Mipango ya majiji Tanzania

Mipango ya majiji Tanzania

tehama

Member
Joined
Nov 21, 2018
Posts
15
Reaction score
9
Habari wakuu,

Mimi ni Mtanzania kindaki ndaki. Nimepata nafasi ya kutembelea maeneo kadhaa nje na ndani ya nchi. Hakuna jambo linanikera kama namna tunaishia kama mifugo katika nchi yetu. Ni kama tuko katika banda la wanyama. Hakuna mpangilio wala hakuna kiongozi yeyote anaezungumzia hilo

Ukiangalia tafiti za mashirika mbalimbali, Dar ni jiji litakalokua na watu wengi sana ifikapo 2030

Utafiti wa the citizen

Utafiti wa world bank

Nimeona nifungue hili jukwaa tuweze kujadili kwa undani, nini hasa kifanyike na pia ni viongozi gani tuweza kuwapata tujiunge na kufanya lobbying katika wizara husika

Tunafahamu nchi yetu ina shida ya ukwasi, hivyo mawazo yetu yawe ya kutumia resources chache na kuleta tofauti kubwa. Mpango huu utaweza kufanya makadirio ya maji na umeme (Wote tunajua shida ya junk electricity <umeme mdogo> tuliyonayo mtaani na pia shida ya maji)

Jiji la Dar kwa miaka 50 - 80 ijayo

Phase I (Upande wa juu wa Morogoro road. Kuanzia Ubungo - Saadani National Park)

Ushauri wangu utaanzia barabara ya mbezi - goba - Wazo hadi Saadani.

1. Bagamoyo - Kibaha - Chalince iwe ni part ya Dar

2. Katikati ya Mogorogo road na Bagamoyo road, serikali itenge Central Park (Amani Central Park) itakayo fika hadi mpakani mwa Saadani National Park. Amani park iwe na upana wa km 2 - 3

3. Kutengenezwa njia kuu 8 upande wa juu na wa chini wa amani central park

4. Upande wa juu na wa chini wa Amani, yaachwe maeneo kwa ajili ya biashara na makazi (skyscrapers)

5. Kila baada ya kiiomita kadhaa, kuwe na barabara za mitaa kugawanya maeneo ya makazi, biashara, burudani, masoko, shule, golf courses + michezo kwa ujumla, nk. Hii itakua ni mistatili. Kila mstatili utapatiwa makadirio ya maji na Umeme na kua maintained kwa urahisi

6. Barabara hizo kuu ziwe sio chini ya njia 4, huku za mitaa ziwe na njia 2 kila upande, hii bila kusahau lane za watembea kwa miguu, treni katikati na at least 2 lanes kila update for future use

7. Katikati ya Amani central Park, kuweke uwanja wa Matamasha ya jijini DSM

8. Mwisho wa Amani Park, itengenezwe Tanzanite Towers itakayo angalia Amani central Park & Saadani national Park

9. Utengenezwe uzio wa kuingia Saaadani na kisha maeneo hayo yawe ni prime kwa ajili ya the super rich

10. Maeneo ya umwagiliaji ruvu yabaki kama yalivyo

Nini tufanye kwa wenye viwanja + nyumba zao

1. Wenye maeneo sasa ivi, waandikishwe na watapewa viwanja baada ya eneo lote kupimwa

2. Walio na nyumba, baada ya zoezi la kupima kukamilika, watapewa nyumba standards katika maeneo yaliyopimwa

Makadirio ya Plan hii inaweza kuchukua miaka 5 - 8 hadi kukamilika

Faida

1. Kuongeza wigo wa ukusanyaji kodi.
a. Kodi ya ardhi
b. Kodi ya mauzo/manunua inapofanyika
c. Mapato kupitia Amani Park

2. Kuongeza soko la mali isiyohamishika (real estate)

3. Miji ikipangwa vizuri + mifumo sahihi, wawekezaji watakuja zaidi na uchumi kukua

4. Kukuza utalii

Karibuni tujadili wakuu
 
Kwa hiyo Tanzania Ni Dar peke yake?
Kila siku kuboresha Dar, Dar, Dar. Majiji mengine ndani ya TZ hayana uhalali WA kuboreshwa?
Mkuu title inasema majiji Tanzania na sio Dar pekee. Dar ni mwanzo tu, lazima tuanze na blue print.

