RJ Enterprises
Member
- May 5, 2024
- 21
- 10
UTANGULIZI
Nitumie fursa hii kuwasalimu wapenda soka wote mlioko humu ndani jamiiforum pia wapenda maendeleo kwa ujumla.Mafanikio ya mpira wa miguu ni matamu sana lakini yanahitaji maandalizi ya hali ya juu, wakati Tanzania tunasherekea kufuzu kucheza Afcon mwaka 2023 wenzetu Senegal mwaka 2002 walishiriki hatua ya robo fainali kombe la dunia, Cameroon 1990 pia robo fainali kombe la dunia, Ghana walifanya mara mbili mfululizo 2006 na 2010 robo fainali, kwa Morocco kila mtu alikuwa shahidi mwaka 2022 alichokifanya ni maajabu kutinga hatua ya nusu fainali.
Hoja yangu ya msingi hapo ni kwamba hayo yote hayatokei kwa bahati mbaya bali ni watu waliweka project wakatrust kwenye process hatimaye ikawalipa, je' sisi kama taifa tumewekeza kwenye project gani ili baada ya miaka 15 au 20 iwe tunacheka.
NINI KIFANYIKE: MIKAKATI
- TUWEKEZE KWENYE ACADEMIA
Academia ni shule za watoto zinazofundusha mpira pekeyake, watoto hufundishwa na kulelewa kanuni za awali za mpira.
Mkakati uwekwe kila timu inayoshiriki ligi kuu iwe na academia baada ya hapo kwa kila msimu ni lazima ipandishe wachezaji watano kwenda kwenye timu ya vijana hapo tutaanza kutengeneza vijana wanaojua soka.
TUWEKEZE KWENYE LIGI YA VIJANA
Ligi ya vijana ipo lakini haijawekewa mkazo hata kidogo ni kama inachukuliwa powa lakini hapa ndo msingi mzuri wa mpira wa nchi, ingekuwa tuko makini tungewazalisha kina Kelvin John wengi sana na wangeleta tija kubwa sana kwa maendeleo ya mpira wetu.
Ligi ya vijana haina mnyororo sahihi wa kimajukumu kama inavyofanywa kwenye ligi kuu, hii ndo hatua ambayo inatakiwa ifanyike promotion kubwa Ili mascout wa nje waje wanunue vijana pia kuwe na mkakati wa kuwauza nje ya nchi Ili wakakue vizuri kisoka, kulikuwa na tetesi za ladack chasambi kutakiwa RB SALZBURG lkn akachagua kwenda Simba ingekuwa we ndo manager wake ungemshauri aende timu gani?, pia kulikuwa na tetesi mzize kihitajika Watford ya Uingereza tuone mwisho wa msimu itakuwaje lakini hizi ofa tusizichukulie powa hata kidogo tuzifuatilie hiyo ndo sehemu ya kumbrand mchezaji hata timu zingine.
- KUWE NA VYUO VYA MAFUNZO YA KISOKA
Kama Kuna vyuo vya kilimo, vyuo vya fundi na zinginezo, serikali pia inatakiwa kujenga vyuo vya mpira ambapo walengwa hapa ni vijana waliotoka sekondari na wachache kutoka mtaani kisha kupewa mafunzo ya kisoka katika level ya kiushindani zaidi, vijana hao hupandishwa ligi ya vijana na baadaye ligi ya wakubwa kisha wengine huuzwa nje ya nchi kwenda kukua zaidi kisoka.
- VIWANJA VIZURI VYA KISASA
Viwanja ndiyo mhimili mkubwa kwenye mpira wa miguu, viwanja ndiyo huvutia wawekezaji kuwekeza nchini, pia viwanja hufanya wachezaji wajifunze mpira kiufundi zaidi, viwanja vya kisasa vilivyokidhi vigezo vyote hadi taa za uwanjani hurahisisha majukumu ya kiratiba maana mechi zitachezwa hadi usiku mfano wenzetu wa ulaya wao wanacheza mpaka saa 5 usiku, viwanja vizuri pia vitachangia uwepo wa vifaa vya mazoezi vya kisasa ambavyo vitafanya wachezaji wajifunze ufundi wa mpira na kufanya mpira utembee uwanjani.
