DaudiAiko
JF-Expert Member
- Dec 2, 2012
- 372
- 310
Wanabodi,
Katika kipindi hiki, mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu, uchaguzi utakaotupa fursa kama wananchi kutafakari masuala mbalimbali yanayotuhusu kisiasa na kimaendeleo, hatuna budi kupasua kichwa tukiwaza jinsi ambavyo kama nchi tunaweza kujikwamua kutoka kwenye hali tuliyonayo sasa hivi.
Utagundua kwamba mbali na kura yako moja kama silaha, tumaini la kuwa na ushawishi wa kutosha kwenye maamuzi nyeti kwenye uendeshaji wa nchi yako ni finyu. Ukitilia hayo maanani, utakuwa na muonekano badala utakao kufanya uelewe kwamba “Miradi ya kimkakati” inachangia kidogo sana katika suala zima la kuikwamua serikali kiuchumi. Miradi hii inaweza ikaleta ahueni kwa wananchi kwa kupata huduma mbalimbali ambazo hazikuwepo katika kipindi cha awali lakini bado Tanzania ni nchi masikini na yenye wananchi wengi wenye kipato cha chini sana.
Niliyoeleza yana dhihirisha kwamba walio katika nafasi za juu serikali wanaweza wakawa wanatupooza kwa kutukumbusha kuhusu miradi ya kimkakati wakati kiini cha matatizo ya taifa kina uhusiano mdogo na miradi hiyo.
Tujiulize je, nchi yenye walipa kodi milioni mbili tu inawezaje kujikwamua kiuchumi?. Je uchaguzi ujao utatuletea viongozi na mipango ambayo itakuwa “Business as usual” au kuna “Risks” ambazo serikali itachukua kututoa tulipo sasa?. Je bajeti ya serikali ita fadhiliwa kwa misaada mpaka lini?.
Ninavyosema “Risks” nina maanisha kwamba serikali inaweza kuwekeza kwenye shughuli zinazo iingizia kipato wakati ikifanya miradi ya kimkakati. Katika hili, serikali haita tegemea kodi za wananchi tu kwasababu ya kipato hiki mbadala.
Inaweza ika “Monopolise” baadhi ya masoko nchini na kutengeneza bidhaa zinazo uzika kwa wananchi, au kutoa huduma ambazo haziwezi kutolewa na wafanyabiashara ilhali tuwe na serikali ambayo ni “active” na haitegemei mapato kutoka kwa walipa kodi tu. Hili pamoja na mambo mengine yanayoweza kufanywa yatahitaji ubunifu wa hali ya juu na ni risk kubwa kutekeleza. Cha muhimu kuelewa ni kwamba risk hizi zisipofanywa, tutabaki pale pale tulipo na hakuna kitakacho badilika
Mwisho, tuwe makini na ahadi tunazo pokea kutoka kwa wanasiasa kwasababu mara nyingi wanachotaka kutekeleza hakitatui kiini cha matatizo tuliyonayo.
Tuwe makini kwasababu maamuzi yetu hutiliwa maanani mara moja tu ndani ya miaka mitano. Nina amini kwamba tukitatua fumbo hili tutakuwa na mawaidha ya kutupeleka mbali sana.
Je Serikali ya Tanzania inaweza kuchukua hatua zipi kujiongezea kipato na kujikwamua kiuchumi?