Mipaka ya kustaajabisha duniani

Mipaka ya kustaajabisha duniani

Kichuguu

Platinum Member
Joined
Oct 11, 2006
Posts
17,048
Reaction score
22,790
Duniani kuna mipaka ya ajabu sana ambayo wengine wetu huwanda hatuielewi. Mipaka hii ina historia zake, leo hii nitaweka ramani za baadhi ya mipaka hiyo ya ajabu, halafu siku nyingine nitajadili historia za mipaka hiyo. kama unaifahamu mipaka mingine ya ajabu, tufahamishe hapa.

Kuna mipaka miwili ya ajabu pale eneo la Jibrota (Gibraltar) kati ya Uhispania na Morocco. Kama umewahi kutembelea uhispania au Morocco unaweza kuwa umekutana na mipaka hiyo.

Wa kwanza uko ndani ya Uhispania ambapo kuna peninsular ndogo iliyomegwa kutoka jiji la La Línea de la Concepción na kupewa jina Gibraltar ambayo siyo mali ya Spain bali ni sehemu ya Uingereza. Ukiwa upande La Línea de la Concepción na ukataka kuingia Gibraltar lazima uonyeshe passport yako.

Mpaka wa pili uko ndani ya Morocco ambapo jiji la Ceuta kwenye kona ya Morocco limemegwa na kuwa mali ya uhispania. Ukitoka ndani ya Morocco kuingia jiji hilo lazima uonyeshe passport yako, na uwe na viza.
1644682386076.png


Sehemu nyingine yenye mpaka wa ajabu ni kati ya India na Bangladesh. Sehemu kubwa ya Bangladesh imezungukwa na india, na mpaka baina ya nchi hizo mbili umepindapinda sana. Kuna sehemu nyingine unapinda ili kumega sehemu ndani ya india na wakati mwingine unapinda ili kumega sehemu ndani ya Bangladesh.

Mpaka unaostaabisha sana ni ule unaozunguka eneo la Dahagram ambalo ni la Bangladesh lakini lote liko ndani ya India. Yaani mtu kutoka Dahagram kwenda makao makuu ya nchi huko Dhaka lazima avuke mipaka miwili, kutoka Dahagram kuingia India halafu tena avuke mpaka mwingine tena kutoka India kuingia Bangladesh.

Kwa bahati nzuri wameelewana kiasi kuwa India inawaruhusu watu wa Dahagram kuvuka mpaka kupitia Tin Bigha Corridor kuingia kwao Bangladesh bila kuhitaji passport wala viza.
1644683428843.png


Mipaka mingi ya Marekani ni mistali iliyonyooka tu. Mpaka kati ya Marekani na Canada kutokea bahari ya Pacific hadi maeneo ya maziwa makuu ni mstali uliyooka. Ukishafika kwenye maneo ya maziwa kati ya Jimbo la Minnesota kwa Marekani na Jimbo la Ontario kwa Kanada ndipo unaaza kupindapinda.

Njia yote kuanzia pale hadi kuingia bahari ya Atlantiki imepindapinda na sehemu nyingie zimepinda kiajabu ajabu ila ninataka kuleta sehemu kati ya Jimbo la Minnesota na lile la Ontario ambapo kuna peninsula mbili za Elm Point na NorthWest Angle zimemegwa kutoka Canada na kuwa sehemu za Marekani.

Mpaka sasa ile peninsula ya Elm point haikaliwi na watu bali ni msitu tu, ila kule NorthWest Angle kuna miji yenye wakazi kadhaa wanokaribia elfu kumi ambao wakitaka kwenda makao makuu ya jimbo lao huko St Paul-Minneapolis kwa gari, ni lazima wavike mpaka waingie Kanada kwanza ndipo wavuke mpaka tena kutoka Kanada kuingia Marekani tena.

Zamani kulikuwa hakuna haja ya kuwa na passport ila baada ya 9/11 ni lazima wawe na passport ingawa hawahitaji kuwa viza.

1644685490517.png


Mipaka ya nchi za Ulaya imetokana na himaya za kizamani sana zilizojengwa kwa kupigapigana vita, kwa hiyo mipaka yao imepinda pinda sana kutoka na jiographia ya eno la Ulaya.

Bara la ulaya ndilo linaloongoza duniani kwa kuwa na mipaka ya ajabu ajabu. Mmojawapo wa ajabu zaidi ni ule kati ya Uswisi na majirani zake. Ndani ya Uswisi kuna eno linaloitwa Büsingen am Hochrhein ambalo limemegwa kutoka Uswis na kuwa mali ya Ujerumani, eneo hili ni sehemu ya jimbo la Baden-Württemberg ndani ya Ujerumani.