UZALISHAJI WA MAKOCHA WAZAWA
Msimu wa 2022-23 ligi yeti ilikuwa na makocha wazawa wapatao 21 tu na kati ya hao makocha wakuu wazawa kwenye timu za ligi kuu ni 5 pekee jambo ambalo siyo sahihi.
Timu za taifa zote zilizofanikiwa kisoka Afrika hazina makocha wa kigeni utaikuta alikuwa mchezaji wa zamani lakini sisi tumekuwa na desturi ya kuajiri makocha wa kigeni ambayo hawana uzalendo, uchungu na nchi pia hawatatekeleza falsafa ya nchi kwa usahihi.
Ujerumani mwaka 2002 ilikuwa na makocha 28,500 ikafungua vituo vya academy 366 nchi mzima na kuanzisha program waliyoiita "Extended Talent Promotion Program" na Wana mafanikio makubwa sana kisoka kuanzia Euro hadi kombe la dunia.
Kama nchi ukiwa na walimu wengi wazawa itapelekea wengi wao waende kifungua vituo vya academia na kuleta mafanikio makubwa sana kisoka.
- KUWE NA MKAKATI WA KUSAKA VIPAJI MTAANI
Clement mzize ambaye ni mchezaji wa yanga anafanya vizuri sana kwenye ligi yetu na anahusishwa na timu kubwa za nje ya nchi lakini miaka kadhaa nyuma alikuwa dereva bodaboda pale Iringa, je' tumejiuliza kuna clement mzize wangapi mtaani nchi mzima.
Kuwe na mfumo wa kasaka vipaji mtaani hapa walengwa ni wale vijana ambao hawakuendelea na elimu lakini wapo mtaani na wanajihusisha na michezo mitaani.Timu ya taifa ya misri karibia asilimia 98 ya wachezaji wanatoka timu ya ndani hapo inaonesha jinsi gani walivyothaminisha vipaji vya ndani.
Mtaani kuna vipaji sana nduguzangu lakini je' kuna mifumo gani ya kuwawezesha hawa vijana waingie kwenye soka la ushindani ni wito kwa wadau na serikali kuweka mifumo rasmi ya kimkakati Ili hawa vijana ambao hawaonekani waanze kuonekana na walete tija kwenye maendeleo ya mpira wetu kitaifa.
- MCHANGO WA SIMBA, YANGA NA AZAM KIMATAIFA
Hizi timu zinatakiwa kutumia fursa ya kucheza mashindano ya kimataifa kuuza wachezaji wa ndani, imekuwa desturi wachezaji wa nje ndo wananufaika sana na hii fursa tumeshashuhudia kwa miquisone, chama, mayele na wengineo lakini wachezaji wetu wamekuwa wakifika kwenye hizi timu wanakuwa na tabia ya kuridhika hawataki changamoto mpya jambo ambalo linawafanya wasiendelee kisoka na soka letu kuwa chini daima.
HITIMISHO
Mafanikio ya mpira wa miguu kitaifa yanahitaji mwitikio wa kila mtu, wadau, taasisi, sekta binafsi na serikali kwa ujumla.
Mpira wa miguu ukiufanyia uwekezaji huo uwekezaji utalipa zaidi kwa sababu mpira wa miguu una mapato mengi sana pia tutatangaza utalii wa nchi yetu.
Kufika kombe la dunia sio kazi rahisi lakini pia ni rahisi kama kila mmoja wetu atakuwa tayari kwa hili kwani kuna mtu aliyetegemea kuwa Argentina angekuwa bingwa wa kombe la dunia 2022 hasa baada ya kufungwa na Saudi Arabia 2-1 lakini mwisho wa siku wakasuka mipango upya na kuongeza hamasa hatimae wakafanikiwa au kuna mtu aliyetegemea Morocco angefika hatua ya nusu fainali 2022 lakini yote hayo huchagizwa na mipango yako ipoje hatuwezi tukaota kwamba tutafika huko wakati jitihada za kuchonga Barabara hazionekani.
Tuweke mradi kisha tuwekeze kwenye mradi, na tuamini kwenye mradi huo hatimaye tutafanikiwa kucheza kombe la dunia 2042.
MWISHO.

Upvote
1