Miquissone na Ripoti ya CAG kwa Triple C

Albinoomweusi

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2016
Posts
3,433
Reaction score
8,585
Kaka ripoti imesomwa, kuna vitu kadhaa ila nikutoe hofu kwenye Wizara yetu ya Burudani, michezo na Anasa kwanza tumepewa hati safi, hesabu zimekaguliwa vyema na bajeti imeendana na mahitaji.

Ripoti inasema Kaka Chama ulinunuliwa kwa kiasi kadhaa kutoka nchini Zambia, malipo ya Simba kwenda Dynamos yaliidhinishwa na bunge la soka, kisha stakabadhi zote za malipo na risiti ya EFD alirejea nayo Afisa Magori, wakiokoa zaidi ya billion 3 za kusajili watumishi hewa kutoka Afrika Magharibi.

Kwenye kipindi cha miaka mitatu CAG anasema umechangia sana pato la nchi, watu wameingia sana uwanjani Kaka Chama, ikapelekea pia kufaulu sana kwa mfumo wa tiketi za Elektroniki, mambo yameenda vizuri, umerejesha sana na sasa unatoa Gawio, itasaidia huduma za afya.

Ripoti ya CAG ilipitia muamala wangu pia mimi LUIS MIQUISSONE, kwanza Afisa Manunuzi alikuwa na shaka baada ya Mamelodi kutonipa nafasi, hawakuamini kama kuna ghafi kutoka Kusini inaweza kutamba Afrika Mashariki, malipo yaliidhinishwa ila kufeli kwangu angetumbuliwa mtu.

Kaka leo hati safi wamepewa tena Simba, Matumizi mazuri ya Kodi na jasho la Wanasimba, wanadai kiwango changu kimefanya mabao yale muhimu Simba izidi kupiga hatua, Mama Ntilie wanapika nje ya uwanja, Wauza jezi wanauza nje ya uwanja na wanalipa Kodi TRA.

Lakini usisahau pia Ripoti imepitia mradi ya RALLY BWALYA, huu ni mradi kama wa SGR huyu bwana ameokoa matumizi makubwa ya madaw kutoka MSD, kipaji chake adhimu kimefanya Wagonjwa wapone bila panadol, hivyo kuokoa mabox takribani 3,600 na kuiepusha serikali na hasara.

Ripoti ya CAG pia wameipa Simba hati safi, ile VISIT TANZANIA imesaidia kuokoa mamilioni ya shilling ambayo yangetumika kuwalipa watu, Simba inatangaza uchumi wa Tanzania bure kabisa na hivyo kuchangia kwenye ukuwaji wa pato la Taifa[emoji6]..

Japo kidogo ripoti inapitia pitia mkataba wa Junior Lokosa na Peter Muduhwa, CAG angetamani kidogo kujua vitu kiundani inakuwaje kuwaje, japo nami sikumsikia vizuri sana nilikuwa nachaji simu[emoji3].

 
Creativity with high capability, congrtas bravo
 
Atuchekie na ripoti ya Mugalu tukimnunua kwa pesa ngapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…