Mradi pekee wa maana tunaotaka uulete ni mradi utakaoinua vipato vya Watanzania wa tabaka la chini (masikini) na kuwapa uwezo wa kuingia kwenye tabaka linalofuata la juu (lifting people out of poverty), na tupewe idadi yao kwa kila baada ya miaka mitano.
Hawa wakishakuwa na "increased spending power" ndiyo tunaweza kuanza kujadili habari za maendeleo. Zaidi ya hapo hiyo miradi yako ni maendeleo ya barabara na flyovers vitu ambavyo havimpi mtu yeyote wa chini mbadala wa maisha anayoishi.
Hili jambo serikali zote zilizopita zimeshindwa, huyu wa sasa naye anapita mle mle kwa hiyo hakutakuwa na tofauti hata atawale miaka elfu kumi.
Chupa tu ndiyo iliyobadilika na kuapishwa November 5, 2015 lakini mvinyo ni ule ule.