Dar ndo jiji la kibiashara kwa sasa, sio rahisi kulipotezea
 
Yaani hata mimi nashangaa sana! Kuna miji mingi mizuri inahitaji maboresho kama Mwanza,Arusha na Mbeya!
Mindset ya kipuuzi sana Dar hii imejengwa sana na serkali lakini hamna la maana mpaka leo!
 
Mkuu, ungezungumza hoja yako kuhusu kupangilia kwa hiyo miji.

Mimi sio mwenyeji wa Mwanza/Arusha/Mbeya. Nimezunguamzia sehemu ninapoishi.

Wakati mwingine badili mtizamo wako wakati unajibu hoja, sio kulalamika kila wakati
 
Habari wakuu,

Mimi ni Mtanzania kindaki ndaki. Nimepata nafasi ya kutembelea maeneo kadhaa nje na ndani ya nchi. Hakuna jambo linanikera kama namna tunaishia kama mifugo katika nchi yetu. Ni kama tuko katika banda la wanyama. Hakuna mpangilio wala hakuna kiongozi yeyote anaezungumzia hilo

Ukiangalia tafiti za mashirika mbalimbali, Dar ni jiji litakalokua na watu wengi sana ifikapo 2030

Utafiti wa the citizen

Utafiti wa world bank

Nimeona nifungue hili jukwaa tuweze kujadili kwa undani, nini hasa kifanyike na pia ni viongozi gani tuweza kuwapata tujiunge na kufanya lobbying katika wizara husika

Tunafahamu nchi yetu ina shida ya ukwasi, hivyo mawazo yetu yawe ya kutumia resources chache na kuleta tofauti kubwa. Mpango huu utaweza kufanya makadirio ya maji na umeme (Wote tunajua shida ya junk electricity <umeme mdogo> tuliyonayo mtaani na pia shida ya maji)

Jiji la Dar kwa miaka 50 - 80 ijayo

Phase I (Upande wa juu wa Morogoro road. Kuanzia Ubungo - Saadani National Park)

Ushauri wangu utaanzia barabara ya mbezi - goba - Wazo hadi Saadani.

1. Bagamoyo - Kibaha - Chalince iwe ni part ya Dar

2. Katikati ya Mogorogo road na Bagamoyo road, serikali itenge Central Park (Amani Central Park) itakayo fika hadi mpakani mwa Saadani National Park. Amani park iwe na upana wa km 2 - 3

3. Kutengenezwa njia kuu 8 upande wa juu na wa chini wa amani central park

4. Upande wa juu na wa chini wa Amani, yaachwe maeneo kwa ajili ya biashara na makazi (skyscrapers)

5. Kila baada ya kiiomita kadhaa, kuwe na barabara za mitaa kugawanya maeneo ya makazi, biashara, buruadni, masoko, shule nk. Hii itakua ni mistatili. Kila mstatili utapatiwa makadirio ya maji na Umeme na kua maintained kwa urahisi

6. Barabara hizo kuu ziwe sio chini ya njia 4, huku za mitaa ziwe na njia 2 kila upande, hii bila kusahau lane za watembea kwa miguu, treni katikati na at least 2 lanes kila update for future use

7. Katikati ya Amani central Park, kuweke uwanja wa Matamasha ya jijini DSM

8. Mwisho wa Amani Park, itengenezwe Tanzanite Towers itakayo angalia Amani central Park & Saadani national Park

9. Utengenezwe uzio wa kuingia Saaadani na kisha maeneo hayo yawe ni prime kwa ajili ya the super rich

10. Maeneo ya umwagiliaji ruvu yabaki kama yalivyo

Nini tufanye kwa wenye viwanja + nyumba zao

1. Wenye maeneo sasa ivi, waandikishwe na watapewa viwanja baada ya eneo lote kupimwa

2. Walio na nyumba, baada ya zoezi la kupima kukamilika, watapewa nyumba standards katika maeneo yaliyopimwa

Makadirio ya Plan hii inaweza kuchukua miaka 5 - 8 hadi kukamilika

Karibuni tujadili wakuu
Mimi nakubali mji wa shinyanga kwa mpangilo ile manispaa haina slams navichochoro kama dar na.miji.mingine barabara za mitaa zimenyooka kama ulaya
 
Sawa mkuu, viongozi wangeandaa mpango kujifunza kutoka Shinyanga.

