SoC04 Mipango ya mabadiliko kiuchumi Tanzania ndani ya miaka mitano hadi ishirini na tano

SoC04 Mipango ya mabadiliko kiuchumi Tanzania ndani ya miaka mitano hadi ishirini na tano

Tanzania Tuitakayo competition threads

SAMWEL LOI WILLIAM

New Member
Joined
Jun 9, 2024
Posts
3
Reaction score
5
MIPANGO MINNE YA MAENDELEO YA KIUCHUMI TANZANIA.

Je! Uchumi wa Tanzania wa sasa unafanana na ule wa Tanzania ya mwaka 2015? Jibu ni HAPANA! Hivi sasa ni mwaka 2024, kwenye kalenda ya serikali tumebakiza mwaka mmoja tu! Tanzania tuingie katika uchaguzi mkuu, yaani uchaguzi wa raisi wa awamu ya saba utaofanyika mwaka 2025. kwa mujibu wa Benki ya dunia mwaka 2021, Tanzania ilikua na ukuaji wa kimaendeleo ya kiuchumi asilimia 4.9%.

Mnamo mwaka 2023 Tanzania iliongeza jitihada katika ukuaji wa kimaendeleo ya kiuchumi hadi asilimia 5.2%. Hivi sasa Tanzania inatarajia kufika asilimia 6.3% katika suala hilo hilo la ukuaji wa kimaendeleo ya kiuchumi ”Hii ilisemwa katika mkutano wa wakurugenzi watendaji wa Baraza la biashara la Afrika Mashariki (EABC) 20/3/2024”.

Tazamia hali ya mabadiliko ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Nchi ya Tanzania ni nchi yenye bahati sana katika suala zima la kisiasa kwani imeweza kudumisha Amani ya nchi katika shughuli zote za kisiasa hasa uchaguzi mkuu. Hii ni wazi kuwa Hali ya ukuaji wa kimaendeleo ya kiuchumi Tanzania hautoathriwa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2025. Baada ya uchaguzi mkuu Tanzania sasa itakua katika hali nzuri ya mabadiliko ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi.

Je! Suala la mipango ya mabadiliko ya ukuaji wa kimaendeleo ya kiuchumi Tanzania baada ya miaka mitano, kumi, na kuendelea ni jukumu la nani? Hili ni fumbo ambalo wenye jibu la fumbo hilo ni umma ya Tanzania na watumishi wake wa umma.

Kama umma ya Tanzania, Tunaweza kufumbua fumbo hilo kwa kutoa maoni ya msingi yatakayoweza kuwapa dira nzuri watumishi wetu wa umma katika utekelezaji mzuri utakaoweza kuleta ukuaji wa kimaendeleo ya kiuchumi wa Tanzania tuitakayo.

Baadhi ya mipango itakayoweza kufumbua fumbo hili ni pamoja na kuboresha muonekano wa hifadhi za Taifa, mapinduzi ya sekta ya mpira wa miguu nchini kufuatiwa na tukio la AFCON 2027, kuongeza uwekezaji katika sekta ya mbao, serikali kuhakikisha miradi yote mikubwa ya kimaendeleo nchini imekamilika ndipo kuanzisha miradi mingine mikubwa ya kimaendeleo nchini na ujenzi wa viwanda vya utengenezaji wa bidhaa za chuma nchini.Mipango hii imefafanuliwa kama ifuatavyo;

Kuboresha muonekano wa Hifadhi za Taifa. Tanzania ni nchi yenye kusifika sana Afrika kutokana na uasili wake mzuri wa kipekee mfano, Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro yenye mvuto wa kipekee duniani, Serengeti pamoja na Kilimanjaro ambao ndio mlima mrefu Zaidi Afrika. Hifadhi hizi za Taifa zinapaswa kuboreshwa muonekano kwa kuzingatia asili ya eneo husika, hii ni pamoja na uboreshaji wa mapokezi, utawala na uongozi katika sekta ya utalii.
Hii nisambamba na kusema “kipaji chako kiboreshe kwani kina faida”. Tanzania ikiboresha zaidi na zaidi sekta ya utalii itajenga picha nzuri na ya kuvutia duniani kuwa Tanzania ni nchi ya kitalii kwani hifadhi zake za taifa zinavutia sana. Hivyo basi sekta ya utalii itaongeza mvuto kwa wageni kutoka pande mbalimbali za ulimwengu kufika Tanzania na kuleta mabadiliko ya kiuchumi nchini ndani ya miaka mitano hadi ishirini na tano.

