Miradi inaendelezwa na awamu ya 6, hakuna kulala

Miradi inaendelezwa na awamu ya 6, hakuna kulala

Rashda Zunde

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2022
Posts
204
Reaction score
231
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeanza mchakato wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Ntorya hadi Madimba lenye urefu wa kilomita 35.

Mchakato huo umeanza kwa kufanya mkutano wa uhamasishaji kwa wananchi wa kata ya Madimba, Moma, Mbawala na Nanguruwe kuhusu ujenzi wa mradi huo ambao utaanzia kijiji cha Ntorya.

Awamu ya 6 inazidi kutuhakikishia kwamba inaendeleza miradi yote hakuna kitu kitaachwa nyuma.
 

Attachments

  • ujenzipiiic.jpg
    ujenzipiiic.jpg
    23.9 KB · Views: 5
Unasema “miradi” halafu unataja mmoja wa kilometa 35 tu?? Ninadhani ungeeleza kwanza SGR, JNHPP inaendeleaje! Sasa hivi haisikiki tena, je hakuna tarehe nyingine ya miradi kuisha?

Katika hali ya kawaida, kwanini tunakuwa na miradi mingi ambayo inafanywa nusu nusu katika wakati mmoja?? Najua utasema ni miradi inayosimamiwa na taasisi tofauti so hakuna haja ya kusubiriana - je iko hivo katika financing pia? Kwamba wafadhili ni tofauti?? Au ni serikali hii unayoisifia?

Kizazi cha kusifiasifia tu bila kuhoji! Bogus!
 
Back
Top Bottom