Njama zimesukwa kuhakikisha kwamba mgombea wa Urais mwenye nguvu zaidi Dr Wilbroad Slaa kutokea Chadema hapati nafasi ya kugombea Urais.
Wapanga mkakati huo wamepenyeza kifungu kwenye Rasimu ya Katiba mpya kinachosema mgombea Urais hapaswi kuwa ameshawahi kuwa mbunge kwa vipindi vitatu mfululizo.
Kifungu hicho ambacho wachunguzi wa mambo wanasema ni kifungu Kandamizi na cha kipuuzi kinawalenga pia wagombea Urais wenye nguvu kutoka CCM kama Edward Lowassa,Bernard Membe,Samwel Sitta na John Magufuli.
Endapo kipengele hicho kitapita kama kilivyo inaonekana wanasiasa watakaokuwa na sifa ya kugombea Urais ni pamoja na January Makamba,Emmanuel Nchimbi,Dr Asha Rose Migiro na wengineo wasiokuwa na majina makubwa.
Wachambuzi wa mambo ya kisiasa wanasema walengwa wakuu wa kipengele hicho ni Dr Wilbroad Slaa na Edward Lowassa wanasiasa wenye nguvu kubwa ndani ya vyama vyao.
Hata hivyo swali la kujiuliza ni Je Tume ya Katiba ya Joseph Warioba ilikubali kusigina haki za watu kwa kununuliwa na wanasiasa uchwara?
Kwa mujibu wa gazeti la Mtanzania baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM wamekuwa wakipiga kelele kubwa kuhusu muundo wa serikali tatu ili kufunika kipengele hiki cha kijinga kisijadiliwe na hatimaye kipitishwe ndipo watu washtuke ambapo watakuwa wameshachelewa.
Source:Mtanzania Jumapili.