marco makungu
New Member
- Jun 12, 2013
- 1
- 0
Dhahiri nianze kwa kuipongeza Serikali kwa mipango yake ya kuwasisitiza watumishi wajiendeleze kitaaluma. Pamoja na jitihada hizi , Serikali imejisahau kutambua kuwa mabadiliko haya yanapaswa kuenda sambamba na baadhi ya mambo fulani fulani. Tukumbuke wahenga walisema 'mabadiliko si tishio bali ni fursa'. Nitoe mfano dhahiri juu ya kile ninachomaanisha. Sasa hivi kuna migogoro mikubwa tu na tena isiyofichika katika mashule mengi hapa nchini baaina ya wakuu wa vituo (shule/vyuo) na walimu/ wakufunzi.Elimu haihitaji siasa. Tusichanganye ujuzi na siasa. Hivi sasa wengi wa wakuu wa shule/vyuo wamekosa sifa zinazoendana na Taifa tunalolihitaji kwani wengi wao uwezo wa kitaaluma walio nao ni mdogo ukilinganishwa na hao wanaowaongoza. Itakuwaje mwalimu wa cheti amwaongoze mtu wa diploma au shahada au uzamili? Hapa hatujengi bali twacheza. Tizama sekondari sasa, mifumo mingi ya kibabe yenye kutotaka kupokea maarifa mapya ndiyo imekuwa tatizo kubwa kubwa kubwa. Unadhani mwalimu wa Diploma atawaongoza hawa wenye shahada moja au mbili.Wengi wao kinachofanyika sasa ni kejeli na kutokuwa tayari kujifunza. Ati mwalimu mwenye taaluma ndogo amseminishe mtu wa uzamili au uzamivu katika taasinia hiyo hiyo au mtu wa shahada ya awali aseminishe na mtu wa chini yake, kweli ???
Nampongeza Mh. John Cheyo kwa kuliona hili na kutoa dukuduku lake siku ya uhitimishaji wa bajeti ya elimu siku chache zilizopita. Ndugu zangu hili ni moja tu, yapo mengi sana ambayo siku tatu zijazo nitayasema.----MARCO
Nampongeza Mh. John Cheyo kwa kuliona hili na kutoa dukuduku lake siku ya uhitimishaji wa bajeti ya elimu siku chache zilizopita. Ndugu zangu hili ni moja tu, yapo mengi sana ambayo siku tatu zijazo nitayasema.----MARCO