Mipango ya matumizi ya ardhi jijini dar es salaam

KASRI

Member
Joined
May 2, 2009
Posts
93
Reaction score
22
Wana JF,
Nimekuwa na shauku ya kufahamu mipango iliyopo ya matumizi ya ardhi hususan kwa jiji la Dar es Salaam. Hii ni hasa kwa maeneo ambayo hayajapimwa bado (unsurveyed) kama vile baadhi ya maeneo ya Mbezi Msakuzi, Mbezi Makabe, Goba, Madale, Mbagala Kuu, Msongola, Kivule, Kibamba - Kwembe, etc.

Maeneo hayo ndiko unakoweza kununua viwanja ukajenga nyumba ya kuishi bila kuwa na kibali maalum cha mipango miji. Ndiko ambako kuna wakazi wengi na wanaendelea kujazana kila siku. Baada ya wakazi hao kuweka makazi yao ya kudumu, huduma za jamii huwafuata na nyingi ya huduma hizi huletwa na serikali.

Niliwahi kusoma mahali kuwa ardhi ni mali ya serikali, hivyo wakati wowote serikali inapoihitaji hiyo ardhi sehemu fulani inaichukua kwa kuwafidia waliopo (sio wakati wote). Pia niliwahi kusikia kuwa miji yote ina kitu kinaitwa "MASTER PLAN", ambayo inaonyesha kila eneo na matumizi yake kama vile; maeneo ya makazi, viwanda, huduma za jamii, hifadhi, maeneo ya hatari, nk. Hata hivyo natambua kuwa serikali yetu inayo maafisa pamoja na kada zingine; maafisa ardhi wapo kila halmashauri na manispaa. Niliwahi kuelezwa kuwa kando kando ya barabara ya Mandela (DSM) kuanzia Ubungo hadi Buguruni lilitengwa kwa ajili ya viwanda na sio makazi kama ilivyo sasa.

Kutokana na hayo hapo juu, nina maswali yafuatayo kwa atakayehusika;
1. Master Plan iliyopo haitekelezwi?
2. MAster Plan iliyopo au iliyowahi kuwepo ni siri kwamba wananchi hawapaswi kuifahamu?
3. Wanapoanza ujenzi watu katika eneo fulani ambalo lina mpango mwingine, wahusika wanakuwa wapi hadi ubomoaji unatokea?
4. Kwanini ofisi zetu ndogondogo za mtaa zisishirikishwe katika kila mpango uliopo katika eneo lao?

Wasalaam









eneo kuanzia
 
Wakiziweka wazi hizi Master Plan itakuwa vigumu kwao kufanya ufisadi wa ardhi na ndio maana wanazificha kwa staili ile ile ya seikali kuficha mikataba inayoingia kwa niaba ya wananchi!!
 
Mama Tiba, anayo original Master plan ya jiji wasiliana nae ......
 
Masterplan ziko wazi sema hazifuatwi na seriakali wala wananchi, nimeshangaa niligoogle ya mwisho ni ya mwaka 1979 inaonyesha maeneo hayo uliyotaja kama mashamba. Jaribu kusearch zipo ila hazifuatwi kabisa. Ila nilisoma gazetini kuwa msimame kujenga maana wanatoa mpya hiyo sikuiona. mama Tiba unamaanisha Anna Tibaijuka? basi tusubiri walisema inatoka mwezi March
 


Asante sana Safari ni Safari kwa hiki kitu angalau kinatupa picha japo ni ya long time kidogo (1992) Ngd Kyessi aliitumia 2002. Naamini kuna mabadiliko makubwa sana kwa sasa katika jiji na DSM na majirani zake hususan katika makazi ya watu.
 
Asante sana Safari ni Safari kwa hiki kitu angalau kinatupa picha japo ni ya long time kidogo (1992) Ngd Kyessi aliitumia 2002. Naamini kuna mabadiliko makubwa sana kwa sasa katika jiji na DSM na majirani zake hususan katika makazi ya watu.

Huyo Kyessi ni source lakini hii ni updated one. See hata Mabwe pande imeingizwa pia ambayo 2002 haikuwemo.
 
Kwa uelewa kidogo nilionao, kuna baadhi ya maeneo mfano Kibamba, ukienda kwa Afisa mtendaji masterplan ipo ... although utekelezaji ni kweli si wakuridhisha! Baada ya kununua eneo tulitakiwa kulipa gharama kwa ajili ya 'Mpango Mji' ili kupimiwa na kupatiwa hati athough toka Nov last year hadi leo hela imedumbukia Bank na wapimaji wameingia mjini ... wanasema tuendelee kusubiri wapimaji na mawe ya mipaka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…