia...." Wakati mwanaume huyo akiendelea na maongezi yake feki simu yake ikaita kwa sauti kubwa!Huyo binti alicheka, hakuwa na mbavu. Yeye yuko "hii simu yangu sijui vipi? mimi naongea na mtu yenyewe inaita! itakuwa na matatizo.
 

hahaah hii kali.
 
Sasa Rose mtu wangu kwa nini unapata shida na wavimba macho, hebu njoo huku kwangu nikupe raha. Naagiza Rolls Royce yangu ije kukuchukua sasa hivi.
Rolls royce ya nini mpelekee ndege ya kukodi kabisa ebo???
 
mhhhhhhhh vice verse is true uongo kwanza otherwise hupati kitu
 
Kuna mshikaji alikuwa na apointment na dada mmoja alipofika eneo la tukio jamaa akaanza kuonyesha funguo za gari demu akasepa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…