Abdalah Abdulrahman
JF-Expert Member
- Aug 29, 2019
- 222
- 202
Janga la corona limetikisa dunia kwa kusababisha taharuki na vifo vya watu zaidi ya laki tatu, kusababisha mdororo wa uchumi kwa kusimamisha uzalishaji, kupunguza ajira na madhara mengine mengi kwa binadamu.Hizi ndizo athari za muda mfupi tunazoweza kuziongelea kwa sasa,athari za muda mrefu zinazotokana na janga hili kwenye uchumi na kijamii zinaweza kuleta matokeo mabaya zaidi.
Tanzania imejiainisha kupambana na janga hili kwa mbinu tofauti tofauti kulingana na mazingira pamoja na hali ya uchumi wa nchi kwa lengo la kuwalinda wananchi wake wasipate madhara yanayotokana na janga la ugonjwa huu sasa hivi na hapo baadae.Mbinu ambazo Tanzania imeamua kuchukua kupambana na janga hili zinatoa matokeo mazuri zaidi ukilinganisha na njia zingine ambazo zina madhara makubwa kwa wananchi.
Miongoni mwa vigezo vilivyozingatiwa na Tanzania na baadhi ya nchi zingine duniani kuchagua njia hizi katika kupambana na janga hili ni kama zifuatazo:
Ugonjwa wa korona kuishi na binadamu muda mrefu
Ugonjwa wa corona kama virusi vya Ukimwi vilishaonekana kuwa vitakaa muda mrefu bila kupatiwa kinga na dawa,hivyo ilikua ni muhimu kwa watu kujiweka tayari kuishi na virusi hivi kwa kuchukua tahadhari na sio kujifungia ndani na kusababisha madhara makubwa zaidi. Raisi John Pombe Magufuli kwa kutumia wataalamu wake ambao ni wazalendo aliamua kuchukua njia sahihi kuliendea hili janga na faida zake zinaonekana wazi. Nchi za Ulaya sasa hivi zimeamua kuchukua njia hii kwa kuita kulegeza masharti baada ya kugundua madhara ya njia ya kuwafungia wananchi wake ndani.
Taarifa za janga la corona
Kwa kuzingatia kuwa ugonjwa wa corona ulikua umeshasambaa katika nchi tofauti kabla hata ya kutangazwa na WHO katika nchi husika ni wazi kuwa kulikua na kila dalili kuwa ugonjwa huu ulikuwepo pia nchini na hivyo kutumia mbinu ya kuwafungia watu ndani kungesababisha madhara makubwa kwa wananchi.Mfano madaktari nchini uingereza na Marekani wamegundua wagonjwa wa corona waliofariki kabla ya ugonjwa kutangazwa kuingia katika nchi hizo.
Uwezo wa kupima wananchi
Uwezo wa seriakli kuwapima wanachi takriban milioni 55 kwa kipindi kifupi ili kujiridhisha juu ya maambukizi ni changamoto kubwa ukilinganisha na idadi ya vifaa na maandalizi katika hili janga.Tukumbuke kuwa mataifa mengi tajiri yalikua yamepandisha bei za vifaa vya kupima na kuhakikisha vifaa vilivyopo vinatosheleza kwanza mahitaji ya nchi zao.Hivyo kutokuwapima watu na kuwafungia ina madhara makubwa kuliko kuwaachia watu,kwani watu wakiwa huru wataweza kufanya mazoezi,kula vizuri na kutibu dalili za ugonjwa na hivyo kuwa salama.
Uchumi wa wananchi
Ni wazi kuwa Tanzania ina raia wenye uwezo tofauti,wapo wananchi wenye uwezo wa kununua na kuuza,kusoma na kufanya kazi kwa njia ya mtandao,wapo wasioweza kupata huduma hizi kwa kutumia Teknolojia.Pia wapo wanach wenye uwezo wa kununua mahitaji ya miezi mitatu na wapo wanaoweza kununua mahitaji ya siku.Kitendo cha kuwafungia ndani wanachi hawa ni kitendo cha kinyama ambacho kingesababisha madhara makubwa kwa wanchi wa hali ya chini.
Licha ya mazingira yaliyoaninishwa hapo juu,pia mafanikio ya hatua ambazo Tanzania ilizochukua na kuleta matokeo mazuri ukilinganisha na baadhi ya nchi zingine yanatokana na uwekezaji mzuri katika miradi ya kimkakati na uongozi imara wa Raisi John Pombe Magufuli.