Mkazi wa Büsingen am Hochrhein akitaka kwenda makao makuu ya jimbo lake kule Munich ni lazima avuke mpaka aingie Uswisi kwanza halafu avuke mpaka wa uswis tena ndipo afike Ujerumani
1644686309876.png


Mpaka mwingine ndani ya uswis wenye utata ni kati yake na Italia ambapo mji wa Campione d'Italia umemegwa ndania ya Uswisi na kuwa sehemu ya Jimbo la Como la Italia. Mkazi wa Campione d'Italia akitaka kwenye makao makuu ya jimbo lake Como, ni lazima avuke mipaka mwili kama ilivyo kwa yule wa Büsingen am Hochrhein.

1644687075869.png


Bara la Ulaya lina mipaka mingi sana ya ajabu likifuatiwa na Bara la Asia. Kama unfahamu mipaka mingine ya ajabu iweka hapa kwa ajili ya kuongezeana maarifa.
 
Suala la mipaka limeleta sintofahamu zaidi juu ya masuala ya umoja na mashirikiano kuliko kutuweka karibu walimwengu.

Barani Africa suala hili limekuwa na athari hasi sana na natamani siku moja hii mipaka iondolewe na tuishi bila hiyo.

Siku moja hii ndoto itatimia.
 
Untold story ni kwamba Nyerere aliweka dili mezani na aliyekua
rais wa Kenya miaka hiyo kuhusiani na uhalali wa Mt. Kilimanjaro. Nyerere aliweka ombi mezani kuwa Tanzania ipo tayari kuuachia mt Kilimanjaro ila ni mpaka pale Kenya itapokubali kuiachia Tanzania mji wa Mombasa.
Kenya walichomoa ilo dili ndio maana ikabaki kuwa hivyo mpaka leo.
Maana yake nikuwa kama dili la Nyerere lingekubaliwa. Pia mpaka wa Tanzania na Kenya ungeusisha kwenye uzi wako huu siku ya leo.
 
Hata Africa ipo. Mpaka wa Senegal na Gambia. Mkia wa Namibia. DRC na Angola. Ziwa Nyasa kuna visiwa vipo Msumbiji lakini ni vya Malawi.
Asante mkuu ngoja niitafute nitaileta. Ila mpaka mwingine wa ajabu ni kati ya Oman na Muungano wa falme za kiarabu (UAE). Huu bila hata maelezo unajionyesha ulivyo ya ajabu. Inawezekana kabisa mtu kutoka sehemu moja ya Oman alazimika kuvuka mpaka kuingia UAE, halafu akavuka mpaka tena kuingia Oman, na kuvuka tena kuingia UAE na kuvuka tena kuingia Oman na kuvuka tena akaingia UAE kabla hajavuka mpaka wa mwisho kuingia Oman tena!

1644696568873.png
 
Hata Africa ipo. Mpaka wa Senegal na Gambia. Mkia wa Namibia. DRC na Angola. Ziwa Nyasa kuna visiwa vipo Msumbiji lakini ni vya Malawi.
Sehemu kubwa ya nchi ya Gambia imezungukwa na Senegal, kwa hiyo raia waSenegal kutoka akitokea kusini kwenda kaskazini au kinyume chake lazima avuke mpaka aingine Gambia halafu avuke tena aingine Senegal, ila anaweza kuizunguka Gambia abakie ndani ya Senegal tu ingawa itakuwa njia ndefu sana, kwa mfano kutokea Diouloulou Senagal kwenda karang Senegal, itamchukua siku mbili kuizunguka Gambia na nusu siku kupitia ndani ya Gambia.
1644697313909.png


Ni vigumu kujua kama Jimbo la Cabinda lilimegwa kutoka DRC au kutoka Congo Brazaville, ila mtu kutoka Cabina kwenda makao makuu Luanda ni lazima avuke mpaka aingie DRC, ndipo avuke mpaka tena kuingia Angola
1644697540422.png
 
Kuna kipande cha mpaka wa Congo kimeingia upande wa Zambia kiasi kwamba unaweza kufikiri ni eneo la Zambia ila bendera ya Congo itakushangaza
 
Haya, ukishangaa ya Musa, basi utayaona ya kushangaza zaidi. Hivyo vinavyoonekana kama "visiwa" ni maeneo ndani ya Kyrgyzstan lakini yanayomilikiwa na nchi jirani za Uzbekistan na Tajikistan
1644699457441.png
 
