The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Leo nimepita mjini kati Posta, Dar es Salaam, muda kidogo sijatembelea mjini kati, nikashangaa kuona mgahawa wa kienyeji (Mama Ntilie) umejengwa mbele ya jengo la mwalimu Nyerere Foundation ambapo kuna hoteli ya Johari Rotana, kwenye geti la kuingilia kwenye Hotel.
Johari Rotana ni 5 stars Hotel, wamekezaji wameweka pesa nyingi sana kuwekeza pale halafu, cha ajabu halmashauri ya jiji la Ilala imeruhusu mtu aweke genge la chakula mlangoni kwa hotel kubwa namna ile, hii inaingia akilini kweli?
Ukiachilia kuharibu mandhari ya mji kwa ujenzi wa hovyo hovyo, mgahawa ulioko mlangoni kwa Hotel kubwa namna ile ni kutowatendea haki wawekezaji wa ile hotel lakini pia kutokuitendea haki foundation ya mwalimu Nyerere.
Mamlaka ya mipango miji waliwezaje kutoa kibali cha ujenzi wa ule mgahawa mbele ya mlango wa hotel ya Johari Rotana?