Je kuna maeneo ya wazi ya kupumzika ? Viwanja vya michezo pia ?
 
Mkuu, ungezungumza hoja yako kuhusu kupangilia kwa hiyo miji.

Mimi sio mwenyeji wa Mwanza/Arusha/Mbeya. Nimezunguamzia sehemu ninapoishi.

Wakati mwingine badili mtizamo wako wakati unajibu hoja, sio kulalamika kila wakati
Title yako inaongelea majiji Tanzania hapa tena unasema Dar!
Dar hii ilishafanyiwa kila kitu na serkali ila bado ya hovyo tu kwa mimi wasijikite kuboresha miji mingine ili watu wahamie huko
 
Vyovyote vile, ila Huo ni upendeleo. Kila mara tunaambiwa Dar imepata mkopo wa sijui Trillion kadhaa kwa ajili ya kuliboresha jiji la Dar. Sijawahi sikiwa Mbeya imepata mkopo wa mabilioni ngapi sijui kwa ajili ya kuliboresha jiji la Mbeya. Inawezekana ChoiceVariable anazo takwimu za mikopo inayoihusu jiji la Mbeya.
Mkuu title inasema majiji Tanzania na sio Dar pekee. Dar ni mwanzo tu, lazima tuanze na blue print.

Dar ndo jiji la kibiashara kwa sasa, sio rahisi kulipotezea
 
Jamaa Ni mzushi Sana. Title na content ni mbingu na ardhi.
Title yako inaongelea majiji Tanzania hapa tena unasema Dar!
Dar imegeuka kama Mtoto mpendwa asiyetosheka kuhudumiwa. Majiji mengine kama Tanga na Mbeya yako hoi bin taaban kana kwamba Serikali haiusiki katika kuyafanyia maboresho.
Dar hii ilishafanyiwa kila kitu na serkali ila bado ya hovyo tu kwa mimi wasijikite kuboresha miji mingine ili watu wahamie huko
 
Jamaa Ni mzushi Sana. Title na content ni mbingu na ardhi.

Dar imegeuka kama Mtoto mpendwa asiyetosheka kuhudumiwa. Majiji mengine kama Tanga na Mbeya yako hoi bin taaban kana kwamba Serikali haiusiki katika kuyafanyia maboresho.
Nchi ilojaa wajinga hii!
Unakutana na wakazi wa Dar walio kwenye umasikini wa kutosha wanawacheka wa mikoani ambao pengine wana maisha bora kuliko wao!
Mentality ya viongozi kufanya kila uwekezaji Dar es Salaam ndo inawasumbua sana mpaka sasa!
 
Sawa mkuu, viongozi wangeandaa mpango kujifunza kutoka Shinyanga.

Je kuna maeneo ya wazi ya kupumzika ? Viwanja vya michezo pia ?
Mimi naongelea upande wa.mpango mji yaani kule barabra huwa zinachongwa na manispaa hata kabla ya watu.kuanza makazi. Jaribu.kuzoom kwa google map afu ulinganishe na mikoa mingine..

Kinachokera miji mikubwa kama Dar ni kwamba watu wanajenga kiholela bila utaratibu na kuzungusha maukuta matokeo.yake hata njia.ya kwenda.kwako huenda ikakosekana ...

Mfano mzuri ni chanika ni mji wa juzi ulifaa upangwe vizuri lakini matokeo yake tumerudi kulekule sijui.wataalamu wetu huwa wanawaza nini.