Sehemu kubwa ya nchi ya Gamboa imezungukwa na Senegal, kwa hiyo raia waSenegal kutoka akitokea kusini kwenda kaskazini au kinyume chake lazima avuke mpaka aingine Gambia halafu avuke tena aingine Senegal, ila anaweza kuizunguka Gambia abakie ndani ya Senegal tu ingawa itakuwa njia ndefu sana, kwa mfano kutokea Diouloulou Senagal kwenda karang Senegal, itamchukua siku mbili kuizunguka Gambia na nusu siku kupitia ndani ya Gambia.
View attachment 2117764

Ni vigumu kujua kama Jimbo la Cabvinda lilimegwa kutoka DRC au kutoka Congo Brazaville, ila mtu kutoka KCabina kwenda makao makuu Luanda ni lazima avuke mpaka aingie DRC, ndipo avuke mpaka tena kuingia Angola
View attachment 2117765
Hapo Senegal na Gambia. Raia kutoka kaskazini au kusini hulazimika kuvuka mto na kivuko. Kuna kipindi serikali ya Gambia inapandisha nauli. Raia wanalalamika, senegal wanafunga mpaka hivyo raia wanalazimika kuzunguka hiyo njia ndefu. wanalalamika tena!! Senegal wanakaa na Gambia kukubaliana. Full drama hapo.
 
Hapo Senegal na Gambia. Raia kutoka kaskazini au kusini hulazimika kuvuka mto na kivuko. Kuna kipindi serikali ya Gambia inapandisha nauli. Raia wanalalamika, senegal wanafunga mpaka hivyo raia wanalazimika kuzunguka hiyo njia ndefu. wanalalamika tena!! Senegal wanakaa na Gambia kukubaliana. Full drama hapo.
Naipenda sana hiyo drama. Majirani wanaishi kwa kuheshimiana sana. Waliwahi kuungana na kuunda nchi moja ya Senegambia lakini walishindwa kuishi pamoja muungano huo ukavunjika kila nchi ikasepa kivyakevyake.
 
Hata Africa ipo. Mpaka wa Senegal na Gambia. Mkia wa Namibia. DRC na Angola. Ziwa Nyasa kuna visiwa vipo Msumbiji lakini ni vya Malawi.
Ule mkia wa Namibia, nimewahi kuuongelea hapa siku za nyuma kidogo. Ilikuwa ni lengo wa Wajerumani waliokuwa wanaitawala nchi yetu hii pamoja na Nambia na Kameruni kutaka kuwa na njia rahisi kati ya makoloni hayo bila kuwa wanazunguka Afrika ya Kusini. Walilazimisha kuchukua mkia ule mpaka kwenye mto wa Zambezi wakidhani ingewawia rahisi kwao kuifikia bahari ya hindi hadi Bagamoyo kwenye koloni lao kwa kupitia mto zambezi, ila hawakujua kuwa ulikuwa na Victoria Falls huko mbele. Vile vile waliwahi kuongea na Mfalme wa Ubeligiji wapewe sehemu fulani ya Kongo kusudi waunganishe Kamerun na Bongo yetu hii; leo hii Roger milla Angekuwa mtu wa Bongo.
 
Kuna kipande cha mpaka wa Congo kimeingia upande wa Zambia kiasi kwamba unaweza kufikiri ni eneo la Zambia ila bendera ya Congo itakushangaza
Hata sisi mpaka wetu kati ya Tanzania na Burundi pale wilayani Ngara kuna sehemu ya namna hiyo; watanzania kutoka sehemu moja ya ngara kwenye sehemu nyingine ya ngara wanalazimika kukatisha mpaka wa Burundi.
1644706822609.png
 
Naogopa sana migogoro ya mipaka Hadi nyumbani sitaki kufuga nyau
In fact mipaka mingi huleta ujirani mwema kwa vile watu wanaoishi mipakani huelewana pande zote, migogoro ya mipaka ni michache sana siku hizi duniani, labda Putin tu ndiye amebaki kuzozana na majirani zake kwa sababu ya mipaka pamoja na kuwa na ardhi kubwa kuliko nchi zote duniani

Angalia hao wenye nyumba katikati ya mpaka kati ya canada na Marekani; huwezi kuelewa iwapo wanabeba passport za Marekani au za Canada. Sijui kodi zao hulipa wapi.
1644707871402.png



Kuna hotelii hii ukiingia front desk unakuwa Switzerland, ukienda chumbani unalala Ufaransa.
1644708365841.png

1644708447932.png
 
Back
Top Bottom