Wana JF,
Nimekuwa na shauku ya kufahamu mipango iliyopo ya matumizi ya ardhi hususan kwa jiji la Dar es Salaam. Hii ni hasa kwa maeneo ambayo hayajapimwa bado (unsurveyed) kama vile baadhi ya maeneo ya Mbezi Msakuzi, Mbezi Makabe, Goba, Madale, Mbagala Kuu, Msongola, Kivule, Kibamba - Kwembe, etc.
Maeneo hayo ndiko unakoweza kununua viwanja ukajenga nyumba ya kuishi bila kuwa na kibali maalum cha mipango miji. Ndiko ambako kuna wakazi wengi na wanaendelea kujazana kila siku. Baada ya wakazi hao kuweka makazi yao ya kudumu, huduma za jamii huwafuata na nyingi ya huduma hizi huletwa na serikali.
Niliwahi kusoma mahali kuwa ardhi ni mali ya serikali, hivyo wakati wowote serikali inapoihitaji hiyo ardhi sehemu fulani inaichukua kwa kuwafidia waliopo (sio wakati wote). Pia niliwahi kusikia kuwa miji yote ina kitu kinaitwa "MASTER PLAN", ambayo inaonyesha kila eneo na matumizi yake kama vile; maeneo ya makazi, viwanda, huduma za jamii, hifadhi, maeneo ya hatari, nk. Hata hivyo natambua kuwa serikali yetu inayo maafisa pamoja na kada zingine; maafisa ardhi wapo kila halmashauri na manispaa. Niliwahi kuelezwa kuwa kando kando ya barabara ya Mandela (DSM) kuanzia Ubungo hadi Buguruni lilitengwa kwa ajili ya viwanda na sio makazi kama ilivyo sasa.
Kutokana na hayo hapo juu, nina maswali yafuatayo kwa atakayehusika;
1. Master Plan iliyopo haitekelezwi?
2. MAster Plan iliyopo au iliyowahi kuwepo ni siri kwamba wananchi hawapaswi kuifahamu?
3. Wanapoanza ujenzi watu katika eneo fulani ambalo lina mpango mwingine, wahusika wanakuwa wapi hadi ubomoaji unatokea?
4. Kwanini ofisi zetu ndogondogo za mtaa zisishirikishwe katika kila mpango uliopo katika eneo lao?
Wasalaam
eneo kuanzia