Baadhi ya miradi ya kimkakati ambayo imechangia kupunguza athari za ugonjwa huu kwa Watanzania ni kama ifuatayo:
Miundombinu mizuri ya huduma za afya
Serikali ya awamu ya tano imefanikiwa kuimarisha huduma za afya ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa dawa,vifaa tiba na wataalamu nchi nzima.Serikali kwa kipindi cha miaka mine ya utawala wa Raisi John Magufuli imeajiri zaidi ya watumishi 13479 na ujenzi wa hospitali na vituo vya afya vinavyokadiriwa kufikia 7,980 zikiwemo ukarabati wa hospitali za rufaa 23. Uwepo wa huduma hizi za afya umesaidia kutoa huduma bora kwa wananchi katika nyanja ya afya.
Miundombinu ya barabara, maji, na umeme,Tehama
Barabara, maji, umeme, mawasiliano ni nyenzo muhimu sana katika kuhakikisha huduma muhimu za kijamii zinawafikia wananchi. Ni wazi kuwa baada ya safari za ndege kutoka nje kufungwa bado huduma muhimu kwa wanchi zinaendelea kupatikana.
Uwajibikaji wa watumishi wa umma
Serikali ya awamu ya tano imejenga nidhamu na uwajibikaji mzuri kwa watumishi wa umma,huduma mbalimbali zimekua zikitolewa kwa wakati bila urasimu.Watumishi tofauti na nchi zingine wamekua wakiwatumikia wananchi na kutotumia janga la corona kama kitega uchumi.
Taharuki ambayo ugonjwa huu umeleta inanifanya na mimi nitoe ushauri wangu kwa serikali pamoja na Watanzania kwa ujumla kama ifuatavyo:
Ugonjwa wa Corona umejenga dhana ya umuhimu wa nchi kujitegemea
Tumeshuhudia miaka kufungwa na makatazo ya watu kuingia ni kutoka nchini, hali hii ingekua mbaya zaidi kama serikali ya awamu ya tano isingeweka misingi imara ya kuwekeza kwenye miradi ya kimkakati. Ushauri wangu ni serikali kumalizia hii miradi na kuwekeza zaidi kwenye viwanda vya mahitaji ya lazima pamoja na kilimo.
Machanganyiko wa masomo kupitia njia za Tehama na ana kwa ana
Serikali iimarishe mfumo wa elimu kwa kuweka mifumo ya Tehama vijijini ili kuwezesha wanafunzi kupata elimu kupitia mitandao. Hili liende sambamba na kuimarisha huduma za umeme vijijini na kuwaweka wananhi karibu na huduma muhimu.
Kuanzisha huduma za kujifungulia nyumbani, kliniki za watoto nyumbani
Kuanzisha huduma za kijamii zinazotembea(mobile services) mfano matibabu, cliniki, kujifungua, vikundi vya dharura, na mambo mengine ambayo yatamuweesha mwananchi kupata huduma muhimu hata akiwa nyumbani.
Madhara ya kuwafungia wananchi ndani
Nchi ambazo zilichukua mbinu ya kuwafungia wanchi wake ndani zilikua na madhara makubwa kwa watu wake hasa kwa nchi maskini ambazo watu wake wanategemea kipato cha siku kuendesha maisha yao. Miongoni mwa watu walio athika kwa kiwango kikubwa ni kina mama,watoto na walemavu na watu maskini.
Kuwafungia watu ndani kama anavyosema Profesa Narendra Nath Tikader unafanywa na serikali ambazo hazitaki kuwajibika kuwalinda wanachi wake na maradhi kwa kuondoa wajibu wa kuwahudumia kwa matibabu ya dalili za corona.Watu wengi watakufa na ugonjwa kuambukiza kwa kuwafungia watu ndani.
Vile vile wachambuzi wa mambo duniaani wanaeleza kuwa nchi zenye watawala mafisadi zimelipokea janga hili la corona kama fursa ya kuiba mali za umma kwa kukiuka taratibu za manunuzi pamoja na kuvunja haki za binadamu, mifano ya uvunjifu wa haki za binadamu kwa nchi za Afrika ni mingi ikiwepo Kenya ambapo Polisi wamempiga risasi mtoto mdogo ambaye alikua ametoka nje kipindi hiki cha corona.
Serikali hizi zimekua zikitia watu wake hofu ili kuendelea kupokea misaada kutoka mashirika ya kimataifa kama vile IMF, WHO na mengine na kutumia hii misaada kwa manufaa yao.
Wito kwa Watanzania ni kuendelea kufanya kazi na kuchukua tahadhari juu ya ugonjwa huu hatari wa corona kwa manufaa yetu na kwa nchi yetu.
Mungu ibariki Tanzania, Mungu mbariki Raisi Magufuli, Mungu wabariki Watanzania kwa ujumla.