Uchaguzi 2020 Miongoni mwa watu watakaokuwa na jambo lao tarehe 28 Oktoba

Uchaguzi 2020 Miongoni mwa watu watakaokuwa na jambo lao tarehe 28 Oktoba

Smt016

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2016
Posts
3,012
Reaction score
4,300
Wafuatao ni kundi la watu wenye shughuli yao maalumu siku ya tarehe 28.

1) Wanachama wa NSSF.

2) Waliotimuliwa kwa vyeti feki pamoja na familia na ndugu zao waliokuwa wanawategemea nao wakijiunga kwenye jambo lao.

3) waajiriwa wa serikalini wasiongezwa mishahara huku waliokuwa tegemezi wao nao wakijumuika katika shughuli maalumu ya hiyo tarehe 28.

4) Waliobomolewa nyumba Kimara.

5) Wamiliki wa sekta binafsi zilizokufa, pamoja na ndugu na familia waliokuwa wategemezi nao kujumuika kwenye jambo lao hiyo siku

6) Waajiliwa wa sekta binafsi waliokumbwa na kuachishwa kazi baada ya kubanwa kwa sekta binafsi huku familia na ndugu wakiwaunga mkono kwenye jambo lao tarehe 28

7) Wamiliki wa vyombo vya habari waliokutwa na kadhia ya kufungiwa kwa vyombo vya habari na huku ndugu tegemezi wakijumuika pia kwenye kazi maalumu tarehe 28

8) Wahitimu wa vyuo tokea 2015 mpaka sasa wanarandaranda mtaani hawana mbele wala nyuma kwa kukosa ajira watakuwa na jambo lao tarehe 28. Bila shaka ndugu zao wataunga mkono juhudi zao kwenye jambo lao.

9) Waliokumbwa na maafa mbalimbali wakitegemea kauli ya faraja lakini wakaambulia kauli ya kebehi, bila shaka watajumuika nawengine kwenye kilele cha jambo lao itakayofanyika tarehe 28.

10) Walipatwa na sekeseke kutoka kwa watu wasiyojulikana bila shaka walionusurika wataungana pamoja na ndugu zao kwenye sherehe ya jambo lao mnamo tarehe 28.

11) Waliopo vijijini waliopigika na maisha wasiona wala kuelewa thamani ya flyover na mandege watakuwa miongoni mwa watu watakaokuwa kwenye sherehe ya kilele cha shughuli maalumu ya tarehe 28.

12) Waliyopewa ahadi na kisha hiyo ahadi mpaka leo haijatekelezwa na wao watukuwa kwenye hiyo sherehe ya tarehe 28.
Mfano wa watu waliyoahidiwa jambo halafu halijatekelezwa ni watu wa wilaya ya Kilombero. Mwaka 2016 rahisi alienda na aliahidi kutengeneza barabara kwa kiwango cha lami kutoka Ruaha mpqka ifakara, lakini tokea 2016 mpaka sasa 2020 hakuna lami.
KHiiiiiiiiiiii bila kusahau.

13) Wafanyabiashara nao watakuwa kwenye kilele cha siku ya jambo lao tarehe 28.

Ongeza mengine unayohisi limesahaulika kwenye kilele cha sherehe la jambo letu itakayofanyika tarehe 28 October.
 
Walioporwa pesa zao bureau de change eti zimekwenda hakikiwa Hadi leo.
 
Kuirudisha ccm madarakani tena ni sawa na kumkopesha tena unaemdai
 
Uzuri ccm imekatiliwa Hadi vijijini sababu ya njaa. Walitusomesha namba Sasa ni zamu zao kuzisoma kura zetu. Trh 28 mbali kweli naona
 
Uzuri ccm imekatiliwa Hadi vijijini sababu ya njaa. Walitusomesha namba Sasa ni zamu zao kuzisoma kura zetu. Trh 28 mbali kweli naona
Meko kajitahidi sana kutengeneza chuki kwa kila aina ya makundi. Kila mtu analia kwa namna lake, miaka mitano watu tumesubiria kwa hamu sana kufikia siku ya mwisho wa mitano yake kuisha
 
Meko kajitahidi sana kutengeneza chuki kwa kila aina ya makundi. Kila mtu analia kwa namna lake, miaka mitano watu tumesubiria kwa hamu sana kufikia siku ya mwisho wa mitano yake kuisha
Zamu yake kuisoma namba awe mpole hakuna cha push up wa goti litakalo okoa jahazi.Anga likikutaa hata uwatumie wa gamboshi inakula kwako
 
Meko kajitahidi sana kutengeneza chuki kwa kila aina ya makundi. Kila mtu analia kwa namna lake, miaka mitano watu tumesubiria kwa hamu sana kufikia siku ya mwisho wa mitano yake kuisha
Amejimaliza kwa mafuta yake mwenyewe.
Laana na baraka ya mtu imo ndani ya ulimi wake
 
Back
Top Bottom