Miradi Mipya ya Elimu Jimbo la Mufindi Kaskazini

Miradi Mipya ya Elimu Jimbo la Mufindi Kaskazini

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301

NAIBU WAZIRI EXAUD KIGAHE AKAGUA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA MADARASA JIMBO LA MUFINDI KASKAZINI

Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe tarehe 29 Julai, 2023 mpaka tarehe 30 Julai, 2023 amefanya ukaguzi wa ujenzi wa Madarasa, Vyoo na Nyumba ya Mwalimu Jimboni kwake.

Mhe. Kigahe amekagua Ihefu Sekondari, Shule mpya ya Wanafunzi walioanza masomo Mwaka 2023 iliyojengwa kwa Shilingi Milioni 160. Pongezi ziende kwa Serikali ya awamu ya Sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mbunge Exaud Kigahe, Diwani Ernei Nyeho, Wananchi na wadau wote kwa namna moja ama nyingine.

Mhe. Kigahe amekagua ujenzi wa Matundu 14 ya Vyoo Shule ya Msingi Kinyimbili iliyopo Kata ya Mdabulo yaliyojengwa kwa gharama ya Shilingi Milioni 38.25 kwa chanzo cha Fedha za Boost.

Mhe. Kigahe amekagua ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu 2 in 1 shule ya msingi Kinyimbili ambapo chanzo cha fedha ni kutoka Serikali Kuu Milioni 30 kwa ajili ya ukamilishaji yaani kupaua, Plasta, Rangi na Marumaru, Msingi, Rinta na tofali ni nguvu ya Wananchi na Mhe. Kigahe alitoa Saruji Mifuko 26 na fedha Shilingi Milioni 1.2

Mhe. Kigahe amefanya ukaguzi wa ujenzi wa madarasa Manne na Ofisi Mbili umekamilika ambapo gharama ya mradi ni Milioni 80, Ni sambamba na ujenzi wa Vyoo Matundu 17 yenye gharama ya Shilingi Milioni 38.25 kwa chanzo cha fedha ni Serikali Kuu
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.13.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.13.jpeg
    123.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.14.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.14.jpeg
    128.6 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.19(1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.19(1).jpeg
    96.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.32.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.32.jpeg
    106 KB · Views: 5
  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.30.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.30.jpeg
    141.4 KB · Views: 4
  • WhatsApp Video 2023-07-31 at 07.14.28.mp4
    4.2 MB
  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.27.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.27.jpeg
    70.8 KB · Views: 7
  • WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.19.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-31 at 07.14.19.jpeg
    152.1 KB · Views: 8
Mama Samia, The Mother of Modern Tanzania, anawapelekesha hawa jamaa si mchezo..........ni maendeleo tu kila pembe!!
 
Back
Top Bottom