Ujenzi wa viwanda vya utengenezaji wa bidhaa za chuma nchini. Huu ni mradi wa maendeleo wa uchumi wa viwanda nchini. Mradi huu wa viwanda vya utengezaji wa bidhaa za chuma nchini utaongeza pato la taifa kwa asilimia nyingi kwani bidhaa za chuma ni bidhaa zenye uhitaji mkubwa katika soko la ndani na nje ya nchi.
Vilevile, bidhaa za chuma zinauhitaji mkubwa katika sekta mbali mbali kama vile sekta ya sayansi na teknolojia nchini, sekta ya viwanda vingine nchin i{katika utengenezaji wa viwanda nakadhalika…}, sekta ya miundombinu ya nchi kama vile barabara an reli.Kama umma tunaomba serikali ushirikiano katika kujadili mradi huu utakaoleta mabadiliko ya maendeleo ya kiuchumi nchini ndani ya miaka mitano hadi miaka ishirini na tano.

Mapinduzi ya mchezo wa mpira wa miguu. Timu ya taifa ya Tanzania {Taifa Stars} ni timu yenye wachezaji wenye vigezo vyote vya kucheza ndani na nje ya nchi mfano Mbwana Samatta mchezaji wa timu ya taifa anaechezea timu ya nje ya nchi PAOK. Mapinduzi yanayo jadiliwa katika hoja hii ni pamoja na kuweza kuandaa mechi za kirafiki na mataifa ya nje ya Afrika kama vile China, Korea na zingine nyingi.
Mapinduzi haya yanaweza kutekelezwa baada ya mechi za kombe la shirikisho la mataifa ya Afrika zitakazochezwa mwaka 2027 katika nchi za Afrika mashariki yaani Tanzania, Kenya na Uganda. Hii ni kufuatiwa na ujenzi wa uwanja wa mpira wa Mama Samia Suluhu Hassan raisi wa nchi ya Tanzania, katika mji wa Arusha ambapo ni mingoni mwa uwanja utakao husika katika michuano ya kombe la shirikisho la mataifa ya Afrika{AFCON}.
Uwanja huu unasifa za kimataifa utakaoweza kuvutia mataifa mengine kushiriki mechi ya timu ya taifa ya Tanzania. Hivyo basi mapinduzi haya yakifanikiwa yatawezesha timu ya taifa kuweza kushiriki mashirikisho makubwa kama vile kombe la dunia, pengine kama mashirikishi ya AFCON yalivyopangwa Tanzania vile vile, mashirikisho ya kombe la dunia huenda yakapangwa Tanzania tena, itakua bahati ya mabadiliko ya kiuchumi ilioje? Mafanikio ya mapinduzi haya yataleta mabadiliko makubwa katika uchumi wa nchi ndani ya miaka kumi na tano hadi ishirini na tano

Kuongeza uwekezaji katika sekta ya viwanda vya mbao nchini. Tanzania ni nchi yenye eneo lenye ukubwa wa kilomita 945,087 za mraba, nchi ina eneo kubwa lililobaki wazi kama akiba hivyo basi serikali ikiongeza uwekezaji katika sekta ya mbao nchi itakua imetumia vizuri rasilimali ya ardhi nchini.Vilevile sekta ya mbao ni sekta yenye faida sana katika soko la ndani na nje ya nchi kwani kwa sasa inachanigia asilimia 4.6% Katika pato la taifa. Uwekezaji katika sekta ya mbao unatakiwa ujihusishe na kupanda misitu ya miti ya mbao katika mikoa yenye kuweza kustahimili shamba la misitu kama vile Njombe na Iringa, Mafanikio ya uwekezaji katika sekta ya mbao utaleta mabadiliko katika maendeleo ya ukuaji wa kiuchumi nchini ndani ya miaka mitano hadi ishirini na tano.

Hivyo basi baada ya kujadili mipango ya mabadiliko ya ukuaji wa maendeleo ya kiuchumi nchini, kama umma tunaomba ujumbe huu uufikie serikali an tunaiomba serikali ushirikiano katika kuzijadili mada hizi na kuzitafutia majibu pia serikali kuhakikisha miradi yote mikubwa ya maendeleo nchini imekamilika ndipo kuanzisha miradi minginemikubwa ya kimaendeleo nchini. Mipango hii italeta mabadiliko makubwa sana ya maendeleo ya ukuaji wa kiuchumi nchini ndani ma miaka mitano hadi ishirini na tano.
 
Upvote 3
Back
Top Bottom