Mipango

Jpinduzi

Senior Member
Joined
Feb 26, 2011
Posts
136
Reaction score
68
Maisha yaliyofanikiwa yana mizizi imara katika Mungu, na yanashamiri kwa utukufu wake. Kupata mwelekeo sahihi, ambao utafanya maisha yako yawe ya faida,ili kufanikisha maisha haya yatupasa kuwa na mipango thabiti katika maisha yetu.Hebu jiulize yafuatayo
Ni nini hasa ninachotaka kufanya?
Ni kwanini ninataka kufanya jambo hili?
Ni wapi hasa ninakotaka kufanyia jambo hili?
Ni lini nitakapoanza na ni lini nitakapomaliza?
Ni nani atakayenisimamia, kufanya kazi pamoja na mimi; na ni nani atakayenufaika na mpango wangu?
Ni kwa namna gani nitatekeleza kazi hiyo? Hatua ya kwanza, ya pili, n.k.
Ni nini gharama yake? (Lk 14:28,29).
Baada ya kujiuliza maswali hayo na kuyapatia majibu, unaweza kutekeleza yafuatayo!

Kwa sababu imani bila matendo imekufa. Uwe tayari kutumia muda wako, nguvu zako, maombi, fedha, hadhi, na heshima ukijua kwamba utendaji kazi kwa bidii huleta faida (Mit 14:23). Usisahau kupokea ushauri mwingi na kujifunza kutoka kwa wengine. Fanya tathmini ya maendeleo kila baada ya miezi mitatu na mwaka mmoja na kufanya mabadiliko yo yote ya lazima.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…