Miradi Wa Nyangaza Kutoa Ajira 1500

Miradi Wa Nyangaza Kutoa Ajira 1500

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Mradi wa uchimbaji mkubwa wa dhahabu uliopo Nyanzaga - Sengerema unatarajiwa kuanza kazi za awali za ujenzi wa mgodi ifikapo Januari, 2025.

Hayo yamebainishwa leo Oktoba 11 , 2024 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde, wilayani Sengerema katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Igalula, Boma na Ibisabageni baada ya kutembelea eneo la mgodi kwa lengo la kupokea na kutoa maelekezo juu ya kutatua changamoto mbalimbali zilizoibuliwa na wananchi.

Akielezea kuhusu mpango wa ajira kutoka sehemu ya mgodi, Waziri Mavunde amesema kuanza kwa mradi kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 1500 na hivyo, ameielekeza Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya kuweka utaratibu mzuri wa kupokea barua za maombi ya ajira kupitia wenyeviti wa vitongoji na kuwasilisha kwa Mtendaji wa Kata ili kupata orodha ya ajira iliyosahihi na uwazi.

Sambamba na hilo, Waziri Mavunde ameielekeza kampuni ya Sotta kutumia mpango wa ushirikishwaji wa Jamii inayozunguka mgodi (CSR) kama Sheria inavyoelekeza kwa kuwashirikisha wananchi katika uibuaji miradi mbalimbali ya kiuchumi inayotokana na mgodi kama kanuni zinavyoelekeza.

Vilevile, Mhe. Mavunde alibainisha kwamba Serikali ambaye ni mbia wa mgodi huo na kampuni ya Perseus kupitia kampuni ya ubia ya Sotta kwa mara ya kwanza inakwenda kunufaika kupitia kuongezeka kwa hisa za Serikali zisizofifishwa (Undiluted Free carried Interest) kutoka asilimia 16 hadi asilimia 20.

Waziri Mavunde amefafanua kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inatambua umuhimu wa wananchi kushiriki katika uchumi kupitia sekta ya madini na hivyo kutoa rai kwa wananchi kuchangamkia fursa za mauzo ya bidhaa na kutoa huduma migodini kwa kuitaka Tume ya Madini kuwajengea uwezo wananchi hao juu ya ushiriki wao kwenye zabuni mbalimbali.
 
Migodi inapiga hela sababu kwa sasa bei ya dhahabu kwa wakia moja ni kubwa sana
 
Back
Top Bottom