Tanzania Majiji makubwa kama huna hela ya kutosha.utaishi maisha.ya taabu sana vichochoroni maana maeneo mazuri yote huchukuliwa na wenye pesa zao
 
Dsm ndio Tanzania ilipo, mji kila kukicha watu wanaongezeka. Sio kwamba miji mingine haina hadhi ya kufanyiwa maboresho, bali first priority ni dsm. Emu niambie mji wa mbeya na tanga unauwekea flyover ili iweje sasa na wakat magari ni ya kuhesabika mkoa mzima.
Hao watu unaodai wanakuja Dar kwa sababu hakuna maboresho ya huduma!
Wewe unadhani miji kama Mwanza na Arusha ikiboreshwa mtu anaweza kutamani kuja Dar kufanya nini?
 
Dsm ndio Tanzania ilipo, mji kila kukicha watu wanaongezeka. Sio kwamba miji mingine haina hadhi ya kufanyiwa maboresho, bali first priority ni dsm. Emu niambie mji wa mbeya na tanga unauwekea flyover ili iweje sasa na wakat magari ni ya kuhesabika mkoa mzima.
Dar ndo nchi ilipo kwa mihemko tu! Ila ukiwaza kwa usahihi Dar haina cha kujitegemea yaani Dar bila mikoa mingine hakuna kitu hapo!
 
Hao watu unaodai wanakuja Dar kwa sababu hakuna maboresho ya huduma!
Wewe unadhani miji kama Mwanza na Arusha ikiboreshwa mtu anaweza kutamani kuja Dar kufanya nini
Uko sahihi, shida ya viongozi wetu hawana maono ya mbeleni, mji wa Dar miaka kumi ijayo utakuwa kama Lagos yani kutakuwa na nyomi la watu kama wasipoboresha maendeleo ya miji mingine. Tatzo ni kupata viongozi wenye maono na kujua kwamba watu wengi wanakimbilia dar wakiamini hii miji mingine haina fursa.
 
Bwana haya maisha ukiangalio unaona kabisa Viongozi maono zero!

Ukiangalia watu wanavyohangaika kupata huduma Kariakoo au Karume na wanahangaika kurudi makwao bila sababu za msingi!

Mfano Dar es Salaam saizi imejaa lakini hakuna mkakati wa kutenga masoko kulingana na huduma!

Mfano Kariakoo ingekuwa soko la vifaa vya kielectric kama simu,radio,tv nk

Tandika ingekuwa soko la nguo kama mapazia,nguo za akina mama nk!

Mbezi ingekuwa soko la magari na spare mbalimbali za pikipiki,bajaji na magari!

Makumbusho lingekuwa soko la viatu na kila aina ya kiatu utakikuta pale!

Hapo moja kwa moja Kariakoo ingepumua na hakuna mtu angehangaika kuja kariakoo!

Mji ungekua na kupendeza pande zote!

Hata China wana miji yameitenga kwa ajili ya Magari,Nguo na Vifaa vya kielectric na mtu akifika tu Airport atapewa taarifa ukitaka bidhaa fulani utaenda mji fulani na utapanda train hapa kwa masaa kadhaa!

Ndo maana China ina miji miji yenye hadhi karibu sana na inaunganishwa na usafiri mzuri wa anga,barabara,reli na maji.

Mji kama Mbeya ungekuwa ni center ya bidhaa kwa miji yote midogo ya kusini na nyanda za juu pamoja na miji kama Ndola,Kitwe,Kalulushi,Chililabombwe Lusaka kwa nchi ya Zambia kutapata bidhaa hapo kutokana na masoko makubwa yenye kila aina ya bidhaa mtu anayoweza kuipata Dar es Salaam!
 
Dar ndo nchi ilipo kwa mihemko tu! Ila ukiwaza kwa usahihi Dar haina cha kujitegemea yaani Dar bila mikoa mingine hakuna kitu hapo!
Mkuu, jikite kuchangia mada kwamba mkoa uliopo uboreshwe kwa namna gani. Sio kulalamika tu
 
Back
Top Bottom